Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

Biden kasema anafanya kazi kwa karibu na ujerumani kuhakikisha Nord 2 (bomba la gesi halisainiwi).
 
Nilikuwa nasubiri hii speech ya Biden. Yaani nilikuwa nasubiri sentesi moja tuu kuwa we will protect Kiev militarily ila sijaisikia zaidi ya sanctions...more sanctions hahaaa...US kikaangoni.
 
Mkuu TUJITEGEMEE , Anthony Blinken kapiga simu Beijing kuomba wasadie kulinda uhuru wa Ukraine. Yaani Marekani atakuwa kwenye hali mbaya sana kama Uchina atakuwa upande wa Urusi: Uchina bado hajasema chochote, wala kuchagua upande mpaka sana. Tusubiri
Mkuu michango yako ni shule tosha kwangu bila shaka na kwa wengine wengi...ni kati ya WanaJF wachache ndani hili jukwaa la Kimataifa unaeongea kitu chanye uhalisia.

Alikuwepo na Mwana JF mmoja Dotworld sijui alipotelea wapi, nae alikuwa mjuvi sana wa siasa za Urusi na Marekani.
 
Ujerumani imekuwa na udhaifu na utegemezi wa gesi na mafuta kutoka Urusi kwa miaka zaidi ya 100. Prof Daniel Yergin kwenye kitabu chake "The Prize" anasema kwamba moja ya sababu zilizomfanya Adolf Hitler avamie USSR ilikuwa ni kuteka visima vya mafuta, gesi, migodi ya chuma na mashamba ya mpira. Angefanikiwa kupata rasilimali za USSR ndipo angenza kupambana na dunia yote.

Italia wamesema wanaitaka sana gesi ya Urusi, hivyo ni suala la muda tu wengine nao watajiunga. Hivi unadhani wazungu ambao wanavamia nchi za kiarabu kuiba mafuta, watakataa gesi ya Urusi kisa Donbas ?? Tusubiri tuone
Warusi wameongeza thamani ya bei ya gesi wanayoiuza Ulaya. Ujerumani amecheza karata yake ya kuusinzisha mkataba baina yake na Urusi. Na kama ulivyosema Ujerumani kwa kipindi kirefu anaitegemea Urusi kwenye hiyo sekta. Grafu ya gesi gharama yake ipo juu kwa nchi za Ulaya ikiwemo Ujerumani. Kwa Urusi kupandisha thamani ya mauzo yake ya gesi nao ni mtego kwa Kansela wa sasa wa Ujerumani. Sidhani kama raia wanaweza kuhimili upandaji wa gharama hiyo naiona kama harufu ya maandamano Ujerumani.

Namuona Ujerumani yupo kwenye wakati mgumu.
 
RAISI VLADMIR PUTIN AMEAMURU URUSI IPELEKE VIKOSI DONBASS:

Baada ya eneo la Donbass kuwa huru, Raisi wa Urusi amempa maelekezo Waziri wa Ulinzi kupeleka vikosi vya kutunza amani na usalama kwenye nchi mpya ambazo ni za Donesty na Lugansk. Pia katoa maelekezo waanzishe mazungumzo ya haraka na nchi hizo ili kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia.

Yaani hajatumia kabisa kuimega Ukraine maana kwenye sheria za kimataifa hajafanya lolote lile. Mikataba ya Umoja wa Mataifa inatambua haki ya watu kujitawala wenyewe (A Right to self-determination). Yaani, hii kwenye mchezo wa CHESS tunaita CHECK-MATE, Urusi ametumia mchezo wa Marekani kumshinda Marekani. Tena kafanya kisasa, bila kumwaga damu kama Marekani.....


Hebu tuone Marekani na washirika wake watafanya nini kukabiliana na hili......
Niwe mkweli; haya masuala unayajua kuliko mimi/sisi. Sifahamu dunia inaelekea wapi ila kwa lugha nyepesi napata tabu Sana.

Russia ama Putin leo ametoa kauli nzito sana baada ya kutoa ufafanuzi sababu ipi inayopelekea Russia kutuma majeshi yake kulinda amani majimbo yaliyojitenga kutoka Ukraine na katoa onyo ya kuwa: "Yeyote atakayejaribu kutuzuia na kuleta tishia kwa nchi ya Urusi na kwa raia wake afahamu ya kuwa Urusi itajibu mapigo kwa haraka na kukuletea athari/sintofahamu ambayo hamkuwahi kukumbana nayo kamwe, na tupo tayari kwa matokeo ya aina yoyote."

Lakini kabla ya hapo aliwatahadharisha majeshi ya Ukraine kuwa lililobora kwao warudi majumbani mwao wakae na familia zao.

Tukirudi nyuma huu mgogoro ni mkubwa kwa maana umejumuisha mataifa makubwa tofauti tofauti. Kuna NATO, kuna Umoja wa Ulaya..kuna (na Marekani ijapokuwa ipo ndani ya NATO), Urusi jumlisha na Ukraine ambaye ndiye uwanja wa hii kadhia. Ukimsikiliza Putin mwisho wa hotuba yake kaishia na wanajeshi wa Urusi kwa utiifu wao ana imani watatimiliza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

Tunaona nguvu za kijeshi na kiuchumi kutumika. Nahitaji kujua, hii dunia kwa sasa inaelekea wapi?
 
Mkuu michango yako ni shule tosha kwangu bila shaka na kwa wengine wengi...ni kati ya WanaJF wachache ndani hili jukwaa la Kimataifa unaeongea kitu chanye uhalisia.

Alikuwepo na Mwana JF mmoja Dotworld sijui alipotelea wapi, nae alikuwa mjuvi sana wa siasa za Urusi na Marekani.
I'm humbled you know.....
 
Urusi leo tena imeshambulia kinu kikubwa Cha nuclear nakukiweka under control baada ya wiki iliyopita kutwaa chenobry hii sass hatari na nadhani naanza kuelewa maana ya military operation anayoizungumzia bwana Putin
 
Back
Top Bottom