Swali kwa waliowahi kuanguka

Swali kwa waliowahi kuanguka

Kama ni mhamiaji halali, kwa miaka 20 ya upinzani kwanini mtu hakuona juhudi za wapinzani? Kwanini atumie mapesa kutaka kupeperusha bendera ya CCM? Je wakiambiwa waanze nyuma kama wageni wengine watakubali?

Hapa kuna hoja ya msingi hasa katika upinzani wa Tanzania ambapo unafanya kazi kwa huruma ya watawala. Hivi hawa wote ambao wanatoka CCM dakika hizi wakati CDM wanapigwa mabomu, wanauawa na kunyanyaswa waliiwahi hata dakika moja kutoa kauli ya kuwatetea? au hata kuonesha sympathy?
 
Wapinzani Tanzania wamebinywa kila upande,kushinda uchaguzi mpaka kipindi ifike watanzania wote wameichoka ccm na wapinzani wapate ushindi wa asilimia kuanzia 80 kwenda juu ambao haufichiki hata kwa goli la mkono,kiasi kwamba wakiiba bado haitoshi,wakitumia dola bado wanaonekana wameshindwa,ila kwa kutegemea upinzani upate asiliamia kama 53 halafu ccm 47 lazima goli la mkono igeuke kama bascketball kitu ambacho ni kawaida,naumia sana ila imahitaji Tanzania ufikie asiliamia 90 ya kura.....2011 kidogo ccm ianguke kwa maandamano ya chadema mzee wa loliondo katokea watu wakaacha kuandamana ili waende kwenye foleni ya kunywa majani ya miti pori yaliyochemshwa
 
uhalisia nimejifunza vitu vingi sana kwa sasa!!! na naanza kuamini kuwa Tanzania ya ya sasa haita pata ukombozi kutoka kwa chama chochote cha siasa!

Nimegundua vyama vyote vya siasa nchini hasa upinzani vipo kwa maslahi binafsi!!! rejea sasa umoja wa UKAWA unavyo hangaika na lowasa lengo sasa imekua kushika dola kwa kigezo kinaitwa ondoa mfumo wa ccm!!! wakati huo mfumo unao uondoa umejengwa na watu na watu wenyewe mmoja wao ni lowasa why sasa!!!!????

lakini pia Uwezo mdogo wa watanzania kupambanua mambo na kusababisha kulaghaiwa na wana siasa kuna nipa picha kuwa hakutakua nauongozi thabiti mika 100 tena ijayo! rejea mikutano ya CCM kwa wananchi hasa ya katibu wao mkuu utaona kabisa kuwa ni porojo kutafuta public sympath! kwa kujifanya kukemea ama kuibua matatizo ya wananchi nakujitia ukakamavu wa kuhaidi kuyatatua kitu ambacho wamefeli kwa 20 years sasa!!!! lakini juzi pia nimesikitishwa na CDM kuna kauli ilitoka pale mwanza kwamba MMEWASAMEHE??????? wengi wakajibu NDIOOOOO! kumbe ni mbinu ya maandalizi ya kumsamehe na Lowasa???? na wenzake walio jenga mfumo wa kifisadi huko ccm kwani cdm haijiamini kwa watuilio nao????

si vibaya kwa watu kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine, ila naangalia mtindo wa sasa, watu wa nahama kutoka ccm kwenda CDM mainly kwasababu maslahi yao binafsi yameshindwa kutimia huko ccm, wengine wanatoka CDM kwasabababu wameshindwa kupata nafasi ya kutetea maslahi yao binafsi kwangu ndo naiona sababu kuu!!! sasa tujiulize swali hawa wanao hamia humu walikuwa wapi siku zote????? yakina kua ya akina shibuda mtafanyaje???? kunania yadhati kweli ya kutukwamua hapa tulipo????

sad news nikwamba viongozi wetu nao wanalalamika kama sisi!!! tutafika???
 
Bado nahangaika endapo Lowassa atapitishwa kuipeperusha bendela ya Ukawa, mwisho wa siku yaani dakika za majeruhi anajiondoa kugombea kwa sababu zake binafsi itakuwaje?
Ni Angalizo tu!
 
Hili ni anguko la Chadema. Ukweli nami nimeshangazwa sana kwa hatua hii iliyochukuliwa na Chadema.
Kuna watu wamepoteza maisha, mali zao pamoja na viungo vyao waliipigania Chadema kwa kuamini kwamba Chadema ni adui wa ufisadi. Leo hii Chadema kinashindwa kufikiria vyema na kinachukua maamuzi kama haya?.

Wanachama wengi wa Chadema watarudisha kadi zao mara tu baada ya uchaguzi.
 
Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, hakuna yoyote anayekatwa CCM, na kuamua kuhamia Chadema eti kwa sababu haipendi CCM na sera zake, wahamiaji wote waliogombea CCM, waligombea CCM kwa sababu waliipenda, na kuhama kwao, CCM, sio kuhama kwa sababu sasa hawaipendi CCM, bali wanahama ili kuiadhibu CCM, na kujiunga kwao Chadema, sio kwa sababu sasa ndio wanaipenda Chadema, bali Chadema ndicho chama pekee kinachoweza kutumika kama bakora ya kuiadhibia CCM, and it is onlt wakiwa nje ya box, ndio wataingiwa na upendo wa kweli kwa Chadema, na hivi ndivyo walivyopatikana baadhi ya viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, Dr.W.Slaa, alikuwa CCM, akagombea kupitia CCM, akashinda kura za maoni za CCM, akakatwa na vikao vya juu vya CCM, akajiengua CCM (huku kadi yake ya CCM akiendelea kuihifadhi kama kumbukumbu hadi leo), ajajiunga Chadema (bila kukabidhi kadi ya CCM kama wafanyavyo wengine), Chadema kikampokea kwa mikono miwili, akagombea kupitia Chadema na akashinda kwa kishindo ubunge!. Hivyo hiki kinachoenelea sasa sio kitu kipya, kimekuwepo huko nyuma, kipo sasa, na kitaendelea kuwepo siku za usoni!.

Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?
Naunga mkono hoja yako ya Chadema kuwasimamisha walianguka Chadema, kwenye majimbo mengine yenye wagombea dhaifu wa CCM, ili siungi mkono hii kauli yako ya kibaguzi ya kuwaita wapokelewa wapya kuwa ni wanamageuzi uchwara!. Wengi ni mashahidi, kuna baadhi ya wana CCM walikuwa ni wana mageuzi shupavu zaidi hata walipokuwa ndani ya CCM kuliko hata baadhi ya wanamageuzi waliopo Chadema!. Tukianza kunyoosheana vidole vya kumuita kila aliyetoka CCM kujiunga Chadema ni mwana mageuzi uchwala, then tuache cherry picking na double standards, kwa kuwaweka wote waliotoka CCM kujiunga Chadema ni wanamageuzi uchara, akiwemo Dr. Wilbrod Slaa!. Is this fair kweli?!. To me, this is not fair hata kidogo!. Hebu pitia uzi huu,
[h=3]Mbunge wa CCM, Mhe. Esta Bulaya, Afanya Tukio la Kishujaa
[/h]uone nilisema nini kumhusu Ester Bulaya, halafu leo mtu aje amuite ni mwanamageizi uchwara!. This is not fair hata kidogo!.
Kuna watu kama Kangi Lugora, Deo Philikunjombe, Dr. Kingwangala, Kessy wako CCM ila ni wanamageuzi wa ukweli!, wakiamua ku cross kuja Chadema, hawa sio tuu ni mashujaa bali pia wanapaswa kupewa ukamanda right away!.

Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...
Kama unatatizo nao, unaonaje kama tukianzia kwa Dr?!, maana na yeye alikatwa ndipo akakimbilia Chadema, kumbe kwako wewe Mkuu Mzee Mwanakijiji, hata Dr.W.Slaa ni mtu mwenye tamaa ya madaraka?!.

Sio kila anayetoka CCM kujiunga Chadema ni Shibuda type!.

Natoa wito kwa wanachama na wapenzi wa Chadema, fungueni mioyo yenu, wapokeeni kwa mikoni miwili wale wote wanaokimbilia kwenu kwa lengo moja la kuisaidia Chadema kuingia ikulu ili kulikomboa taifa toka ukuloni wa miaka 30 ya mkoloni CCM!.

Pasco

[h=3][/h]
 
uhalisia nimejifunza vitu vingi sana kwa sasa!!! na naanza kuamini kuwa Tanzania ya ya sasa haita pata ukombozi kutoka kwa chama chochote cha siasa!

