Swali La KIZUSHI: Kwa nini Watanzania tunafeli mitihani ya Kiswahili?

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Yaani tumezaliwa tunazungumza Kiswahili lugha ya kwanza (wengine wetu). Kila siku tunazungumza Kiswahili. Tunazungumza sana Kiswahili mpaka tunajulikana pande ile kuwa sisi ni ile mitu iko na Kiswahili-mrefu. Hatuna umahiri wa lugha zingine kama tulio nao kwa Kiswahili.

Kwa nini basi tunafeli Kiswahili? Nilitegemea watu wengi wangekuwa wanapata "A" za Kiswahili kwenye mitihani ya kidato cha nne kuliko wanaopata "A" za hisabati (Basic Mathematics.) Hata wapo wale wanaopata Divisheni Wani ya pointi saba, unakuta hawana "A" za Kiswahili.

Kulikoni?
 
Tuanze na wewe mkuu kwanini huku pata hiyo A ya kiswahili?
Mimi nilipata A
 
Kiswahili cha darasani si sawa na kile cha kuongea. Huku koromije kuna watu wanazaliwa hadi wanazeeka na kuresti in pisi bila kutaja maneno kama; sarufi, fasihi, vishazi, virai, kutohoa, kunyumbulisha, etc. Ili upige mabanda ya kiswahili lazima uwezee hayo masuala
 
Yaani tumezaliwa tunazungumza Kiswahili lugha ya kwanza (wengine wetu). Kila siku tunazungumza Kiswahili. Tunazungumza sana Kiswahili mpaka tunajulikana pande ile kuwa sisi ni ile mitu iko na Kiswahili-mrefu. Hatuna umahiri wa lugha zingine kama tulio nao kwa Kiswahili.

Kwa nini basi tunafeli Kiswahili? Nilitegemea watu wengi wangekuwa wanapata "A" za Kiswahili kwenye mitihani ya kidato cha nne kuliko wanaopata "A" za hisabati (Basic Mathematics.) Hata wapo wale wanaopata Divisheni Wani ya pointi saba, unakuta hawana "A" za Kiswahili.

Kulikoni?
Ukijua tofauti Kati ya kiswahili na somo la kiswahili utajua kwanini watu hawafeli kiswahili Bali somo la kiswahili
 
Kiswahili cha darasani si sawa na kile cha kuongea. Huku koromije kuna watu wanazaliwa hadi wanazeeka na kuresti in pisi bila kutaja maneno kama; sarufi, fasihi, vishazi, virai, kutohoa, kunyumbulisha, etc. Ili upige mabanda ya kiswahili lazima uwezee hayo masuala

hahahaha jf buana!
 
Tanzania lugha ya taifa n kiswahili lakin ninauhakika asilimia 80 hawajui kiswahiliiiiiii....nikikupa dakika tano apaa uongee kiswahili lazma utachanganya kiingereza au kikabila automatic bila wew kutambua....ndo maana darasan kiswahili n kigumu,,,,,,,,hata marekan wanaojua kiingereza ukiwapa mtihan wa english wa apa bongo lazma wascore zero ....sufuri kabisa na kiingereza chaooo
 
Back
Top Bottom