Swali kwa wanawake: Kwanini mwanaume alipe Mahari?

Swali kwa wanawake: Kwanini mwanaume alipe Mahari?

Vijana wa siku hizi banaa, yaan mnapenda vya Bure Bure, mpate Wanawake wa Bure, muwale Bure, wakiomba Hela za matunzo mnasingizia "Demu malayaaa, nmemtema Kwa Kupenda Hela"

Mamaeee.

Na Kupenda Bure mpaka kwenye starehee, na pombe za Bure, mmejikuta mnawatunuku wanaume wenzenu.



Mahari sio suala la Mwanamke, Mahari ni suala la Lazima , Shukran , Heshima Kwa wazazi/walezi wa mwanamke uliyomuona anafaa kua Mke wako!!.
Mkuu suala ni sababu za kutoa mahari ingetosha tu kusema sababu zako bila fujo kuna watu wana pesa nyingi tu na hawaoni umuhimu wa kutoa mahari
 
Katika dini ya Uislam, mahari ni wajibu ambao umewekwa na Allah katika Qur'an

وآ توا النساء صدقاتهن نحلة

“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)

يا أيها النبي إنا أحللنا لك أزواجك اللاتي آتيت أجورهن

“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-Ahzaab: 50)

فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة

“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)

Hivyo katika Uislam mahari ni wajibu iliyowekwa Kishari'ah.

Na mahari ni makubaliano ya pande mbili na hakuna ndoa ila kwa mahari. Ila kinachopendeza katika mahari ni ile hafifu ambayo haimkalifishi muoaji.

Na Allah anajua zaidi.
 
Ningependa kupata mtazamo wa wanawake waliopo hapaa Jukwaani kuhusu suala la mwanaume kulipa mahari anapotokea amempenda mwanamke fulani na anahitaji kuishi naye.

Naomba kufahamu ni kwanini unadhani ni halali/lazima "Mahari" itolewa kuelekea upande wa Mwanamke?

Soma hii thread humu jukwaani:​


 
Kwenye jamii nyingi za Africa, South America, some tribes za N. America na sehemu za nchi nyingi za Asia; utoaji wa mahari kwenye familia ya mwanamke ni ishara ya heshima na kuthamini familia ya mwanamke kwa kukutunzia mke (zamani lazima awe locked kwa down).
Ila hakuna uhusiano wa Moja kwa Moja kutoa mahari na unyanyasaji (zipo mila kandamizi kwa mwanamke ila sababu si kwa ajili ametoa mahari). Case study nzuri ilikuwa India mpaka walipoamua kuingilia kati utaratibu wa mahari, surprisingly iliwakandamiza wanawake.
 
Jibu

Jibuni mkiwa hamjavuta basi.
Shukrani kwa wazazi, kwani mwanamke Hana wazazi? Hajatunzwa au kulelewa na wazazi?

Binafsi sioni umuhimu, Ni ukandamizaji tu na kutengeneza mazingira ya utumwa kwa mwanamke.
Kiongozi, masuala ya ndoa kati ya familia Moja na nyingine ni kama siasa tu...jamii nyingi inamuweka mwanamke kwenye daraja la juu na lenye thamani...ila sasa wakishaona inakuwa ni another family ambayo Ina values na norms za kwao...(bahati mbaya mfumo wetu duniani,mwanaume ndio general wa hiyo familia,it can be a dictatorship gov, democratic gov or egalitarian gov).
 
Back
Top Bottom