Swali: Humphrey Pole pole unamtumikia nani?

Swali: Humphrey Pole pole unamtumikia nani?

Hapa waadilifu na wachapa kazi tu. Mafisadi kwetu mwiko. Tuko pamoja Kiongozi Humphrey
 
Tatizo wamekariri mambo bila hata kuweka chembe ya busara.
Angelisikiliza ushauri wa mzee Mengi aliposema 'kuna maisha baada ya uchaguzi' ingelimsaidia sana. Maana Mengi amefanya biashara na Mwalimu, Mzee Mwinyi, Mkapa, JK na sasa anausoma mchezo wa awamu ya tano bila kwakwaruzana na yeyote hadharani.
 
nilimwona anatoa povu anadhani tunamwelewa.Tulishampuuza kama karatasi ya chooni iliyotumika. Kama alikuwa anatetea katiba ya Warioba mbona leo haitetei? Njaa mbaya kuliko maelezo
 
Polepole analipwa ili awadanganye watanzania lakini watanzania wa leo wamezinduka. hawadanganyiki.
POLEPOLE UNAMTUMIKIA NANI?

Na Ally Rama.

Nimetoka kuangalia mdahalo kuhusu amani; umoja na haki kupitia star TV pale ubungo blue pearl hotel..

Kwa title ya mdahalo; niliamini watajadili kuhusu haki; umoja na amani lakini wakajielekeza kwenye uchaguzi mkuu bila kugusa vipengele husika..

Miongoni mwa hoja zilizotawala mjadala (si kwa Bahati mbaya) ni mjadala Wa urais kati ya wagombea wawili Magufuli na lowassa..

Polepole kwa nafasi yake; aliendelea kuonesha chuki zake kwa lowassa na alitumia mchakato Wa kupata katiba mpya kuelezea namna Lowassa alivyohujumu mchakato ule hivyo hafai kuwa rais na huo ndio ugomvi wake na lowassa ulipoanza..

Polepole kwa maelezo yake anasema; Lowassa ndie aliharibu mchakato na akaratibu harakati za kupinga kupatikana kwa katiba ya wananchi kwa kigezo cha kuwa mapendekezo Yale yanadhoofisha taasisi ya Urais..

Akaendelea kudai; walienda kumuomba akubali maoni yao lakini akakataa..

Nikaanza kuukumbuka mchakato ulivyokaenda na nikaja na maswali yafuatayo..

1: Lowassa ndani ya CCM hakuwa mwenyekiti wala katibu mkuu..
ndani ya serikali hakuwa hata Waziri..
Sasa nguvu ya kuhodhi mchakato ule bungeni aliitoa wapi?

2: hasimu wake kisiasa Mzee Sitta ndie Alikuwa mwenyekiti Wa bunge maalum la kufinyanga katiba ya wananchi..
Nae aliingizwa king na Lowassa??

3: mama Samia Suluhu Hassan ambaye leo ni mgombea mwenza Wa magufuli; nae aliingizwa king na lowassa afinyange katiba?

4: Mwigulu Nchemba; January na Vijana wengine Makini ndani ya CCM waliipinga rasim ya warioba; nao waliingizwa king na lowassa?

5: inajulikana hata adui mwingine Wa lowassa; paul Makonda alishadadia swala la kifinyanga maoni ya wananchi hasa kwenye kipengele cha muundo Wa muungano..
Akampiga Mzee warioba...
Akazawadiwa ukuu Wa Wilaya ya kinondoni..
Nae aliingizwa king na lowassa??

6: membe nae alipinga muundo Wa muungano..
Nae aliingizwa king na lowassa??

7: Mzee kikwete km rais Wa nchi aliishiwa nguvu ya kuhimili mihemko ya wabunge Wa CCM hadi akaelekea kibra..

Nae aliingizwa king na lowassa??
Aliwazawadia ukuu Wa wilaya Akina Makonda kwa kupinga katiba ya warioba..
Nae aliingizwa king na lowassa??

Eti kweli lowassa pekee ndie alikwamisha mchakato ule?

Kakangu Polepole; hebu kuwa mkweli hapa...

Hao unaowapigia kampeni ndio walokwamisha mchakato Wa katiba mpya..

Polepole Vaa uzalendo; Vaa utanzania..
Zungumza ukweli..

La sivyo tuambie unamtumikia nani??

Ni wazi kuwa Pole Pole hana Moral Authority ya kuwaambia Watanzania kuwa Lowassa aliingilia Mchakato wa Maoni ya Watanzania katika kuipata Katiba Mpya, Mchakato wa kuipata Katiba Mpya kama ni kukwamisha nadhani arudi kwa Mwenyekiti wa Ccm ambaye aliridhika na mambo ya kihuni yaliyopelekea kuvunja utu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Time ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.

