Swali kwa waliowahi kuanguka

Swali kwa waliowahi kuanguka

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,184
Reaction score
44,051
Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?

Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?

Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...
 
Hii hoja na maswali yako yalishajibiwa na viongozi wakuu wa Chadema labda kama huamini kama kile wanachokisema ndiyo wanakiishi!

Pitia hapa,

Kwa kifupi sehemu ya habari ya Gazeti la Mwananchi ni hii,
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitasubiri wanachama watakaoachwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uteuzi wa wagombea katika uchaguzi mkuu ujao.

Kutokana na tamaa ya kuingiza watu wengi kwenye Bunge, vyama vya upinzani vimekuwa na tabia ya kuwapokea wanachama wa CCM wanaoshindwa kwenye kura za maoni na baadaye kuwapa nafasi ya kugombea ubunge, lakini Dk Slaa anasema safari hii hawatakuwa tayari kufanya hivyo.

"Tulishasema kwamba kwa ngazi zozote hata ngazi za udiwani au ubunge hatusubiri mabaki, makapi yatakayotokea CCM ndiyo yaje kwetu," alisema Dk Slaa katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
 
Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?

Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?

Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...

Demokrasia ya kiAfrika inajengwa kwa kuhama vyama. Mfano Kenya, Nigeria, Malawi n.k
 
Hii hoja na maswali yako yalishajibiwa na viongozi wakuu wa Chadema labda kama huamini kama kile wanachokisema ndiyo wanakiishi!

Pitia hapa,

Kwa kifupi sehemu ya habari ya Gazeti la Mwananchi ni hii,

Actually sio kila wanaochwa na CCM ni makapi. Kwa sababu katiba haiuruhusu mgombea binafsi, watu wanatafuta vyama vya kuwadhamini hata kama hawavipendi.

Vilevile kutokana na umaarufu wa CDM kuongeza, wapo watakaotoka CDM kwenda vyama vingine kupata udhamini.
 
usijidanganye kuwa chadema ina malengo ya kweli ya kumkomboa mtanzania. chadema inachoangalia ni masilahi. huoni wanavyofurahia kupokea wale wanaokatwa/kuogopa kukatwa huko ccm? inasemekana mpaka sasa mbowe keshavuta bil 10 kutoka kwa lowasa, tatizo linakuja kwa slaa aliyemtangaza pale mwembeyanga kuwa lowasa ni miongoni mwa wale mafisadi wakuu 11 katika nchi hii. je slaa atakula matapishi yake? hicho ndo kikwazo. vinginevyo dili limekamilia.

Swali la Jumapili: Hivi kweli kabisa CHADEMA baada ya miaka mitano ya kujijenga, kuhamasisha wananchi na wanachama wake na kutikisa malango ya CCM inahitaji wana CCM kugombea nafasi zake mbalimbali ili kishinde katika Uchaguzi? Kwanini isisimame na watu wake waliokuwa nayo wakati wanapigwa mabomu, wanauawa, wanajeruhiwa, wananyanyaswa? Leo wanaibuka mashujaa wa dakika za mwisho kutoka CCM wanakumbatiwa kama wana mageuzi kweli? Kwanini wasingetoka wakati nafasi ilipokuwepo kuonesha kweli walikuwa hawaipendi CCM na sera zake?

Tusije kuona dakika hizi za majeruhi hata watakaokatwa CCM nao watakimbilia CDM na kuimba sifa za upinzani. Si bora hata Kamati Kuu ikawasimamisha vijana wake au wanachama wake walioanguka sehemu nyingine kwenye majimbo ambayo CCM ina wagombea dhaifu na ambapo CDM haikupata mtu wa kujitokeza? Kuliko kuwasimamisha wanamageuzi Uchwara? Si ni bora kuanguka na waliosimama nawe kuliko kusimama na waliokuangusha?

Sina tatizo na wana CCM ambao waliamua kundoka kabla ya mchakato wao kuwakata; nina tatizo na wale ambao wanakatwa CCM halafu wanakimbilia CDM! Kama ni tamaa ya madaraka tuwaache iwatokee kichwani? Hadi hivi sasa sijasikia mwana CDM aliyeanguka CDM akaamua kukimbilia CCM halafu akapewa nafasi kule katika mwaka huu wa Uchaguzi... hasa kama alikuwa ni mwiba kwa CCM...
 
mkuu huyo kibabu ni msahaulifu sana. umesahau alishawahi kukana uwepo wa kipengele cha ukomo wa madaraka kwenye katiba ya chama ambacho yeye ndo mtendaji mkuu.
hayo uliyoyanukuu alishayasahu kitambo. yaani dakika mbili tangia ayatoe kinywani mwake.

