Swali kwa Makonda: Nauli bure kwa Walimu katika mradi wa mabasi ya mwendo kasi

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
Kuna changamoto imezuka sasa hivi katika mabasi yaendayo kasi hakutmiwi vitambulisho Bali kadi za malipo, namuomba mh Makonda ajitokeze kuelezea mpango wake utakavotekelezwa kupitia UDART. Mh Makonda ukowapi walimu sasa wanalipa 650, 800 toka sh 400 Hivi sasa ndio leadership inahitajika zaid kutatua suala la nauli.

cc Paul Makonda
cc UDA manager
cc
 
Walimu wa Dar sasa wakavitunze vitambulisho vyao, waingie mifukoni kutafuta kilichosalia ili kulipia nauli, DART haiwatambui na wala serikali haina mpango na walimu. Huo wa Makonda ulikuwa wa kuchukua kick kutoka kwa Rais Magufuli. Tayari ameshaukwaa.
 
Wakati mwingine tufikiri zaidi ya tunavyoweza kufikiri. Je, ilikuwa halali kwa walimu wa Dar kusafiri bure? Ni kwanini wao tu na si kada zote za idara mbalimbali zilizopo Dar na kwingineko nchini? Hapa nauona ubaguzi tena wa wazi mno. Inakuwaje kiongozi wa umma anawabagua wafanyakazi wa eneo analoliongoza na kuwaacha wengine tena wenye umuhimu mkubwa kama polisi, manesi na madaktari? Waliobaguliwa wanajisikiaje? Morali ya waliopendelewa imepanda au ilibaki kama awali na huenda kushuka zaidi?
Tija kwa waliopendelewa ipoje? Na walioachwa je? Tukiweza kujijibu maswali haya basi uje mpango wa wote na sio huu wa nusunusu.
Kimsingi sikuona mantiki katika hili na cha kufanya ni kuwalipa mishahara mizuri itakayowawezesha kujilipia nauli. Hebu fikiri, mwanafunzi analipa 200/=na mwalimu mwenye mshahara unapanda bure. Je, watu hawa wawili wanajisikiaje kwa mfano? Kama wewe ni mwalimu wa mwanafunzi huyu huko darasani anakuchukuliaje? Tuwaache walipe nauli ili wajifunze kudai maslahi bora yenye kuwatosheleza vinginevyo ni kudanganywa kwa pipi kwa ahadi kuwa chakula cha kushibisha kinaandaliwa.
 
Siasa za msimu zisizo na maono ya mbali....kukimbizana na wanaotupa makopo ya maji....kuzibua mitaro wakati kuna kampuni zenye mikataba ya usafi
 
Naona sasa hivi hana ajenda,inawezekana hata ukaguzi wa silaha ameshausahau,
 
Kuna ule mpango wa kufanya baa zote zikae mtaa mmoja,sijui umefikia wapi?walevi wote wakutane hapo,najaribu kuupima urefu wa mtaa na je utauweka umbali gani kutoka katikati ya jiji....
 
Pole sana ndugu mwalimu , hiyo ilikuwa gia ya kupandia ngazi , kutoka UDC kwenda Ukuu wa mkoa .
 
Walimu kupanda daladala Bure, baa zote kuwa sehemu moja, uhakiki wa silaha, Wananchi wote wa Dar kuhakikiwa majina yao, mitaa yao na shughuli wanazofanya, ..... Hebu ongezea mengine sijui yote yameishia wapi.. Makonda bwaaaaana
 
Walimu kupanda daladala Bure, baa zote kuwa sehemu moja, uhakiki wa silaha, Wananchi wote wa Dar kuhakikiwa majina yao, mitaa yao na shughuli wanazofanya, ..... Hebu ongezea mengine sijui yote yameishia wapi.. Makonda bwaaaaana
Gereji zote kuwa mtaa mmoja,maduka ya vifaa vya ujenzi mtaa mmoja
 
Back
Top Bottom