Swali la Kizushi: Kwanini Buhari Hakusubiri Matokeo Rasmi Kutangaza Ushindi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
buhari.jpg

Tume ya Uchaguzi ya Nigeria iliwaasa Wanigeria na vyombo vya habari kutokutoa matokeo ya uchaguzi hadi yatakapotazwa rasmi na tume hiyo. Hata hivyo hilo halikuzuia vyombo vya habari hasa Associated Press kukusanya matokeo na kutangaza kwa kadiri walivyokuwa wanayapata. Matokeo yake kabla ya Tume kutangaza rasmi ilishaoneokana Buhari alikuwa anaongoza kwa mbali. Hiki kilimfanya Buhari kutangaza ushindi mapema na kuanza kusherehekea hata kabla ya Tume kutangaza rasmi.

Kwanini hakusubiri? Ingekuwaje kama angejaribu kusubiri hadi jumla ya matokeo yote itolewe? Buhari na kundi lake walikuwa na wenyewe wanakusanya matokeo na hivyo waliona walichoona AP na wengine.

Hili inabidi liache swali - rejea mada yangu ya kukusanya matokeo - upinzani na vyombo vyetu vya habari vinafanya nini kujiandaa kukusanya matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kusubiri na kutegemea Tume ya Taifa ya UChaguzi? Au na wao watafanya tena walichofanya 2010 kwamba wataka chini kusubiri TUme iwatangazie matokeo "rasmi"?
 
Cha msingi na vyombo vyetu vikusanye utani bila vitisho na kutangaza matokeo bila kusubiri matokeo ya nec ya kupigwa yasio ainisha kura za kituo na kituo wala jimbo kwa jimbo ili w3zi wa kura
 
Mzee Mwanakijiji

Mwanakijiji kabla ya kujibu swali niweke dokezo kidogo. General amefanya ujanja kwa kusema ameongea na Jonathan ambaye amekubali kuwa ameshindwa. Ukiangalia ufundi wa maneno hayo unaweza kuona kuwa ni hajavuka mstari wa tume ya uchaguzi kujitangaza mshindi, ni kama anasema Jonathan amemtangaza kuwa mshindi. Ukiangalia kwa undani unaweza kugundua kuwa wagombea wote wawili wamekosea.

Ukiangalia ballot boxes za Nigeria, utaratibu wa kuhesabu kura zilikopigiwa na kuthibitihswa na wawakilishi, na uhuru wa vyombo vya usalama kutoka kwenye minyororo ya chama tawala, unaweza kuona kuwa vimeweka msingi imara wa mwamko wa wanigeria.

Kitu kingine ni kuwa kuiba kura Nigeria si rahisi. Hapa Tanzania ni rahisi na watu wanakaa kimya, Nigeria ungekuwa muziki mkubwa.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji Hivi unataka kutuaminisha kuwa Tanzania tuna tume huru ya uchaguzi? Kwa hiyo kama tume ingetangaza matokeo kuwa Jonathan Goodluck ameshinda hao AP wangekuwa kwenye matatizo, kwa bahati nzuri mkuu wao hana akili za jaji Lubavu. Ameona mbali na ametumia akili zake zilizo sahihi na kukubaliana na ukweli.

Nafikiria kama ingekuwa Tanzania AP na wapinzani ndio wanazijumlisha hizo na kupata ukweli wa hali hali, sijui ingekuwaje na CCM wangeingiza jeshi lao mitaani tayari kwa vita, au serikali ya mseto.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwanakijiji kabla ya kujibu swali niweke dokezo kidogo. General amefanya ujanja kwa kusema ameongea na Jonathan ambaye amekubali kuwa ameshindwa. Ukiangalia ufundi wa maneno hayo unaweza kuona kuwa ni hajavuka mstari wa tume ya uchaguzi kujitangaza mshindi, ni kama anasema Jonathan amemtangaza kuwa mshindi. Ukiangalia kwa undani unaweza kugundua kuwa wagombea wote wawili wamekosea.

