Swali gumu kidogo: Kwanini Urusi iliyosambaratika na dhaifu kuliko USSR inawasumbua sana NATO?

RAISI VLADMIR PUTIN AMEAMURU URUSI IPELEKE VIKOSI DONBASS:

Baada ya eneo la Donbass kuwa huru, Raisi wa Urusi amempa maelekezo Waziri wa Ulinzi kupeleka vikosi vya kutunza amani na usalama kwenye nchi mpya ambazo ni za Donesty na Lugansk. Pia katoa maelekezo waanzishe mazungumzo ya haraka na nchi hizo ili kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia.

Yaani hajatumia kabisa kuimega Ukraine maana kwenye sheria za kimataifa hajafanya lolote lile. Mikataba ya Umoja wa Mataifa inatambua haki ya watu kujitawala wenyewe (A Right to self-determination). Yaani, hii kwenye mchezo wa CHESS tunaita CHECK-MATE, Urusi ametumia mchezo wa Marekani kumshinda Marekani. Tena kafanya kisasa, bila kumwaga damu kama Marekani.....

Hebu tuone Marekani na washirika wake watafanya nini kukabiliana na hili......
Shukrani sana Mkuu nilikuwa nasubiri uchambuzi wako. Mpaka sahivi nimeshindwa kulala sijajua nini kitaendelea huko.
 
Shukrani sana Mkuu nilikuwa nasubiri uchambuzi wako. Mpaka sahivi nimeshindwa kulala sijajua nini kitaendelea huko.
Sifahamu nini kitaendelea, lakini Marekani amewekwa kwenye kikaango kibaya sana: Kuvimbisha misuli ili atunze uso wake mbele ya Ulaya au Kufyata mkia kwa kufanya APPEASEMENT POLICY kama Neville Chamberlain alivyofanya mwaka 1939 baada ya Ujerumani kuvamia Czechslovakia. Akivimba msuli na kufanikiwa, basi atatuma ujumbe hadi Uchina kuhusu kuvamia Taiwan, pia hata kumuogopesha Serbia kuvamia Kossovo.

Ujumbe tunaoupata hapa ni huu: Kama Marekani akishindwa kuilinda Ukraine, unadhani ataweza kuilinda Taiwan ??? Binafsi sina jibu la moja kwa moja, kwasababu mazingira ya kisiasa barani Ulaya na Mashariki ya mbali yako tofauti. Ulaya mataifa mengi hayako na Marekani kwenye baadhi ya sera zake, na tofauti kabisa na zamani, siku hizi Ukomunisti haupo hivyo nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kukaa na kuzungumza na Urusi na kuelewana.

Nchi kama Ufaransa na Ujerumani zinacheza karata vizuri kwasababu zitapata faida kubwa sana endapo Marekani atadhalilika na ushawishi wake kupungua barani Ulaya. Ikumbukwe Umoja wa Ulaya ulitaka kuanzisha jeshi lake tangu miaka ya 50's kipindi cha Jean Monnet na Charles De Gaulle lakini aliyewafitini kufanya hivyo ni Marekani kwa kuleta NATO.

Wafaransa walichukia kiasi cha kufanya vituko hadi kujitoa NATO. Mpaka mwaka majuzi kwenye bunge la Ulaya Nigel Farage alikuwa anamshambulia sana Ulsura Von Deleyen alivyotoa pendekezo la kuanzisha jeshi la Ulaya. Usione Macron na Olaf wanaenda sana Urusi, na kujihusisha sana na Putin, huu mgogoro una maslahi sana kwao. Tena wao ndiyo wana mkono wa juu kuliko Marekani kwasababu Uingereza haimo tenda ndani ya UMOJA WA ULAYA.

Sasa ili Marekani afanikiwe kwenye hili anahitaji azungumze kwa sauti moja na kutenda kwa nguvu moja na wenzake wa nchi za Magharibi (The Atlantic Alliance), lakini bahati mbaya haipo hivo kama zamani. Nchi kubwa ndani ya Umoja wa Ulaya kama Ujerumani na Ufaransa zina maslahi yao binafsi, pia kwao Urusi ni changamoto wanayoweza kuimudu.

Mashariki ya mbali kuna utofauti kidogo na Ulaya. Tofauti na Urusi, Uchina anapambana mataifa mengi ambayo anagombania nayo mipaka, hayana umoja wao, huku yakiendeshwa na rimoti ya Marekani kutoka Washington. Hapa Marekani yuko na mkono wa juu, shida inakuja pale ambapo mataifa haya yote yamefungamana sana kiuchumi na Uchina. Hebu ona:

Ukiitoa Vietnam peke yake, nchi kubwa Mashariki ya mbali kama Japan, Korea-Kusini, Singapore, Ufilipino na Australia wanaongozwa kijeshi na Marekani. Hebu fikiria haya yafuatayo, ndiyo uone jinsi gani Marekani ni muhuni:
1. Japan - Hana jeshi anategemea Ulinzi kutoka Marekani.
2. Korea Kusini - Ana jeshi lakini linaongozwa na Majenerali wa Marekani.
3. Australia - Iko chini ya Uingereza
4. Ufilipino - Lilikuwa ni koloni la Marekani.

NB: Hivyo Marekani anaweza kucheza vizuri na Mashariki ya mbali, kuliko Ulaya kwasababu kule mbali na kuwa na vikosi vya jeshi nchini Ujerumani, hawezi kuwapelekesha wajerumani endapo watamkazia. Pia Ujerumani haina tatizo na Urusi kwasababu wanahistoria ndefu ya pamoja, tofauti kabisa na Japan ambao hawapikiki chungu kimoja na Uchina.

Sasa mpira kapewa Marekani, tuone atachezaje: Maana vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi haviwezi kufanya kazi kwasababu ili vifanye kazi ni lazima nchi zote za Umoja wa Ulaya zikubali kupambana na Urusi, kitu ambacho siyo rahisi, japo kinaweza kutokea.
 
Ametangaza kuyatambua majimbo ya Donbass (Lugansk and Donestky) kama nchi huru,
Nilitegemea media za magharibi zilete habari hii kwanza kwa sababu ndiyo walikuwa wanapanga na kutangaza tarehe lini Russia anaivamia Kiev. Sasa, naanza kuamini maneno ya mrussia kuwa wamefyeka mules kibao wa Marekani kwenye mifumo yake.
 
Marekani alikuwa anafahamu kwamba Urusi lazima atatumia nguvu ya kijeshi, aidha kwa kuanzisha vita ya kivamizi (A War of Aggression). Lakini Urusi hajanasa kwenye huo mtego. Ametumia diplomasia na sheria za kimataifa kuhalalisha vikosi vyake kuingia nchini Ukraine bila kurusha risasi hata moja.

Anachokifanya Urusi tunaita The Salami Slicing Tactic, kwamba adui anakukata kidogo kidogo, mwishowe unakuta una vidonda mwili mzima na damu imetoka ya kutoasha. Alianza na Crimea mwaka 2014, leo 2022 yuko Lugansk na Donestky. Sasa anachofanya Vladmir Putin ni kuionesha dunia na raia wa Ukraine kwamba serikali ya Zelensky ni dhaifu.

Kinachoweza kutokea ni kwamba Zelensky anaweza kuwekwa pembeni aidha na wananchi wake au Wamarekani, na wakachagua (ULTRA-NATIONALIST NEO NAZI) kama Mikhail Saakhashvilli kule Georgia anayeweza kuvimba kwa Urusi. Sasa kiongozi huyo akichaguliwa akianza kutumia nguvu kuwatesa Warusi walioko Ukraine au kuyadhibiti majimbo ya Donbass, au kuiingiza Ukraine NATO hapo ndipo Vladmir Putin atapata uhalali wa kisheria na kidiplomasia mbeya ya jumuiya ya kimataifa ili kuvamia Ukraine.
 
Mkuu TUJITEGEMEE imefahamika kwamba eneo la Donbass lina majimbo mengine ya Lahansk and Donetsky ambayo yako chini ya Kiev. Imeshaanza kupendekezwa na wanasiasa wenye mlengo mkali kwamba nayo itabidi yatambulike na serikali ya Urusi. Ndiyo maana nikasema, mchezo umekuwa mbaya na Urusi hataaishia Donbass, anasubiri wafanya makosa apate sababu, aidha kupitia vurugu za ndani (Internal Chaos) au uvamizi (Military Invasion).

Marekani na Uingereza mpaka sasa wametishia vikwazo tu, na ishaonekana kwamba hawawezi kufanya jambo lolote lile kijeshi dhidi ya Urusi. Umoja wa Ulaya nchini ya nchi kama Ujerumani na Ufaransa ndiyo wanaweza kugeuza huu mchezo ukawa mgumu kidogo kwa Urusi: Lakini bila wao, sidhani kama Marekani na Uingereza wanaweza kufanya chochote kile kikubwa.
 
Umoja wa Ulaya nchini ya nchi kama Ujerumani na Ufaransa ndiyo wanaweza kugeuza huu mchezo ukawa mgumu kidogo kwa Urus
Ni kweli mkuu. Hata hivyo, naona Ujerumani anataka kufanya jambo la ajabu. Eti anakataa kuidhinisha mradi wa bomba la gesi kutoka Russia usianze.

Naliita jambo la ajabu kufanywa na nchi kama Ujerumani kwa sababu Hili likitekelezwa, litakuwa lina hatarisha uaminifu wa serikali ya Ujerumani kwa wawekezaji wanaojielewa. Wawekezaji hawa watawaza mara saba kabla ya kufanya mapatano na serikali ya nchi hiyo kuhusu masuala ya uwekezaji. Maana risk ya Ujerumani kuwabadilikia itakuwa kubwa kama inavyotaka kutokea kwa Gasprom ya Russia na makampuni mengine makubwa ya nishati Ulaya yaliyohusika kulaza bomba hilo la gesi.

Mkuu, inasemekana, Donobass ni mjumuiko wa LPR na DPR. Hivyo, kwa pamoja wanaitwa hivyo.
 
Uingereza ameshaweka vikwazo kwa benki kubwa tano za urus pamoja na matajir watat wanaosapot viongoz wa majimbo yaliyojitenga
Walifanya hivyo hata mwaka 2014 lakini ilifika wapi ??? Uingereza na Marekani hawawezi kucheza huu mchezo peke yao bila ushirikiano wa asilimia 100% kutoka Umoja wa Ulaya.
 
Naliita jambo la ajabu kufanywa na nchi kama Ujerumani kwa sababu Hili likitekelezwa, litakuwa lina hatarisha uaminifu wa serikali ya Ujerumani kwa wawekezaji wanaojielewa. Wawekezaji hawa watawaza mara saba kabla ya kufanya mapatano na serikali ya nchi hiyo kuhusu masuala ya uwekezaji. Maana risk ya Ujerumani kuwabadilikia itakuwa kubwa kama inavyotaka kutokea kwa Gasprom ya Russia na makampuni mengine makubwa ya nishati Ulaya yaliyohusika kulaza bomba hilo la gesi.
Kwahiyo Ujerumani atanunua gesi kutoka Marekani ??? Hebu tuone...

Mkuu, inasemekana, Donobass ni mjumuiko wa LPR na DPR. Hivyo, kwa pamoja wanaitwa hivyo.
Nafahamu mkuu, nachokisema ni kwamba LPR na DPR kabla ya mwaka 2014 zilikuwa na eneo kubwa zaidi ya eneo ambalo wanalo leo. Maeneo mengine ya Donbass (LPR na DPR) yamekaliwa na vikosi vya serikali ya Kiev. .
 
Kwahiyo Ujerumani atanunu gesi kutoka Marekani ??? Hebu tuone...
Tena Medvedev kasema watainunua kwa bei ya mara mbili kuliko ya sasa.

Halafu, Ulaya wanasema wanajari mazingira, wakati kutumia LPG hasa inayotokana na " cracking of rocks/ shale gas" kunachafua zaidi kuliko kutumia Natural Gas. Nilitegemea waendeleze huu mradi kwa udi na uvumba.
 
