Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,008
Kwanini hakusubiri? Ingekuwaje kama angejaribu kusubiri hadi jumla ya matokeo yote itolewe? Buhari na kundi lake walikuwa na wenyewe wanakusanya matokeo na hivyo waliona walichoona AP na wengine.
Hili inabidi liache swali - rejea mada yangu ya kukusanya matokeo - upinzani na vyombo vyetu vya habari vinafanya nini kujiandaa kukusanya matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kusubiri na kutegemea Tume ya Taifa ya UChaguzi? Au na wao watafanya tena walichofanya 2010 kwamba wataka chini kusubiri TUme iwatangazie matokeo "rasmi"?