Swali Gomvi: Ni nani Unayemwamini na Kwanini?

Kuhusu sakata la mchanga wenye madini; ni nani unayemwamini kuwa anasema kweli?


  • Total voters
    90
  • Poll closed .

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Ni nani unayemwamini? Wawekezaji wanaosema "hatukudanganya" au Serikali inayosema "Wamedanganya" na kwanini? Yule usiye mwamini ungependa afanye nini ili umuamini kuwa anachosema ni kweli?

Unaweza kupiga kura hapo juu lakini hapa chini unaweza ukadadavua sababu zako ili tuzidi kubadilishana mawazo na mitazamano na kushawishiana kwa hoja na si vihoja.
 
1. ACACIA's too little, too enclosed, too much NDA-ish. Too much questionable, too much 'we didnt' than this is what has been done
2. Committee's bloated, too much (ultra-)resource nationalistic. Sentimental, attention seeking of sorts, ugly we-couldve-done-it-ourselves attitude that works not in these times.

None of which makes any bloody sense!
 
Acacia wanadanganya hao. Walivyo waona wale wenzetu tuliowaweka pale kuwa angalia wasituibie, wakaziona njaa zao, Tizama, waliwalambisha muwa wakajisahau kutazama kazi zao, wakabaki kuguguna muwa. Mali si zikapita?? Ndo maana JPM kasema, wachunguzwe, wakibainika wapelekwe mahakamani. Tunmatizamia watu wafilisiwe.
Serekali, imechukua maamuzi ya haraka mno. Wangekaa chini, wajadiliane jambo hili ndani ya ukumbi maalum uliosheheni wanasheria. Kwa kuwa hili jambo ni la kisheria. Wakiona tutashinda ndio wamshauri JPM akamate makontena husika.
Lakini, kama kweli uchunguzi uliofanywa utaonesha hata robo kilo ya madini ambayo hayaku be declared na ACACIA, nasema, B/up sana JPM.
 

Hakuna shaka kwa hapa tulipofikia Lazima kuiamini serekali KIKAMILIFU!


Hao ACACIA sio wakuamini kabisa anyway kwanini wasijitetee ..! Kwa uharamia wa wazi kabisa wanaofanya.

Watanzania lazima kuwa wamoja na kushikana kwenye hii vita sio vita ndogo. Inabidi kuweka tofauti zetu zote kando na kuja pamoja kwenye hili kama Taifa.
 
Nawaamini acacia kwa sababu procedure za kuchukua sampuli, kukokotoa 'grade, tonnage, metal content & recovery' ni za uwazi na zinakubalika kimataifa tena hizo parameters zote zinapatikana kwa kuzishirikisha idara za serikali kama TRA, TMAA, mineral residential officers etc baada ya kuchukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara za nje na ndani!
Nina uhakika kabisa nikimuuliza Mruma amepata vipi hizo data kutoka kwenye makontena zaidi ya 200 alizo mkabidhi muheshimiwa na kuutangazia umma wa watanzania anaweza kujikojolea kama si kuji***a kabisa!
 
Naiamini serikali kwasababu imeundwa tume makini iliyokuja na issues zilizolalamikiwa miaka mingi. Statement ya ACACIA ilikuwa na lengo la kutuliza upepo huko kwenye stock exchange while trying to solve the issue ....
 
ACACIA Wana hoja ya msingi. Ila huwezi amua nani wa kumwamini mpaka ipatikane ripoti kamili inayoonyesha "among other things", methodologies, who and where the samples were analyzed, credibility(international) of the analyzer and other things. Tatizo la watanzania walio wengi wanachukulia haya mambo kiurahisi-rahisi. Kwenye mambo haya kama tukiangukia pua tutaomba ardhi ipasuke tujifiche na haitapasuka. Tunatakiwa kuwa na proper legal standing na sio siasa.
 
Naiamini serikali inaposema tulidanganywa sana na kwa muda mrefu tumeibiwa sana. Tatizo ni kwamba kwa sababu ya uongozi mbovu katika sekta ya madini tumeibiwa huku tunaona tena huku sheria ikionekana kuwa na uwezo wa kuwalinda wawekezaji "majizi" sababu ya mikataba mibovu tuliosaini.

Nashauri kuwa namna nzuri ya kushughulika na majizi haya ni kuvunja mikataba kisheria na hata kwa gharama itumike ili kujitoa kwenye makubaliano mbali mbali yanayolinda majizi, bila kuvunja sheria.
 
Kabla niliwaamini acacia kwa sababu data zao zilifanana kwa karibu na watu wa TMAA na watu waliowahi kutumwa na serikali kutafiti makinikia 2011 Ila sasa naiamini tume ya Magufuli Bila Shaka, ntabadilika ikitokea wamekuwa challenged kwa tafiti na takwimu za kisomi huku wao wakishindwa kutetea walichokigundua.
 
..suluhisho ni serikali kuchukua jukumu la kusafirisha, kutafuta smelter ya kuchambua mchanga, na baadaye kuuza kilichomo ktk mchanga huo. Baada ya hapo wawakatie acacia kiasi chao, na sisi tusepe na kilicho chetu.

..halafu naona tumebeba bango kuhusu mchanga. Je dhahabu inayochimbwa tumejiridhisha kwamba hawatupunji?

Cc Nguruvi3
 
Mie nafikiria wewe unajitoa ufahamu
Unaongelea Sampuli, kukokotoa, grade, tonnage, metal content and recovery...........
Wakati sampuli iliyochukuliwa na tume imeleta matokeo tofauti...
Tonnage wamekuta container lina mpaka tons 23 over
Tume imekuta madini aina chungu nzima ambayo hayakuonyeshwa kwenye document tangu wameanza kuchimba,
Mbona bado wenye migodi lazima wajambe cheche.
Wakitoka kwenye dhahabu wanahamia kwenye Tanzanite
 
Tume haikuwa huru. Imeundwa na Magufuli wakati ambapo Magufuli alishasema wazi msimamo wake hasi dhidi ya haya makampuni. Wajumbe waliounda tume iliyochunguza hili sakata walionekana wazi wakati wa kuwasilisha kwamba walikuwa na shauku ya kumpa Magufuli matokeo aliyoyatarajia (kwamba ACACIA ni wezi). Kwa kifupi, ilihitajika tume huru, siyo tume ya kuteuliwa na upande mmoja.

ACACIA. Sina sababu ya kuwaamini. Sina sababu ya kuwatilia mashaka pia. Sijaona ushahidi wa kimahakama wa ACACIA kuwa wezi. Ninachosikia ni tuhuma tu dhidi yao.

The whole thing smells like a political stunt by the accuser.
 
Reactions: SMU
kwenye mambo ya trust, the most trusted ni the most experienced! .

Hii iliwahi kutokea hapa
Kauli tata za Mkulu
Kwenye hili la mchanga wa madini, the gap ya 10X ni too big and too good to be true. Let's wait and see, na ikitokea hesabu hiyo ikawa ni kweli, then hawa Acacia they can just pack and go!. Na tutahakikisha hawaondoki na kitu hadi wa bring back our money!.

Paskali
 
ACACIA hawawezi kuaminika
Walianza na kukwepa kodi kwa kutoa taarifa ya uongo TRA,wakajisahau wakapeleka taarifa sahihi London stock exchange ili kupata bei nzuri ya hisa.TRA wakapiga kodi kwa kutumia hesabu walizopeleka LSE.
Kama wanaweza kuwa na taarifa mbili za kodi utawaamini vipi watu kama hawa.
Kwa hili tunapaswa kuwa na Magufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…