Hii hoja na maswali yako yalishajibiwa na viongozi wakuu wa Chadema labda kama huamini kama kile wanachokisema ndiyo wanakiishi!

Pitia hapa,

Kwa kifupi sehemu ya habari ya Gazeti la Mwananchi ni hii,
 
Demokrasia ya kiAfrika inajengwa kwa kuhama vyama. Mfano Kenya, Nigeria, Malawi n.k
Mkuu,
Sio demokrasia za Africa pekee hata Ulaya.

Tumeona chaguzi nyingi za Uingereza ambapo mbunge wa chama anahama na kwenda kugombea chama kingine na kushinda.

Hii mara nyingi inatokea ambapo anayehama anatoka kwenye chama kikubwa na kwenda chama kidogo.

Viongozi wa CHADEMA walitoa kauli ya 'makapi' kwa sababu nadhani waliamini CHADEMA kwa sasa ina uwezo wa kupata wagombea wazuri bila kutegemea mgombea kutoka nje.
 
usijidanganye kuwa chadema ina malengo ya kweli ya kumkomboa mtanzania. chadema inachoangalia ni masilahi. huoni wanavyofurahia kupokea wale wanaokatwa/kuogopa kukatwa huko ccm? inasemekana mpaka sasa mbowe keshavuta bil 10 kutoka kwa lowasa, tatizo linakuja kwa slaa aliyemtangaza pale mwembeyanga kuwa lowasa ni miongoni mwa wale mafisadi wakuu 11 katika nchi hii. je slaa atakula matapishi yake? hicho ndo kikwazo. vinginevyo dili limekamilia.

Kwa zaidi ya miaka 7 sasa viongozi wa CHADEMA wametuaminisha kuwa wanapigana na ufisadi na wakaenda mbele zaidi kwa kutaja majina ya watu wanaowaita ni mafisadi, Lowassa mmojawapo. Leo hii tunaposikia kuwa Lowassa yuko mbioni kwenda CHADEMA na Chama kinakaa kimya bila kukubali au kukanusha hizo taarifa ni dalili ya giza!

Na haingii akilini kuwa miaka yote hiyo CHADEMA hawakuwa wamejiandaa kuhusu mgombea urais!
 
Mwanakijiji
Alikuwa anapiga madongo kweli Lowasa alipokuwa anagombea CCM. Sasa the ball is in your court. Sijui utatoka na calculus ya aina gani.
 
Hoja yako ni ya msingi.

Hata hivyo, katika siasa sio lazima iwe hivyo wakati wote.

Kwa kutaja wachache tu;Dr. Slaa alikatwa CCM enzi hizo na akatimkia CHADEMA. Hivi sasa huko ameshakuwa lulu.

Inawezekana pia hata kwa wengine ikawa hivyo hivyo, jambo la msingi ni kuangalia nia ya dhati awe "mhamiaji halali" si

"mhamiaji haramu..."
 
Umeandika vizuri kama chadema ni GT watanote kitu hapa
 
Mwanakijiji
Alikuwa anapiga madongo kweli Lowasa alipokuwa anagombea CCM. Sasa the ball is in your court. Sijui utatoka na calculus ya aina gani.

Aah.. mimi tena; mbona nilishasema kwenye ile makala nyingine. Ila kuna upande mwingine unahitaji kutafakari. Je, akitaka kujiunga kama mwanachama wa kawaida naonaje? Na akiwa mwanachama wa kawaida akachangia mno katika kuiondoa CCM madarakani niseme nini?
 
Hoja yako ni ya msingi.

Hata hivyo, katika siasa sio lazima iwe hivyo wakati wote.

Kwa kutaja wachache tu;Dr. Slaa alikatwa CCM enzi hizo na akatimkia CHADEMA. Hivi sasa huko ameshakuwa lulu.

Inawezekana pia hata kwa wengine ikawa hivyo hivyo, jambo la msingi ni kuangalia nia ya dhati awe "mhamiaji halali" si

"mhamiaji haramu..."

Ni vizuri kidogo kukumbuka mazingira ya siasa ya wakati ule 1995 na mazingira ya wakati huu... CDM ya 1995 siyo ya sasa; mwaka ule watu tulikuwa tunazungumzia NCCR Mageuzi, UMD, CUF n.k...
 