Ukiangalia ballot boxes za Nigeria, utaratibu wa kuhesabu kura zilikopigiwa na kuthibitihswa na wawakilishi, na uhuru wa vyombo vya usalama kutoka kwenye minyororo ya chama tawala, unaweza kuona kuwa vimeweka msingi imara wa mwamko wa wanigeria.

Kitu kingine ni kuwa kuiba kura Nigeria si rahisi. Hapa Tanzania ni rahisi na watu wanakaa kimya, Nigeria ungekuwa muziki mkubwa.

Mbona hakukanusha kusema hakumpigia simu mpinzani wake? wachakujipa moyo Bongolander. Jonathan amekubali huku akijua kuwa hana chake. Next stop to Tanzania october lazima haya majambazi yaliovamia CCM na kujifanya wanasiasa lazima yang'olewe. Tanzania ni ya Watanzania sio ya watu wachache wanojificha kwenye mwamvuli wa siasa wakati ni majambazi na mauaji. Serikali ya Tanzania inaongozwa na ma-criminal
 
Mzee Mwanakijiji naweza kusema hii mada ni muendelezo tu wa ile ya jana, ila leo tuna na mfano hai. Watawala wameshayaone haya kwa darubini ya mbali.

Wanajiandaa... Kutaa ubeberu wao ni juu yetu wananchi... No free lunch.
 
Last edited by a moderator:
buhari.jpg

Tume ya Uchaguzi ya Nigeria iliwaasa Wanigeria na vyombo vya habari kutokutoa matokeo ya uchaguzi hadi yatakapotazwa rasmi na tume hiyo. Hata hivyo hilo halikuzuia vyombo vya habari hasa Associated Press kukusanya matokeo na kutangaza kwa kadiri walivyokuwa wanayapata. Matokeo yake kabla ya Tume kutangaza rasmi ilishaoneokana Buhari alikuwa anaongoza kwa mbali. Hiki kilimfanya Buhari kutangaza ushindi mapema na kuanza kusherehekea hata kabla ya Tume kutangaza rasmi.

Kwanini hakusubiri? Ingekuwaje kama angejaribu kusubiri hadi jumla ya matokeo yote itolewe? Buhari na kundi lake walikuwa na wenyewe wanakusanya matokeo na hivyo waliona walichoona AP na wengine.

Hili inabidi liache swali - rejea mada yangu ya kukusanya matokeo - upinzani na vyombo vyetu vya habari vinafanya nini kujiandaa kukusanya matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kusubiri na kutegemea Tume ya Taifa ya UChaguzi? Au na wao watafanya tena walichofanya 2010 kwamba wataka chini kusubiri TUme iwatangazie matokeo "rasmi"?

Sisi nchi yetu ni watii Sheria tulizojiwekea na tunaheshimu Dola na mamlaka zake, hivyo kama Wanigeria wao hawaheshimu Dola yao hiyo ni shauri yao lakini usitake kutupeleka huko! Hapa TZ tuna chombo cha kusimamia karibu kila kitu kuanzia chombo kama EWURA mpaka tume ya Uchaguzi na itabaki kuwa hivyo kwani hata Wapinzani nao wakiingia madarakani pia hawatapenda Chama cha Upinzani kikiuke taratibu!
 
ukiwa umevuka lengo ukijitangaza si vibaya ata kama kura zinahesabiwa,Marekani mshindi wa urais anajulikana wakat kura zikiendelea kuhesabiwa dakika ya mwisho.Inategemea na unaongoza kwa asilimia ngapi na kura ambazo hazijahesabiwa ni asilimia ngap

Ndio maana ata mpira kwenye penati penati wakat mwingine team inasherekea ushindi ata kabla ya kumaliza penati zote,utegemea team imepata ngap na kupoteza ngap
 
Tanzania masanduku yenye kura yanabebwa na JWTZ nani anathubutu kuwauliza maswali?
 