Nimegundua vyama vyote vya siasa nchini hasa upinzani vipo kwa maslahi binafsi!!! rejea sasa umoja wa UKAWA unavyo hangaika na lowasa lengo sasa imekua kushika dola kwa kigezo kinaitwa ondoa mfumo wa ccm!!! wakati huo mfumo unao uondoa umejengwa na watu na watu wenyewe mmoja wao ni lowasa why sasa!!!!????

lakini pia Uwezo mdogo wa watanzania kupambanua mambo na kusababisha kulaghaiwa na wana siasa kuna nipa picha kuwa hakutakua nauongozi thabiti mika 100 tena ijayo! rejea mikutano ya CCM kwa wananchi hasa ya katibu wao mkuu utaona kabisa kuwa ni porojo kutafuta public sympath! kwa kujifanya kukemea ama kuibua matatizo ya wananchi nakujitia ukakamavu wa kuhaidi kuyatatua kitu ambacho wamefeli kwa 20 years sasa!!!! lakini juzi pia nimesikitishwa na CDM kuna kauli ilitoka pale mwanza kwamba MMEWASAMEHE??????? wengi wakajibu NDIOOOOO! kumbe ni mbinu ya maandalizi ya kumsamehe na Lowasa???? na wenzake walio jenga mfumo wa kifisadi huko ccm kwani cdm haijiamini kwa watuilio nao????

si vibaya kwa watu kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine, ila naangalia mtindo wa sasa, watu wa nahama kutoka ccm kwenda CDM mainly kwasababu maslahi yao binafsi yameshindwa kutimia huko ccm, wengine wanatoka CDM kwasabababu wameshindwa kupata nafasi ya kutetea maslahi yao binafsi kwangu ndo naiona sababu kuu!!! sasa tujiulize swali hawa wanao hamia humu walikuwa wapi siku zote????? yakina kua ya akina shibuda mtafanyaje???? kunania yadhati kweli ya kutukwamua hapa tulipo????

sad news nikwamba viongozi wetu nao wanalalamika kama sisi!!! tutafika???
Mkuu , I see your point, ila siasa ni vita, ili kuingia ikulu, inabidi wapinzani watumie kila silaha, kamwe huwezi kumshinda adui yako kama hijui nguvu yake, ndio maana kwenye mbinu za medani kuna kitu kinaitwa infiltration, au hata kutumia chambo, au kukamata mateka!, hawa big fish kutoka CCM ni WMD zitakazo tumika kuiangamiza CCM na kuuingiza Chadema Ikulu!.
Pasco
 
Makapi yanajulikana tu, makaoi ni watu kama Mwigulu, kibajaji, Riziwani, Rage, Makamba, Membe n.k
 
Hii hoja na maswali yako yalishajibiwa na viongozi wakuu wa Chadema labda kama huamini kama kile wanachokisema ndiyo wanakiishi!

Pitia hapa,.soma uelewe hatutasubiri bali aina maana hatutapokea wanachama wapya wa chadema.kugombea .kumbuka unakuwa mwanachadema kwanza baada ya hapo ruksa kugombea .kwa kazi muhimu kuitoa ccm madarakani

Kwa kifupi sehemu ya habari ya Gazeti la Mwananchi ni hii,
soma uelewe hatutasubiri bali aina maana hatutapokea wanachama wapya wa chadema.kugombea .kumbuka unakuwa mwanachadema kwanza baada ya hapo ruksa kugombea .kwa kazi muhimu kuitoa ccm madarakani
 
Potelea mbali hata kama tunawapokea muhimu akiwa chadema Au upinzani aimbe wimbo wa chadema
 
Ni vizuri kidogo kukumbuka mazingira ya siasa ya wakati ule 1995 na mazingira ya wakati huu... CDM ya 1995 siyo ya sasa; mwaka ule watu tulikuwa tunazungumzia NCCR Mageuzi, UMD, CUF n.k...

Tuko pamoja mkuu.

CDM ya wakati huu si ile ya miaka takribani 20 iliyopita. Bado pia wanakabiliwa na changamoto ya elimu ya uraia kwa

wapiga kura hasa vijijini. Kwa mantiki hiyo, wanaposimamisha mgombea lazma waangalie kukubalika kwa mgombea husika

na uungwaji mkono kwake toka kwa wapiga kura.Haijalishi kama mgombea huyo ni "mhamiaji" au "mkazi" wa siku nyingi

katika chama chao...
 
Kama ni mhamiaji halali, kwa miaka 20 ya upinzani kwanini mtu hakuona juhudi za wapinzani? Kwanini atumie mapesa kutaka kupeperusha bendera ya CCM? Je wakiambiwa waanze nyuma kama wageni wengine watakubali?

Mkuu, ukitumia kigezo cha aina hiyo siasa itakuwa ngumu. Kumbuka, CCM imekuwepo tangu wakati wa chama kushika

hatamu. Kwa mantiki hiyo, karibu kila Mtanzania, kabla ya mfumo wa vyama vingi alihesabiwa ni mwana CCM. Kwa wakati

huu, watu wana uhuru wa kuamua kwa sababu wana-ma-chaguo, vyama ni vingi. Sitoshangaa aliye CCM kwa miaka yote

anapoamua kwenda chama cha upinzania iwapo amejiridhisha katika hilo. Asiulizwe: "ulikuwa wapi miaka yote 20 ya

mfumo wa vyama vingi, mbona hukujiunga nasi tangu wakati huo?"
 
