Swali la kichokozi: Wataalamu wa IT wanatolewa Rwanda,wataalamu wa viwandani watatolewa wapi?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Serikali ya Tanzania ya awamu ya tano,chini Rais Magufuli,inajipambanua kama Serikali ya viwanda. Ingawa bado hakujajengwa wala kuwa na matayarisho ya kiwanda chochote,'mahubiri' ya Serikali ni nchi ya viwanda.

Hivi juzi,Rais Magufuli amemuomba Rais Paul Kagame wa Rwanda wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano ili kusuka mifumo ya ukusanyaji kodi wa TRA. Maombi hayo ya Rais yamejadiliwa,yamelalamikiwa na kusifiwa. Wataalamu wa Kinyarwanda watatua nchini muda wowote.

Kama wataalamu hao tu wanatoka Rwanda,wataalamu wa kujenga na kuendesha viwanda lukuki vitakavyojengwa nchini watatolewa wapi? Hivi,mfumo wa Rwanda wa IT aliutengeneza nani? Hivi,ni kweli Tanzania inazidiwa utaalamu na wataalamu wa IT na Rwanda?

Nchi ya viwanda,CCM mbele kwa mbele!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Rwanda bila shaka! Wahitimu wenyewe wanahitimu pale College of Engineering UDSM ahahahahaaaaas.
 
Nadhani kunakitu kinapotoshwa. Siamini serikali inaweza achia taifa lingine isuke mifumo yake ya kitechnologia kama hili la mfumo wa ukusanywaji kodi. Hapa itakuwa wataalam toka Rwanda watashare ujuzi, changamoto, mafanikio waliyopata wakati wanasuka mfumo wao. Kufanya hivi inalenga kusaidia wataalam wetu wasuke mfumo wetu kirahisi wakitumia experience ya experts wa Rwanda kuepuka makosa.
 
Na yule mtaalamu wa mifumo ya computer jeshini alitorokeaga wapi? Asije akawa ni moja wapo!
Jamii Forum kuna watu mna kumbukumbu mpaka Raha,ukisikia kupatwa Raisi kama Mwezi,Magufuli ana mihemko na Pia huenda ile kauli yake kuwa Uraisi angejua asingegombea,zile Thread za Rwanda za mwaka jana nani kazisahau haraka namna hii,huenda kuna special inerest kwa ccm kuivuruga nchi hii kila kona,but hivi sisi mbona hata hatushituki,May be ile thread ya IQ Inatuhusu sote.
 
Serikali ya Tanzania ya awamu ya tano,chini Rais Magufuli,inajipambanua kama Serikali ya viwanda. Ingawa bado hakujajengwa wala kuwa na matayarisho ya kiwanda chochote,'mahubiri' ya Serikali ni nchi ya viwanda.

Hivi juzi,Rais Magufuli amemuomba Rais Paul Kagame wa Rwanda wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano ili kusuka mifumo ya ukusanyaji kodi wa TRA. Maombi hayo ya Rais yamejadiliwa,yamelalamikiwa na kusifiwa. Wataalamu wa Kinyarwanda watatua nchini muda wowote.

Kama wataalamu hao tu wanatoka Rwanda,wataalamu wa kujenga na kuendesha viwanda lukuki vitakavyojengwa nchini watatolewa wapi? Hivi,mfumo wa Rwanda wa IT aliutengeneza nani? Hivi,ni kweli Tanzania inazidiwa utaalamu na wataalamu wa IT na Rwanda?

Nchi ya viwanda,CCM mbele kwa mbele!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Rwanda ina kila kitu kuzidi hata Europe, USA
 
Nadhani kunakitu kinapotoshwa. Siamini serikali inaweza achia taifa lingine isuke mifumo yake ya kitechnologia kama hili la mfumo wa ukusanywaji kodi. Hapa itakuwa wataalam toka Rwanda watashare ujuzi, changamoto, mafanikio waliyopata wakati wanasuka mfumo wao. Kufanya hivi inalenga kusaidia wataalam wetu wasuke mfumo wetu kirahisi wakitumia experience ya experts wa Rwanda kuepuka makosa.
Kwanini wasipelekwe wakajifunze huko,mafunzo kazini,huwezi jifunza ujuzi kwa kukaribishwa chumba cha operation
 
Rwanda mfumo wao wa mapato ni asycuda ambao sisi tuliwacha na kwenda tancis kwa maelezo kuwa ni mpana na unakidhi sehemu zote kwa maana unaweza kuunganisha na sehemu tofauti zenye lengo moja. Sasa sijui hao wataalamu wataturudisha kwenye mfumo tuliouacha kwamba haukidhi.
 
Back
Top Bottom