Swali kwa Waziri Mkuu kuhusu kuhamia Dodoma

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,453
Kwa heshima na Taadhima, naomba kukuuliza Mkuu wangu. Suala la kuhamia Dodoma mliliamua baada ya kufanya utafiti wa kitaalamu au mliamua tu kisiasa? Kwa sababu kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kwamba limekwama.

Pia nakuomba mkuu wangu, uwaweke wananchi unaowaongoza wazi ili wajue. Kama je, mmeahirisha au mmegairi kabisa? Mkuu hakuna kitu kizuri Kama sisi wananchi wako tunapoamka tujue tunaelekea wapi. Sasa ukikaa kimya namna hii, wananchi hawatajua waelekee wapi. Kumbuka ili Serikali istawi inategemea wananchi walipe kodi.

Kuna watu mpaka sasa hivi wameshaamua kuwekeza Dodoma lakini kila Siku wasi wasi wao unaongezeka na hii inatokana na jinsi hili zoezi la kuhamia linavyosua sua. Sasa Mkuu ebu Nikuombe. Kwanini usiitishe vyombo vya habari na ukawaambia wananchi wako wakajua Ukweli ili na wao wajipange vinginevyo?
 
Kama umeona unasuasua kwa vyovyote wananchi wotr wanaona hivyo hivyo sasa kwanini mpk utangaziwe? Umeshajua serikali imeshindwa endelea na mambo yako.
 
Bajeti ya kuhamia Dodoma ni zaidi ya Trilioni 4 sasa zinatoka wapi? Vuta subira mkuu wangu tunakuja.
 
Wanamalizia calculation za mshahara kwa watumishi wanaohamia dom from dsm ili wajue garama halisi za uhamisho.
 
Jamaa walituona wajinga tena waziri mkuu akatupungia na mkono kwakhelini mimi narudi dom na huko dom wakampokea kwa mbwembwe pale airport karibu mkuu. Sasa mbona umerudi dar tena maisha ya maigizo yamekushinda? Sisi bado tunakumbuka ratiba yote yakuhamia dom mda ukifika vzr tunaomba majibu .
 
itakuwa kitu cha ajabu sana kama ile ofisi ya waziri mkuu iliyoko Dar kama bado inatumika,kwa mbwembwe alizoondoka nazo waziri mkuu ilitakiwa hiyo ofisi iwe imetiwa kufuli au iwe wamepewa UDA
 
Mleta uzi umenikumnbusha kitu Fulani ambacho nilikuwa nakifiria jana.Kuna mwaka siukumbuki lakini Serikali ilisema itatoa UAMUZI MGUMU (Sijui ni JK na Shein?),tukakaa roho juu.Siku ikafika tukawasikiliza..Wakatoa maamuzi magumu.Moja ya maamuzi magumu ilikuwa ni kupiga marufuku mifuko ya Plastic.Jana nilikuwa natembea sehemu Fulani Tanzania nikakutana na uchafu wa mifuko ya Plastic hatari.Kuna hivi vimifuko vya plastic vyepesi sana vyeusi vimeshika Chart.Hivi ni vyepesi na vinapeperushwa na upepo vimekuwa kero kweli kweli
 
Wananchi wako njia panda. Hawajui haswa kipaumbele ni nini.tunaishi Kama mbuzi wasio na mchungaji
 
Mleta uzi umenikumnbusha kitu Fulani ambacho nilikuwa nakifiria jana.Kuna mwaka siukumbuki lakini Serikali ilisema itatoa UAMUZI MGUMU (Sijui ni JK na Shein?),tukakaa roho juu.Siku ikafika tukawasikiliza..Wakatoa maamuzi magumu.Moja ya maamuzi magumu ilikuwa ni kupiga marufuku mifuko ya Plastic.Jana nilikuwa natembea sehemu Fulani Tanzania nikakutana na uchafu wa mifuko ya Plastic hatari.Kuna hivi vimifuko vya plastic vyepesi sana vyeusi vimeshika Chart.Hivi ni vyepesi na vinapeperushwa na upepo vimekuwa kero kweli kweli
Hahahaha. Nimecheka mpaka basi! Nakumbuka ssna. Jamaa walitup shauku kubwa ya kusubiria maamuzi magumu, kumbe ni kupiga marufuku mifuko ya plastic? Au kuna kitu walitaka kufanya wakabadili mawazo?
 
Back
Top Bottom