Michango na gharama za matumizi ya shughuli za kijamii kwa siku hizi ni maajabu!
Mtu akiugua, watu wanavuta miguu sana kuchangia matibabu.Akifa ndio utashangaa budget zinatengenezwa na michango kuitishwa.
Kinachonishangza ni ile budget ya kupiga picha za video za tukio zima.Hii iko hadi vijijini!
Cha kujiuliza - hivi, watu hasa wafiwa huangalia lini hii mikanda na kwa kuangalia inamaanisha nini?
Ni kuiga wazungu basi hakuna lingine hapo
hayo ya mikanda mimi nimejiuliza sana sijapata jibu..............................
watu wanaenda salon kushonea weaving na mambo mengine ya urembo............. hapo kafiwa na baba, mama, kaka etc......
yaani siku hizi ladha ya misiba imepotea kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hizi video zinaweza kusaidia uchunguzi/upelelezi kwa vifo venye utata!
unaangalia mkanda wa mazishi ili ukumbuke nini? ...binafsi sioni sababu ya vdeo. Kwenye mazishi,ni umbea tu baada ya mazishi oh, mbona nimeangalia mkanda sikukuona kwenye mazishi ya babangu...nk. Harusi ,b.day sawa .
Humdhalilisha marehemu jamani! Hata mimi hili nalikubali sana. Inasikitisha na kukasirisha maana hakuna kumsitiri marehemu.Ni kweli tunaiga ila wenzetu mazishi yao jeneza huwa limefunikwa na watu wanalia ila hawapigi mayowe. Yaani ukiangalia video au picha, ndio inahuzunisha ila haiogopeshi. Sasa ssisi kibongobongo tunampiga marehemu picha ndani ya jeneza tena wanamkuza kabisaa......nilikwenda kumpa pole ndugu yangu mmoja alifiwa basi ile nafika tu napewa album(sikuwepo kwenye mazishi), kwani niliweza kuangalia basi? nimefungua kurasa mbili tu nikafunga, hata ndugu yangu mwenyewe hakuweza kutizama. So maybe its ok kupiga picha ila upigaji uzingatie kumstiri marehemu.
starling..........
story by.......
scirpt writer........
casting..1,2,3,4,5,6,7,
director.............
makeup............
sound......
editor.........
location........
etc.etc.........
the end
Je umewahi kusikia hata kesi moja ilitolewa ushahidi wa mkanda wa video?
Huweza kuchochea uhasama...pwenti hii!
Humdhalilisha marehemu jamani! Hata mimi hili nalikubali sana. Inasikitisha na kukasirisha maana hakuna kumsitiri marehemu.
Jamani wewe! Ni sinema kumbe!