Mhe. Waziri wa Elimu na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, naomba ufafanuzi natumai mnasoma swali hili, ni kwamba inapofika wakati wa Mitihani ya Form 6 na Form 4 Askari huwa ni walinzi pale Strong Room yalipo Mitihani, na huwa wanapewa posho kwa ajili ya ulinzi huo, sasa imeanza kuwa desturi au tamaduni za ma OCD na wakuu wa vituo kukubaliana na ma Afisa Elimu na Watendaji husika kuwa Fedha wanazolipwa ASkari kama posho kwenye ulinzi wa Mitihani ma OCD au wakuu wa vituo huwa wanaomba wamegewe sehem ya posho hizo nao walipwe wakati wao hawalali usiku kucha wakilinda mitihani hiyo (Askari hujikuta hapewi pesa iliyo kadiriwa kama posho kwenye ulinzi)isingekuwa utaratibu unaopangwa mhasibu asingekuwa na mamlaka ya kupunguza posho hizo.
Ni sheria ipi inayotumika kumega kwenye posho hizo za askari ili na wao ma OCD wapate, zoezi hili ni la muda mrefu hawajaanza leo ndio maana wamekuwa wakiendelea tu kufanya hivyo.
Askari wenye Nyota wao pia huenda hawaruhusiwi kwenda kulinda mitihani HUKO MA SHULENI, ila kwa sasa wana wanyanyasa ma coplo na constable kuwazuia wasiende wao ndio waende huku wakijua wao hawawezi kubeba silaha kwenye lindo hilo. Kupata uhakika zaidi kagueni shule zote mtawakuta askari wenye Nyota wapo wa kutosha karibia kila baada ya shule 3 lazima utamkuta askari mwenye nyota mmoja yupo kwenye kituo wanafunzi wanapofanyia mtihani, Msaada wa ufafanuzi kama kuna sheria inayo walinda au la. Kwako Mhe. Waziri wa Elimu na IGP.