Swali kwa infidelity members. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa infidelity members.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by St. Paka Mweusi, Sep 24, 2010.

 1. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Rafiki yangu ameoa,na mungu amewajalia ndoa yenye furaha tele na watoto wawili juu.Bwana ni bosi mkubwa tu katika wizara moja,na mama naye ni katibu muhtasi katika moja ya idara nyeti serikalini inayoshughulika na masuala ya fedha.Hivyo katika maisha yao shida ya maisha wanaisikia kwa wengine tu.Sasa siku ya siku jamaa yangu akampigia simu mkewe kuwa atachelewa kurudi kwani kazi zimemzidi,mke naye bila hiyana akamwambia usiwe na wasiwasi mimi utanikuta nyumbani.kumbe jamaa ana lake moyoni,baada ya kumaliza kazi siku hiyo akamchukua sekretari wake ambaye ni binti mdogo na mbichi kabisa na kwenda naye guest house moja maeneo ya sinza ambayo inasifika kwa maficho yake .Kufika tu kabla hata hajaingia ndani akashangaa kukuta gari ya mke wake iko parking.Ile tu anatoka kutaka kujua kulikoni anamuona mke wake anatoka huku akijifunga vizuri bazee lake na pembeni yake ameandamana na kijana ambaye wamemuajiri shambani kwao ili awasaidie kutunza mifugo yao.Ingekuwa wewe ndio limekukuta balaa hilo ungefanyaje?
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Japo mimi si mwanachama wa infidelity lakini nimevutiwa kujibu: Kwa wakati huo nitakapomwona hayo maeneo ya Sinza nitajikausha kabisa, tena nitajificha ili asijue kama nipo mahali hapo. Halafu nitafuatilia kila hatua wanayokwenda ili kukusanya ushahidi. Niikifika home ninamweleza ukweli wa yale aliyoyafanya kwa vielelezo vya hatua ya kwanza hadi ya mwisho aliyokwenda wakati akitoka pale mahali. Mwisho wa ushahidi huo ni mtu kufunga kilicho chake na kuondoka.
   
 3. 2my

  2my JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nn ukazanie yeye kufungasha?kwani huyo jamaa atakuwa kasahau alikwenda kufanya nn hapo mahala????yeye mwenyewe c alienda kuharibu!!!so inabidi afanye km vile hajaona chochote!
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapa na utamaduni pia unatumika. Kwa utamaduni wetu, mwanamme tu ndiyo anaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja. Kwa hiyo mme akicheat, inaweza kuwa anafanya maandalizi ya kuwa na mke wa pili jambo ambalo siyo kosa. Lakini mwanamke hana ruhusa ya kuolewa na mabwana wawili kwa hiyo akidanganya, huyo anasumbuliwa na tamaa za mwili tu. Kulingana na utamaduni wa mtanzania, mwanaume akidanganya, kosa lake ni dogo au haliwi kosa kwa kuwa inawezekana anatafuta bibi mdogo, lakini mwanamke akidanganya huyo ni malaya kwa kuwa anafanya hivyo ilihali anajua hana nafasi ya kuolewa na mabwana wawili kwa wakati mmoja.
   
 5. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  halafu kinachouma zaidi ni kuwa aliye naye ni mtu ambaye unamtuma kazi na kumlipa mshahara
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapo hakuna ujanja. Ngoma ni droo. Aliyeuza chani kauza cheni bandia, na alieyetoa pesa naye katoa pesa bandia. Na kampiku mwenzake?

  Akubali tu yaishe. Ila wanaweza kukaa wakapingezana na kupanga jinsi ya kusihi wote wakiwa ni members we infii club. Inaruhusiwa kwa kuwa wote wamevunja sheria za Teamo. Huwezi kufanya infidelity kwenye uwanja wa karibu na home.
   
 7. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Swali hili ni kwa wanamama pia maana linawahusu wote mume na mke na hata kama wewe sio member waweza kutoa maoni yako kama mshauri kwani hili ni tukio la kweli.
   
 8. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,583
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  imekaa vizuri sana hiyo, chamsingi ni kuwekana chini muachane na hayo ambo ili ndoa idumu.ingekuwa mbaya kama angefanya mmoja wapo.kwa vile ni wote safi sana.
   
Loading...