Tanzania ni vigumu wananchi kulinda kura kwa ajili ya mgombea yeyote kwakuwa wote hawaaminiki..wezi na waongo
 
Sisi nchi yetu ni watii Sheria tulizojiwekea na tunaheshimu Dola na mamlaka zake, hivyo kama Wanigeria wao hawaheshimu Dola yao hiyo ni shauri yao lakini usitake kutupeleka huko! Hapa TZ tuna chombo cha kusimamia karibu kila kitu kuanzia chombo kama EWURA mpaka tume ya Uchaguzi na itabaki kuwa hivyo kwani hata Wapinzani nao wakiingia madarakani pia hawatapenda Chama cha Upinzani kikiuke taratibu!

Nigeria hawana vyombo vya kusimamia kila kitu? Kati ya Tanzania na Nigeria ni lipi Taifa lenye nguvu zaidi? Acha porojo zako,uoga wa Watanzania ndio unafanya watawala wafanye hizo sarakasi wakati wa kutangaza matokeo( sitasahau staili ya utangazaji matokeo 2010).Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu,kwa Nigeria wangejaribu kuiba kura mziki wake ungekuwa mnene!
 
Kama matokeo yanayotangazwa ni halisi kutoka vituoni kuna shida gani mpaka watu wasubiri tume inayofanya kazi kigoigoi? Kama wewe ndio ulikuwa na wenzako mnategemea tume iwape ushindi na sio matokea halisi toka vituoni safari hii hatukubali. Tume imetumika mara nyingi kutoa matokeo tofauti na kwenye vituo vya kura na bado unadhani watu wataendelea kuiamini tume ambayo sio huru. Kama mnataka watu wasubiri matokeo ya tume ni lazima iwe huru na washindani wote waridhike sio tume hii inayopokea maelekezo toka lumumba. Safari hii kazi mnayo na wale viongozi wa dini wameshawastukia kuhusu kuombea nchi amani wakati mnaiba kura kimachomacho kwenye kwenye BMK, hii imekula kwenu.
 
Kama wao (Nigeria) wanavyo vyombo vya kusimamia kila kitu na bado hawaviheshimu hilo ni tatizo lao lakini kwetu ni HAPANA, hapa TanZania Mshindi wa Uchaguzi anatangazwa na Tume iliyopo Kikatiba!
 
Kama matokeo yanayotangazwa ni halisi kutoka vituoni kuna shida gani mpaka watu wasubiri tume inayofanya kazi kigoigoi? Kama wewe ndio ulikuwa na wenzako mnategemea tume iwape ushindi na sio matokea halisi toka vituoni safari hii hatukubali. Tume imetumika mara nyingi kutoa matokeo tofauti na kwenye vituo vya kura na bado unadhani watu wataendelea kuiamini tume ambayo sio huru. Kama mnataka watu wasubiri matokeo ya tume ni lazima iwe huru na washindani wote waridhike sio tume hii inayopokea maelekezo toka lumumba. Safari hii kazi mnayo na wale viongozi wa dini wameshawastukia kuhusu kuombea nchi amani wakati mnaiba kura kimachomacho kwenye kwenye BMK, hii imekula kwenu.

Shida ipo tena kubwa tu sana kwa maana unakuwa umefungua ukurasa wa kutokutii Sheria tulizojiwekea kitu ambacho kimetufanya tuishi vizuri na kwa amani (kwa kiasi fulani) mpaka leo hii!

Kumbuka ni kwa maslahi pia ya Upinzani pale sisi kama nchi tunabaki kuwa watii wa Dola yetu kwani hii itawasaidia hata wao Upinzani siku wakiwa madarakani kuongoza kwa Amani na Utulivu na kutekeleza sera zao bila ya bugudha kama ilivyo sasa hivi lkn unapoanza kutokutii Dola basi hata siku Upinzani wakiwa madarakani watakuwa na kzi ngumu pia!
 
Watakachofanya upinzani ni kuhakikisha kunakuwa na tume huru itakayoaminika. Usilazimishe watu kutii sheria kwenye tume inayofanya kazi kwa kupokea maelekezo toka mmojawapo ya washindani. Ila iwapo na upinzani nao watafanya kosa la kutokuwa na tume huru ya uchaguzi watakutana na tatizo hilohilo la watu kutokutii sheria.
 