Duh! Hapo Ukraine kwisha habari yake. Na majimbo haya nasikia yalikuwa injini ya uchumi wa Ukraine.
 
Tena Medvedev kasema watainunua kwa bei ya mara mbili kuliko ya sasa.

Halafu, Ulaya wanasema wanajari mazingira, wakati kutumia LPG hasa inayotokana na " cracking of rocks/ shale gas" kunachafua zaidi kuliko kutumia Natural Gas. Nilitegemea waendeleze huu mradi kwa udi na uvumba.
Ujerumani imekuwa na udhaifu na utegemezi wa gesi na mafuta kutoka Urusi kwa miaka zaidi ya 100. Prof Daniel Yergin kwenye kitabu chake "The Prize" anasema kwamba moja ya sababu zilizomfanya Adolf Hitler avamie USSR ilikuwa ni kuteka visima vya mafuta, gesi, migodi ya chuma na mashamba ya mpira. Angefanikiwa kupata rasilimali za USSR ndipo angenza kupambana na dunia yote.

Italia wamesema wanaitaka sana gesi ya Urusi, hivyo ni suala la muda tu wengine nao watajiunga. Hivi unadhani wazungu ambao wanavamia nchi za kiarabu kuiba mafuta, watakataa gesi ya Urusi kisa Donbas ?? Tusubiri tuone
 
Kuna viwanda vikubwa na migodi mikubwa ya chuma na makaa ya mawe. Jina lenyewe Donbas linatokana na neno "Coal Basin". Hatari tupu...
Ndiyo maana UK na US walita Kiev ayachukue kinguvu asayape kabisa mamlaka ya ndani majimbo haya.
===
Mkuu, Hivi US na wenzake wanaweza kuiruhusu Kiev (Maana Ukraine imebaki jina) irejeshe uwezo wake wa nyuklia kuikabili Russia katika mazingira ya sasa?
 
===
Mkuu, Hivi US na wenzake wanaweza kuiruhusu Kiev (Maana Ukraine imebaki jina) irejeshe uwezo wake wa nyuklia kuikabili Russia katika mazingira ya sasa?
Mkuu, sifahamu nini kitatokea mbeleni, japo nachofahamu ni kwamba kulikuwa na makubaliano mwaka 1994 (The Budapest Memorandum on Security Assurances) ambao ulisainiwa na Belarus, Kazakhstan, Ukraine, Urusi, Marekani na Uingereza.

Kwamba haya mataifa matatu (Belarus, Kazakhstan na Ukraine) hayatakuwa na silaha za nyuklia huku Urusi akiahidi kuheshimu mipaka ya nchi hizo endapo wataziondoa silaha za nyuklia. Lakini kubwa pia ni kwamba haya mataifa matatu tayari ni wanachama wa mkataba wa Nuclear Non-Proliferation Treaty.

Ukraine, Kazakhstan na Belarus wana uwezo wa kuwa nchi za kinyuklia, lakini unadhani Urusi atawaruhusu wafanye hivyo ??? Kiongozi wa Marekani leo kasema hawana mpango wa kuifanya Ukraine liwe taifa la kinyuklia. Ila tusubiri
 
Walifanya hivyo hata mwaka 2014 lakini ilifika wapi ??? Uingereza na Marekani hawawezi kucheza huu mchezo peke yao bila ushirikiano wa asilimia 100% kutoka Umoja wa Ulaya.
Tangu mwanzo ujeruman alikua mzito sana kutoa silaha kwa ajili ya Ukraine mpaka alipopata mualiko wa white haus ndipo alipoanza utoaj.

Na sidhan km ujeruman atakubal kuiacha gesi ya urus yenye gharama kidogo afakamie gesi ya mbali kwa gharama kubwa kwa maslah ya wengine
 
Borrell kasema EU wataiwekea Urusi vikwazi vinavyouma. Ujerumani katishia kwamba Nord Stream 2 hawataendelea nayo.
 
Back
Top Bottom