KALINZI NYUMBANI
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 2,066
- 2,147
Tunahitaji vijana wazalendo kama Polepole ambao hawaendeshwi na mihemuko.
Watanzania Wa Leo wameshaujua ukweli dhidi ya Richmond na wanajua bayana kuwa nani mhusika, na ndiyo maana Watanzania hawataki kusikia kuhusu upuuzi wa Richmond na ujinga mwingine, alishasema kuwa Mamlaka za juu ndiyo zinahusika.
Tundu Lissu alishasema pia kuwa JK anahusika nayo
Nashangaa unajipa moyo na unakufa na yai shingoni. Kila uchao tuhuma zinapotolewa huwa zinaondoka na wanachama wengi sana huwezi amini. Utashangaa. Utapiga kura wewe usishangae hata mkeo labda atampigia Magufuli.Hata aletwe malaika kumchafua Lowasa tutamchagua tuuu. Nguvu Kubwa inayotumika na CCM haitashinda.
Watanzania wa leo ndio sisi na tunajua kuwa Richmond lowasa alipiga dili hata kikwete alisema kwwnye mkutano wa kampeni
Hata dr slaa alisema anao ushahidi wote kuhusu richmond na lowasa
Dr mwakyembe ndio usiseme kabisaa. Ushahidi upo na kesi itafunguliwa wakati wowote.
Mchungaji mtikila alisema ushahidi anao ndio maana alikuwa anajiandaa kumpeleka mahakamani lowasa., bahati mbaya wamemuwahi.!
Sasa kamanda unatuambia nini
Ccm wanatumia njaa zetu kututawala ,ipingen njaa popote pale mtakapo isikia
Tunahitaji vijana wazalendo kama Polepole ambao hawaendeshwi na mihemuko.
Wananchi tuwe macho mchana na usiku tusije chagua mtu yeyote ambaye alihusika kukataa maoni yetu ya Katiba mpya kwani anatudharau na hatutakii mema. Hasa waie wahusika wakuu.
Hivi Kingunge anamtumikia nani? Gwajima analipwa na nani? Haya maswali nyumbu hawapendi kujiuliza
Kuna mambo mengi ambayo tunatakiwa kuhoji kama wananchi, mbali na kujiuliza kuwa Humphrey pole pole yupo kwa masilahi ya nani, lakini pia tujiulize, Gen. Davis Mwamunyange yuko wapi?
POLEPOLE UNAMTUMIKIA NANI?
Na Ally Rama.
Nimetoka kuangalia mdahalo kuhusu amani; umoja na haki kupitia star TV pale ubungo blue pearl hotel..
Kwa title ya mdahalo; niliamini watajadili kuhusu haki; umoja na amani lakini wakajielekeza kwenye uchaguzi mkuu bila kugusa vipengele husika..
Miongoni mwa hoja zilizotawala mjadala (si kwa Bahati mbaya) ni mjadala Wa urais kati ya wagombea wawili Magufuli na lowassa..
Polepole kwa nafasi yake; aliendelea kuonesha chuki zake kwa lowassa na alitumia mchakato Wa kupata katiba mpya kuelezea namna Lowassa alivyohujumu mchakato ule hivyo hafai kuwa rais na huo ndio ugomvi wake na lowassa ulipoanza..
Polepole kwa maelezo yake anasema; Lowassa ndie aliharibu mchakato na akaratibu harakati za kupinga kupatikana kwa katiba ya wananchi kwa kigezo cha kuwa mapendekezo Yale yanadhoofisha taasisi ya Urais..
Akaendelea kudai; walienda kumuomba akubali maoni yao lakini akakataa..
Nikaanza kuukumbuka mchakato ulivyokaenda na nikaja na maswali yafuatayo..
1: Lowassa ndani ya CCM hakuwa mwenyekiti wala katibu mkuu..
ndani ya serikali hakuwa hata Waziri..
Sasa nguvu ya kuhodhi mchakato ule bungeni aliitoa wapi?
2: hasimu wake kisiasa Mzee Sitta ndie Alikuwa mwenyekiti Wa bunge maalum la kufinyanga katiba ya wananchi..
Nae aliingizwa king na Lowassa??
3: mama Samia Suluhu Hassan ambaye leo ni mgombea mwenza Wa magufuli; nae aliingizwa king na lowassa afinyange katiba?
4: Mwigulu Nchemba; January na Vijana wengine Makini ndani ya CCM waliipinga rasim ya warioba; nao waliingizwa king na lowassa?
5: inajulikana hata adui mwingine Wa lowassa; paul Makonda alishadadia swala la kifinyanga maoni ya wananchi hasa kwenye kipengele cha muundo Wa muungano..
Akampiga Mzee warioba...
Akazawadiwa ukuu Wa Wilaya ya kinondoni..
Nae aliingizwa king na lowassa??
6: membe nae alipinga muundo Wa muungano..
Nae aliingizwa king na lowassa??
7: Mzee kikwete km rais Wa nchi aliishiwa nguvu ya kuhimili mihemko ya wabunge Wa CCM hadi akaelekea kibra..
Nae aliingizwa king na lowassa??
Aliwazawadia ukuu Wa wilaya Akina Makonda kwa kupinga katiba ya warioba..
Nae aliingizwa king na lowassa??
Eti kweli lowassa pekee ndie alikwamisha mchakato ule?
Kakangu Polepole; hebu kuwa mkweli hapa...
Hao unaowapigia kampeni ndio walokwamisha mchakato Wa katiba mpya..
Polepole Vaa uzalendo; Vaa utanzania..
Zungumza ukweli..
La sivyo tuambie unamtumikia nani??
Ni wazi kuwa Pole Pole hana Moral Authority ya kuwaambia Watanzania kuwa Lowassa aliingilia Mchakato wa Maoni ya Watanzania katika kuipata Katiba Mpya, Mchakato wa kuipata Katiba Mpya kama ni kukwamisha nadhani arudi kwa Mwenyekiti wa Ccm ambaye aliridhika na mambo ya kihuni yaliyopelekea kuvunja utu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Time ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.
Pole pole alikuwa mfuasi wa Katiba ya maoni inayoungwa Mkono na Wananchi ya Serikali tatu na aliipigania sana na ambayo inaungwa Mkono na UKAWA. Ni ajabu sana kuona anaegemeza matusi na hoja dhaifu kwa Mgombea Urais wa UKAWA ambaye anatetea Katiba aliyoipigania.
Tumpuuze kwa kuwa in dhahiri kuwa anatumika na Ccm.
Edited by,
pg.