Swali kuhusu Mahakama zetu na mrundikano wa kesi

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
620
342
Taarifa iliyotolewa na Jaji Mkuu kwenye siku ya sheria inaonyesha kuna mrundikano wa kutisha wa kesi kwenye Mahakama zetu

Mahakama ya Rufani (Court of Appeal) ndiyo kwanza sasa inashughulikia kesi za mwaka 2016 na 2017. Hapo haijagusa kesi za mwaka 2018, 2019 na 2020.

Kwa speed hii inamkatisha tamaa mtanzania kutafuta au kutetea haki yake Mahakamani. Kimsingi haki katika mahakama zetu ni haki iliyocheleweshwa.

Wagombea watajieleza na kuulizwa swali kuhusu kila Sekta.

Katika sekta hii ya sheria wajieleze au waulizwe watatumia mbinu gani ya kumaliza mirundikano ya kesi.
 
Back
Top Bottom