Swali kutoka harun | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kutoka harun

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KABAVAKO, Jul 28, 2012.

 1. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Siku moja Harun alikuwa katika Qasri yake akiangalia mandhari iliyokuwa ikimzunguka na sauti ya mbubujiko wa maji ya mto Tegris. Na mara hapo akatokezea Bahlul, na Harun alimwambia Bahlul: "Ewe Bahlul! leo hii nakuuliza fumbo, iwapo utafumbua vyema basi nitakupa dinar elfu moja na iwapo utashindwa basi nitatoa amri ya kukutosa majini."


  Bahlul alimwambia Harun: "Mimi sihitaji dinar hizo, bali ninakubali kwa sharti moja."
  Na alipokubali Harun, Bahlul alisema: "Iwapo nitaweza kulijibu vyema basi itakubidi kuwaachia marafiki zangu mia moja - kutoka Gereza lako, na iwapo nitashindwa basi unao uhuru wa kunitupa majini."

  Alianza Harun kulielezea fumbo lake: "Iwapo mimi ninaye mbuzi mmoja, mbwamwitu, na fungu la majani. Je nitawezaje kuvivusha vyote hivyo, kwamba majani hayataliwa na mbuzi na wala mbuzi kuvamiwa na mbwamwitu?"

  Bahlul alianza kumjibu: "Kwanza utamvusha mbuzi kwenda ng'ambo ukimwacha mbwa mwitu na majani. Baadaye utachukuwa majani uyavushe huku ukirudi na mbuzi upande huu. Utamwacha mbuzi upande huu na utamchukua mbwamwitu ng'ambo. Mwishoni utampeleka mbuzi. Kwa hivi majani hayataliwa na mbuzi wala mbuzi kuvamiwa na mbwamwitu."
  Harun alifurahishwa mno kwa majibu ya Bahlul. Na hapo Bahlul alimpa orodha ya majini mia moja ya wafuasi na wapenzi wa Ali bin Abi Talib (a.s.). Lakini Harun alimgeuka Bahlul. Lakini Bahlul aliendelea kusisitiza, na hatimaye aliwaacha huru watu kumi tu na akimwamwuru Bahlul kuondoka.
   
 2. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  wew kabavako si mboysia?bwana kabavako mbona ulikuwa kimya sana kwenye jukwaa la elimu? alaf hadith yako tupe funzo lake inatufundisha nin sisi vijana?
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Majini mia? Sijaelewa....
   
Loading...