Mwanakijiji

Two names come in my mind Mark Reckless and Douglas Carswell tena hawa walijua kabisa kuwa Tories wanaenda kushinda ila wakaondoka ili yaliyomo moyoni yaweze kupewa nafasi. Si uliona immigration ilivyokuwa ni siisue kwenye uchaguzi baada ya labour kuifanya none issue kwa takribani miaka 15 hivi . Kila mtu anaye defect lazima upime nia yake na malengo yake na faida atakazoleta kwa hiyo jumii.

Hivi leo Luicifa akiamua ku defect na kutubu kwa Mungu unajua nini kitatokea kwa dunia hii. Uovu utakosa kiongozi na kusamabaratika , je utapenda arudi kwenye kazi yake kuu ya zamani ya kumsifu na kumtukuza Mungu? bila shaka, Biblia haijasema malaika aliye chukua nafasi yake so hatuwezi ku compare.

Ni furaha iliyoje mwenye dhambi mmoja akitubu na ni zaidi akiamua kuhakikisha dhambi haziwatafuni wengine.
 
WaSira alihamia nccr frm ccm akarudi ccm leo n waziri miaka 8...na akaweka jina kwa kutangaza nia..siasa tamu jamani..embu nikabet ntarudi..
 
MM inaonyesha ni kiasi gani UONGOZI wa ndani ya CDM wameshindwa kuwaheshimu wanachama wake.Na pia imeshindwa kujua kuwa wanachama ndiyo wanaoijenga au kubomoa chama.

Sikutarajia kwamba hata Dr.Slaa,Tundu Lissu,Prof.Safari hivi hawa wote wameshindwa kuona kero hii?Hivi ni sababu Lowassa ana pesa au?

Nimeshindwa kuelewa aliyekuwa mchafu CCM leo amesafishwa na Omo au Sunlight?Hivi Uso wa Dr.Slaa atauweka wapi alipotaja list of shame na Lowassa akiwa kwenye nyumba?

In short my vote will be NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO to Lowassa kama watamteua kuwa mgombea Urais.

Kuna watu wenye vigezo na ni wasafi mmeamua kumleta huyu aliyeamua kuwaibia Watanzania miaka ya 80 haki zao za msingi.

Hapa ndipo nitakapomdharau Dr.Slaa kwa uhakika kabisa kama atakubaliana na hili la kumsimamisha Lowassa.Na ili nimuheshimu itabidi arudi pale alisemea kuhusu ufisadi wa Lowassa vinginevyo ajiuzulu nafasi yake ili aendelee kuheshimika.
 
Hapa kuna hoja ya msingi hasa katika upinzani wa Tanzania ambapo unafanya kazi kwa huruma ya watawala. Hivi hawa wote ambao wanatoka CCM dakika hizi wakati CDM wanapigwa mabomu, wanauawa na kunyanyaswa waliiwahi hata dakika moja kutoa kauli ya kuwatetea? au hata kuonesha sympathy?

Kinachoendelea sasa hakiingii akilini mwangu. Hivyo nakubali kuwa God works in mysterious ways.
 
Mkuu, ukitumia kigezo cha aina hiyo siasa itakuwa ngumu. Kumbuka, CCM imekuwepo tangu wakati wa chama kushika

hatamu. Kwa mantiki hiyo, karibu kila Mtanzania, kabla ya mfumo wa vyama vingi alihesabiwa ni mwana CCM. Kwa wakati

huu, watu wana uhuru wa kuamua kwa sababu wana-ma-chaguo, vyama ni vingi. Sitoshangaa aliye CCM kwa miaka yote

anapoamua kwenda chama cha upinzania iwapo amejiridhisha katika hilo. Asiulizwe: "ulikuwa wapi miaka yote 20 ya

mfumo wa vyama vingi, mbona hukujiunga nasi tangu wakati huo?"

Kwa hiyo unataka kusema kuwa misukosuko waliyopata wapinzani ilikuwa ni sehemu ya wepesi wa kisiasa? Au kuna wateule ni lazima wafanye siasa za kiyoyozi?
 
Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?

Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?

Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...
Tatizo nilionalo huko mbele ni kuwa wanaunda CCM ndani ya CHADEMA. Sina hakika watadhibitije hili na hasa watawafanyia nini wale wanachama wao waliokwishapita kwenye kura za maoni?
 
Back
Top Bottom