Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Niko njiani kutokea nyumbani Visiga, Kibaha mkoa wa Pwani. Jana, nilishuhudia uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za wagombea wa CCM, Mtaa wa Visiga A kwa ngazi ya Mwenyekiti na Wajumbe. Leo, uzinduzi utaendelea kwa Mitaa mingine ya Visiga B, Madafu na Maili Thelathini na Tano.
Kadiri nijuavyo, katika mitaa yote hiyo hakuna mgombea wa chama cha upinzani ambaye alichukua na kurejesha fomu au kuteuliwa kugombea. Kadiri nijuavyo, Mitaa hiyo ina wagombea wa CCM pekee.
Imezoeleka na kueleweka kwenye chaguzi kuwa endapo atabaki mgombea mmoja kwenye uchaguzi, mgombea husika hutangazwa mshindi katika kile kinachojulikana kama 'kupita bila kupingwa'. Tena hutangazwa tu na Msimamizi wa Uchaguzi husika.
Je, uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa ni tofauti? Kwenye uchaguzi huu hakuna 'kupita bila kupingwa'? Kama 'kupita bila kupingwa' kupo, kwanini kampeni zimezinduliwa na zinafanyika?