SUMATRA yatangaza nauli kwa mabasi yaendayo kasi

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Uongozi wa SUMATRA leo umetangaza Gharama za nauli kwa Mabasi yaendayo kwa kasi zitakazoanza kutumika tarehe 12 Mei mwaka huu.

Njia ya pembeni ni Shilingi 400 kwa mkubwa na mwanafunzi ni 200.

Njia kuu ni shilingi 650 kwa mkubwa na mwanafunzi 200

Njia ya pembeni + njia kuu ni shilingi 800 kwa mkubwa kwa mwanafunzi 200

Na hii sasa kuna wa kulalamika?

==========


Taarifa zaidi..

dart.jpg

Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA imetangaza rasmi viwango vya nauli ya mabasi yaendayo kasi Jijini Dar es salaam huku ikitoa leseni kwa kampuni itakayosimamia mabasi hayo.

Akitangaza nauli hizo mpya kwa umma, jijini Dar es Salaam leo Mei 9.2016, Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe amebainisha kuwa baada ya kupokea maombi na kisha kuyafanyia kazi wamekuja na kiwango hicho cha nauli kutokana na njia zilizopo kwenye barabara za mabasi hayo yaendayo haraka.

Ambapo katika njia hizo kutakuwa na aina Zaidi ya mbili ambazo zitakuwa na tofauti ya ulipaji wake ikiwemo ile ndefu ambayo ni (Trunk route) huku ile ndogo itakuwa ni (Feeder route ) ama (Trunk+Feeder route).

Kwa upande wa njia ya FEEDER kwa njia fupi ni kwa abiria wanaotoka Mbezi Mwisho kwenda Kimara ambapo nauli itakuwa ni Tsh. 400 kwa mtu mzima na Wanafunzi itakuwa ni Tsh. 200. Hii ni hivyo hivyo kutoka Kimara kwenda Mbezi mwisho.

Kwa upande wa njia TRUNK- nauli itakuwa ni Tsh. 650 ni ile inayozihusisha njia za:

Kimara-Kivukoni/Kivukoni Kimara

Kimara-Kariakoo/Kariakoo-Kimara

Kimara –Morocco/Moroco-Kimara

Moroko-Kivukoni/Kivukoni-Morocco

Morocco-Kariakoo/Kariakoo-Morocco

Kariakoo-Kivukoni/Kivukoni-Kariakoo

Kwa upande wa njia za FEEDER+ TRUNK- Nauli kwa njia hizi itakuwa ni TSH. 800 ni ile inayozihusisha njia za:

Mbezi Mwisho-Kimara-Kivukoni/Kivukoni-Kimara-MbeziMwisho

Mbezi Mwisho-Kimara-Kariakoo/Kariakoo-Kimara -Mbezi Mwisho

Mbezi Mwisho-Kimara-Morocco/Morocco-Kimara-Mbezi Mwisho

Aidha, katika tukio hilo, Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe alikabidhi leseni maalum kwa Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT, Bw. David Mgwassa ambapo alimtaka afanye kazi kwa mujibu wa sharia huku leseni hiyo ikiwa ni ya mwaka mmoja ambapo itaisha mpaka Mei 8 2017, Hata hivyo alieleza kuwa, UDA wanayo haki ya kuongeza mkataba kadri watakavyoona inafaa.

Aidha, Mabasi hayo siku ya kesho Mei 10 na 11, watatoa ofa ya bure kwa kwa wananchi wote kupanda bure ilikupata elimu elekezi na namna ya uendeshaji. Hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kuyapanda mabasi hayo kama taratibu zitakazowekwa.
DSC_3049.jpg

Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza nauli hizo za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wakala wa Mabasi haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare na kuliwa ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, Johansen Kahatano.
DSC_3087.jpg

Mkuu wa Wakala wa Mabasi haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare akitoa ufafanuzi wa namna walivyojipanga kudhibiti magari mengine ambayo hayaruhusiwi kutumia njia hiyo ya DART. wakati wa mkutano huo wa SUMATRA wa kutangza nauli kwa mabasi yaendayo haraka.
DSC_3119-1.jpg

Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe akionyesga leseni maalum kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kukabidhi leseni hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT, Bw. David Mgwassa (Katikati). Kushoto ni Mkuu wa Wakala wa Mabasi haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare. Tukio limefanyika leo Mei 9.2016 jijini Dar e Salaam.
 
sina uhakika nimeelewa au ninaona namba tu, unaposema njia za pembeni wanamaana ipi? na njia kuu 650 hadi 800 ni zipi? waje na root za mjin, kwamba kutoka kimara to mjin ni sh ngp na kutoka moroco to kko o kivukon ni sh ngp,

hizi swaga hiz wanahitaji elim haswaaaa
 
sina uhakika nimeelewa au ninaona namba tu, unaposema njia za pembeni wanamaana ipi? na njia kuu 650 hadi 800 ni zipi? waje na root za mjin, kwamba kutoka kimara to mjin ni sh ngp na kutoka moroco to kko o kivukon ni sh ngp,

hizi swaga hiz wanahitaji elim haswaaaa
ROOT=ROUTE
 
Back
Top Bottom