VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Serikali ya Tanzania ya awamu ya tano,chini Rais Magufuli,inajipambanua kama Serikali ya viwanda. Ingawa bado hakujajengwa wala kuwa na matayarisho ya kiwanda chochote,'mahubiri' ya Serikali ni nchi ya viwanda.
Hivi juzi,Rais Magufuli amemuomba Rais Paul Kagame wa Rwanda wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano ili kusuka mifumo ya ukusanyaji kodi wa TRA. Maombi hayo ya Rais yamejadiliwa,yamelalamikiwa na kusifiwa. Wataalamu wa Kinyarwanda watatua nchini muda wowote.
Kama wataalamu hao tu wanatoka Rwanda,wataalamu wa kujenga na kuendesha viwanda lukuki vitakavyojengwa nchini watatolewa wapi? Hivi,mfumo wa Rwanda wa IT aliutengeneza nani? Hivi,ni kweli Tanzania inazidiwa utaalamu na wataalamu wa IT na Rwanda?
Nchi ya viwanda,CCM mbele kwa mbele!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)