Unaongelea kitu ambacho hakipo na maadamu Upinzani hauko madarakani hatuwezi kujua kama ni kweli watasimamia hiyo unayoiita tume Huru au wataendelea na hii iliyokuwepo hivyo ni muhimu kwa sasa tuendelee na utaratibu huu huu wa kutii vyombo vyetu vilivyopo na kama hatuvitaki basi tutumie njia inayokubalika kuviondoa au kuvibadilisha kama vile Bunge lakini maadamu hivi vya sasa tuliviweka wenyewe basi hatuna budi kuvitii na hivyo kazi ya kutanganza Matokeo ya Uchaguzi TanZania inabaki kuwa ya Tume ya Uchaguzi mpaka hapo tutakapoamua vinginevyo!
 
Mwanakijiji kabla ya kujibu swali niweke dokezo kidogo. General amefanya ujanja kwa kusema ameongea na Jonathan ambaye amekubali kuwa ameshindwa. Ukiangalia ufundi wa maneno hayo unaweza kuona kuwa ni hajavuka mstari wa tume ya uchaguzi kujitangaza mshindi, ni kama anasema Jonathan amemtangaza kuwa mshindi. Ukiangalia kwa undani unaweza kugundua kuwa wagombea wote wawili wamekosea.

Ukiangalia ballot boxes za Nigeria, utaratibu wa kuhesabu kura zilikopigiwa na kuthibitihswa na wawakilishi, na uhuru wa vyombo vya usalama kutoka kwenye minyororo ya chama tawala, unaweza kuona kuwa vimeweka msingi imara wa mwamko wa wanigeria.

Kitu kingine ni kuwa kuiba kura Nigeria si rahisi. Hapa Tanzania ni rahisi na watu wanakaa kimya, Nigeria ungekuwa muziki mkubwa.

BUHARI hajajitangazia ushindi bali ni vyombo vya habari vya nyumbani na kimataifa ndivyo vilinyokua vinatoa taarifa kuhusu mwenendo wa kura jinsi zinavyotangazwa ukizingatia kuwa kulikuwa na tofauti kubwa kati ya hao wawili na majimbo yaliobaki kuleta matokea ni machache ,Hata kama hayo majimbo yangetngaza kura yasingeleta tofauti kwa Buhari
 
buhari.jpg

Tume ya Uchaguzi ya Nigeria iliwaasa Wanigeria na vyombo vya habari kutokutoa matokeo ya uchaguzi hadi yatakapotazwa rasmi na tume hiyo. Hata hivyo hilo halikuzuia vyombo vya habari hasa Associated Press kukusanya matokeo na kutangaza kwa kadiri walivyokuwa wanayapata. Matokeo yake kabla ya Tume kutangaza rasmi ilishaoneokana Buhari alikuwa anaongoza kwa mbali. Hiki kilimfanya Buhari kutangaza ushindi mapema na kuanza kusherehekea hata kabla ya Tume kutangaza rasmi.

Kwanini hakusubiri? Ingekuwaje kama angejaribu kusubiri hadi jumla ya matokeo yote itolewe? Buhari na kundi lake walikuwa na wenyewe wanakusanya matokeo na hivyo waliona walichoona AP na wengine.

Hili inabidi liache swali - rejea mada yangu ya kukusanya matokeo - upinzani na vyombo vyetu vya habari vinafanya nini kujiandaa kukusanya matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kusubiri na kutegemea Tume ya Taifa ya UChaguzi? Au na wao watafanya tena walichofanya 2010 kwamba wataka chini kusubiri TUme iwatangazie matokeo "rasmi"?

Channel Ten waliwahi kufanya hivyo kwenye uchaguzi wa Zanzibar na ilikuwa dhahiri kwamba ccm walishindwa. lakini matokeo "rasmi" ikaonekana "Komandoo" ameshinda.

Mwaka huu, tusifanye makosa hayo tena. Matokeo "rasmi" ya tume yakiwa tofauti na hali halisi bora pachimbike tu!
 
Hiyo Associated Press inanikumbusha DTV mwaka 1995, walifanya walicho kifanya AP kwa kule Zanzibar na hatimae wakatangaza CUF imeshinda Zanzibar, kilichotokea Enzi hizo wote tunajua!
 
Back
Top Bottom