Swali kwa Wanawake: Kwa nini mwatumia vipodozi?

Swali kwa Wanawake: Kwa nini mwatumia vipodozi?

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
77,141
Reaction score
111,023
Katika pitapita zangu mitandaoni nimekutana na picha ya huyu binti ambaye kaoneshwa kabla na baada ya kujikwatua...

Binafsi nimepatwa na hamaki mkono kinywani maana kama si kutizama maneno "Before & After" ningelidhani nawatazama viumbe wa kike wawili tofauti, lakini ni sura ya mtu mmoja aliyekwatulia kutengeneza sura nyingine tofauti...

Sasa nawauliza ninyi walimbwende mliopo humu jukwaani, hivi huwa hamna kipimo cha kujipara hizo nyuso zenu?

Ndio maana huwa kuna watoto wanaogopa kubebwa nanyi huku wakilia, wengine huwa mwadhani watoto hawajazoea wageni kumbe ni hizo nyuso zenu huwatisha...


DSC_0813-horz.jpg
 
Huyo dada inaonekana alivaa make up kwa ajili ya shughuli (send off, chicken party and the like), sidhani kama in normal days anaweza akajipodoa hivyo.

Halafu, ndio maana tukawa wanawake, ni kawaida mdada na kujipodoa. Ukiwa too plain haipendezi sana ingawa na kuzidisha pia sio.
 
tuna create market ya vipodozi, imagine wote tusitumie si watafunga kiwanda?

Nikimuangalia huyo binti hapo kwa picha naona ni mrembo akiwa hajavaa make-ups zozote lakini baada tu ya kukwatulia ni kama anakera vile...

Sasa kwa mantiki hiyo je unaona kama anatangaza biashara au ndio anaididimiza?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom