Waziri Mkuu aagiza kufikishwa mahakamani kwa maafisa wanne wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa tuhuma za ubadhirifu

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
591
1,374
Haya sasa Waziri Mkuu ameanza kazi yake leo ameshalamba vichwa vinane vya watumishi huko Kigamboni akitaka wafikishwe mahakamani mara moja.
============================

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameelekeza kufikishwa mahakamani mara moja kwa maafisa wanne wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na watumishi wanne wa kitengo cha Akaunti Jumuifu ya Amana (TSA) kilichopo TAMISEMI kwa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi milioni 165.6.

Aidha ameagiza Bi. Annie Nyabugumba Maugo wa Kitengo cha Akaunti Jumuifu ya Amana asimamishwe kazi kutokana na ushiriki wake kwenye muamala uliohamisha fedha kutoka TAMISEMI kwenda katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Oktoba 06, 2024) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi. Waziri Mkuu yupo mkoani Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Soma Pia: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza kusimamishwa kazi kwa maafisa wa Halmashauri ya Kilolo kwa Tuhuma za Matumizi Mabaya ya Fedha za Umma

Mheshimiwa Majaliwa amefikia maamuzi hayo kutokana na uchunguzi uliofanywa na timu aliyoiunda kufuatilia tuhuma za ubadhirifu huo pamoja na ukaguzi maalum uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ili kujiridhisha na ukweli wa tuhuma hizo.

Waziri Mkuu amesema kuwa matokeo ya timu ya uchunguzi aliyoiunda yalionesha kuwa watumishi hao walikuwa wanatumia akaunti ya Amana kuficha fedha hizo tofauti na malengo ya matumizi ya akaunti hiyo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Septemba 05, 2022 watumishi watatu wasio waaminifu kutoka TAMISEMI walishirikiana na watumishi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kuleta shilingi milioni 165.6 na kuzihifadhi kwenye akaunti ya Amana na zikakaa mwaka mzima bila Mkurugenzi, Baraza la Madiwani na Wakuu wa Idara wengine kujua.

“Watu hawa wachache walikutana Dodoma, wakati wa mapitio ya mahitaji ya fedha kwa ajili ya Halmashauri na wakakubaliana na maafisa wa kitengo cha fedha za Halmashauri wa TAMISEMI, Bw. Aidan Mponzi, Adora Mwombeki Mbalilaki na kukubaliana wataingiza fedha lakini baada ya muda fedha hizo wazirudishe na fedha zikaingia na baada ya muda wakaanza kufanya matumizi.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa walianza kutumia fedha hizo bila kulijulisha Baraza la Madiwani na bila kuingizwa kwenye bajeti ya Halmashauri ili wakuu wengine wa idara wajue kwamba kuna fedha.
 
Niruhusu nitoke nje ya mada yako lakini, ndio nini hii kufanya vikao vya kazi siku isiyo ya kazi (jumapili) kwa jambo ambalo sio emergency?

Nachelea kusema sababu ya dini, sitaki kuleta udini
 
Hii statement ya kusimamishwa kazi imezoeleka sana na ina chain ndefu, ilitakiwa tufike mahali wapigwe risasi hadharani kila mtu angeheshimu mali ya umma
 
Wafilisiwe kwanza,ndipo wapelekwe mahakamani.
Wakienda kuachiwa huru tuwr tumesha chukua vyetu
 
Ila kufanya kazi halmashauri ni aidha ufe maskini au ubetie Jela au kuwin.
Halmashauri kuna njaa sana na sehemu yenye njaa kuna majungu.
Hapo zimetajwa pesa nyingi lakini kiuhalisia jamaa labda wamekula milioni 5 tu kwa kila mmoja au pungufu

Kuna njaa imepitiliza. Na kibaya watu wengi wamekaa kuvizia upigaji. Hakuna maarifa wala kutumia akili. Ni kuangalia sehemu gani kuna mnyonyo, tena kwa gharama yoyote ile.
Kweli kuna usomi hauna manufaa
 
Back
Top Bottom