Swali la kichokozi: Wataalamu wa IT wanatolewa Rwanda,wataalamu wa viwandani watatolewa wapi?

Nchi Ya Viwanda Vya Kusadikia! Wacha Watu Waendelee na "False Hope" ya Kusubiri Viwanda.
 
Rwanda mfumo wao wa mapato ni asycuda ambao sisi tuliwacha na kwenda tancis kwa maelezo kuwa ni mpana na unakidhi sehemu zote kwa maana unaweza kuunganisha na sehemu tofauti zenye lengo moja. Sasa sijui hao wataalamu wataturudisha kwenye mfumo tuliouacha kwamba haukidhi.

Nchi ya Rwanda ni kama mkoa wa Pwani. Wao hata wakiamua kukusanya kodi manually wanaweza.
 
Tatizo la wataalamu wa hapa NYUMBANI wakitengeneza mageti makubwa(mfumo)ni lazima pia waweke tundu la kuvujishia ili waendelee kula dili,bora waje wasio na maslahi,tuacheni kupiga dili kwenye kila kitu,ndiyo maana haya yanatokea.
 
Serikali ya Tanzania ya awamu ya tano,chini Rais Magufuli,inajipambanua kama Serikali ya viwanda. Ingawa bado hakujajengwa wala kuwa na matayarisho ya kiwanda chochote,'mahubiri' ya Serikali ni nchi ya viwanda.

Hivi juzi,Rais Magufuli amemuomba Rais Paul Kagame wa Rwanda wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano ili kusuka mifumo ya ukusanyaji kodi wa TRA. Maombi hayo ya Rais yamejadiliwa,yamelalamikiwa na kusifiwa. Wataalamu wa Kinyarwanda watatua nchini muda wowote.

Kama wataalamu hao tu wanatoka Rwanda,wataalamu wa kujenga na kuendesha viwanda lukuki vitakavyojengwa nchini watatolewa wapi? Hivi,mfumo wa Rwanda wa IT aliutengeneza nani? Hivi,ni kweli Tanzania inazidiwa utaalamu na wataalamu wa IT na Rwanda?

Nchi ya viwanda,CCM mbele kwa mbele!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
TUPA TUPA MZEE UNA CHEO GANI HUKO MAGAMBANI???
 
Nadhani kunakitu kinapotoshwa. Siamini serikali inaweza achia taifa lingine isuke mifumo yake ya kitechnologia kama hili la mfumo wa ukusanywaji kodi. Hapa itakuwa wataalam toka Rwanda watashare ujuzi, changamoto, mafanikio waliyopata wakati wanasuka mfumo wao. Kufanya hivi inalenga kusaidia wataalam wetu wasuke mfumo wetu kirahisi wakitumia experience ya experts wa Rwanda kuepuka makosa.
Unatoa mawazo yako au una quote alichoongea raisi?
 
UKIONA MADAWATI ULIYOCHANGIA YAMECHAKAA BASI UJUWE NA WATAALAMU WA IT NA VIWANDA WATAPATIKANA TANZANIA
 
UKIONA MADAWATI ULIYOCHANGIA YAMECHAKAA BASI UJUWE NA WATAALAMU WA IT NA VIWANDA WATAPATIKANA TANZANIA
 
UKIONA MADAWATI ULIYOCHANGIA YAMECHAKAA BASI UJUWE NA WATAALAMU WA IT NA VIWANDA WATAPATIKANA TANZANIA
 
UKIONA MADAWATI ULIYOCHANGIA YAMECHAKAA BASI UJUWE NA WATAALAMU WA IT NA VIWANDA WATAPATIKANA TANZANIA
 
Tamaa yanmaendeleo inawasumbua, maendeleo hayaji kwa tamaa, yanakuja kwa sera zenye mashiko.

Mara nataka ivi kesho ivi kesho kutwa jingine, awamu ya mikuripuko.
 
1467865345451.jpg
 
Back
Top Bottom