Aah.. mimi tena; mbona nilishasema kwenye ile makala nyingine. Ila kuna upande mwingine unahitaji kutafakari. Je, akitaka kujiunga kama mwanachama wa kawaida naonaje? Na akiwa mwanachama wa kawaida akachangia mno katika kuiondoa CCM madarakani niseme nini?

Mkuu ningependa kujua mtazamo wako juu ya hili la Lowassa kuhamia CDM kama mwanachama wa kawaida ila mwenye influence na kuchangia kuongezeka kwa kura nn mtazamo wako, apokelewe bila kujali makandokando yake????
 
mkuu sio kwamba wamekaa kimya bali wamemkaribisha. mbowe ametamka hadhari kumkaribisha, lema vile vile na wanachama wengine wengi. na wale wachache wanaopinga wameambiwa wafungashe virago kama hawamtaki lowasa. huoni wanavyoshangilia humu mitandaoni.
hapa kwa wajanaja wanajua fika kuwa hawa ni wasaka tonge tu kama walivyo wasakatonge wengine.

Kwa zaidi ya miaka 7 sasa viongozi wa CHADEMA wametuaminisha kuwa wanapigana na ufisadi na wakaenda mbele zaidi kwa kutaja majina ya watu wanaowaita ni mafisadi, Lowassa mmojawapo. Leo hii tunaposikia kuwa Lowassa yuko mbioni kwenda CHADEMA na Chama kinakaa kimya bila kukubali au kukanusha hizo taarifa ni dalili ya giza!

Na haingii akilini kuwa miaka yote hiyo CHADEMA hawakuwa wamejiandaa kuhusu mgombea urais!
 
Mkuu,
Sio demokrasia za Africa pekee hata Ulaya.

Tumeona chaguzi nyingi za Uingereza ambapo mbunge wa chama anahama na kwenda kugombea chama kingine na kushinda.

Hii mara nyingi inatokea ambapo anayehama anatoka kwenye chama kikubwa na kwenda chama kidogo.

Viongozi wa CHADEMA walitoa kauli ya 'makapi' kwa sababu nadhani waliamini CHADEMA kwa sasa ina uwezo wa kupata wagombea wazuri bila kutegemea mgombea kutoka nje.

Ni kweli kabisa ata Ulaya watu wanahama. Lakini tukumbuke kuwa vyama vya Ulaya vina itikadi. Hivyo mara nyingi watu wanahama kwa itikadi au kusimamia kitu fulani.

Tukirudi kwenye uchokozi wa mwanakijiji, huku kwetu watu wanahama kwa sababu ni lazima yeye agombee ubunge, udiwani au urais. Na akinyimwa nafasi basi yupo tayari kuhamia chama kingine.

Vilevile ukumbuke kuwa CDM walisema hawapokei makapi ya CCM. Inaoneka sio vyote vilivyoachwa na CCM ni makapi. Si unaona jinsi ya neno fisadi lilivyopungua nguvu katika kipindi cha wiki mbili.

Kwa malengo ya kuiondoa CCM madarakani, upinzania unaweza kumpa nafasi mtu yoyote wamtakaye. Lakini kama malengo hayo hayatafanikiwa, kuna hatari ya kutokea yale yalioikumba NCCR mageuzi baada ya uchaguzi wa 1995. Waliokaribishwa wanaweza kuleta mambo ambayo hayako compatible na wenyeji.

Nasubiri kwa hamu majina ya wagombea wa CDM na UKAWA
 
Hoja yako ni ya msingi.

Hata hivyo, katika siasa sio lazima iwe hivyo wakati wote.

Kwa kutaja wachache tu;Dr. Slaa alikatwa CCM enzi hizo na akatimkia CHADEMA. Hivi sasa huko ameshakuwa lulu.

Inawezekana pia hata kwa wengine ikawa hivyo hivyo, jambo la msingi ni kuangalia nia ya dhati awe "mhamiaji halali" si

"mhamiaji haramu..."

Kama ni mhamiaji halali, kwa miaka 20 ya upinzani kwanini mtu hakuona juhudi za wapinzani? Kwanini atumie mapesa kutaka kupeperusha bendera ya CCM? Je wakiambiwa waanze nyuma kama wageni wengine watakubali?
 
Rudi nyumbani ugombee udiwani, ujenge Taifa, nchi bado inakuhitaji
 
Back
Top Bottom