Pole pole alikuwa mfuasi wa Katiba ya maoni inayoungwa Mkono na Wananchi ya Serikali tatu na aliipigania sana na ambayo inaungwa Mkono na UKAWA. Ni ajabu sana kuona anaegemeza matusi na hoja dhaifu kwa Mgombea Urais wa UKAWA ambaye anatetea Katiba aliyoipigania.
Tumpuuze kwa kuwa in dhahiri kuwa anatumika na Ccm.

Edited by,
pg.
 
Polepole sijui hata hajioni alivyopauka kama ana kwashiokor
 
Kumjadili Magufuli ruksa, ila Lowassa Nongwa.!

HIVI KWELI LOWASA NDO ALIYETOA SPEECH YA KULIFUNGUA BUNGE MAALUM LA KATIBA NA KUTOA MWONGOZO?...Hakuna kizuizi cha kumjadiri mtu ila mahaba yanapozidi Uongo na ukipofu huchukuwa nafasi....POLEPOLE ameongopa
 
Njaa mbaya sana inapotoka tumboni akaamia kichwani hata uwezo wa kufikili unakuwa mdogo au utajikuta unafikili kutumia ......buli
 
Kumjadili Magufuli ruksa, ila Lowassa Nongwa.!

Kwani hapa jamvini mbona kuna mada kibao zinazomwongelea jamaa yenu inakuwaje unasema mnazuiwa kumuongelea? ni nani anawazuia?
 
Huo ndio uwezo wake,mkuu umewwka hoja za msingi sana. Asituaminishe matatizo tuliyonayo lowassa ndio chanzo. Mungu amsamehe kwa huyo bwana amtumikiaye.

Lowasa ni jambazi linalotembea mtaani ndio maana wafungwa segerea wanalalamika kila siku kwa kuwa wanaona kuna majizi zaidi yao yapo huru na yanatalii tu mikoani yakijifanya mfano wa raisi.
 
Kuna mchangiaji alimwambia kuwa yeye anafanya kazi ya @Nape hii ni kweli kabisa. amekuwa katibu mwenezi wa ccm. nilichofurahi alimwambia huku wakiangaliana uso kwa uso na ujumbe wake ulimfikia moja kwa moja tofauti na sisi tunao andika huku kwane social networks.

Polepole wewe ni katibu mwenezi wa CCM. endelea kufanya kazi za ccm tuachia tufanye maamuzi yetu wenyewe
 
Polepole kasema ukweli wake na mimi sishangai kuyaona hayo. Kwani kama mtu alinunuwa watu wote ingeshindikana nini kupiga kampeni na wakamgomea hata huyo Mwwnyekiti unaemsema? Au hujui nguvu ya ushawishi inavyofanya kazi? Na kwa taarifa yako hata nyie humu mnasukumwa na nguvu ya ushawishi na mnajikuta wakati mwingine mnashabikia vitu msivyovifanyia utafiti na wala hamhangaiki kupata historia za hawa watu mmoja mmoja. Bora mkae kimya kuliko kuwa mnajiaibisha.

waliokufikisha hapo wakiwemo Kingunge,Sumaye,Guninita,Marsha, na Lowasa.

Ati wanashindw kugundua hata hilo tu jamani .
 
Lowasa ni jambazi linalotembea mtaani ndio maana wafungwa segerea wanalalamika kila siku kwa kuwa wanaona kuna majizi zaidi yao yapo huru na yanatalii tu mikoani yakijifanya mfano wa raisi.

Nadhani Jambazi ni JK, Mkapa, Kinana na waliobaki Ccm, akiwa Chenge, Tibaijuka na wengine wengi tu. Mnajaribu kumsema kwa mabaya Lowassa lakini yuko fit.
Ccm mnateseka sana mwaka huu
 
Polepole anataka kutuambia hata elimu bure eti haiwezekani,huyu mtu ni mjinga kiasi gan?km kuna ufisadi mkubwa unaofikia trilion 18 kw mwka,ukijumlisha misamaha ya kodi,ukwepaji wa kodi,wizi km escrow n.k pesa zote hzo zikidhibitiwa,utashindwaje kutoa elim bure?anawaambia watz eti elimu bure haiwezekani ni uzalilishaji.Huu ni ujinga wa polepole,unaweza ukawa msomi lkn ukabaki na ujinga.
 
Polepole anataka kutuambia hata elimu bure eti haiwezekani,huyu mtu ni mjinga kiasi gan?km kuna ufisadi mkubwa unaofikia trilion 18 kw mwka,ukijumlisha misamaha ya kodi,ukwepaji wa kodi,wizi km escrow n.k pesa zote hzo zikidhibitiwa,utashindwaje kutoa elim bure?anawaambia watz eti elimu bure haiwezekani ni uzalilishaji.Huu ni ujinga wa polepole,unaweza ukawa msomi lkn ukabaki na ujinga.

Tumwoneshe kuwa Elimu bure inawezekana kwa kufanya mabadiliko
 
Back
Top Bottom