Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Pamoja na Ripoti 'nzuri' ya PAC chini ya Zitto Kabwe iliyojadiliwa na kuazimiwa na Bunge, mambo yanakwenda tofauti. Wapo watu waliohusishwa na kashfa hiyo ya Escrow lakini CCM na Serikali yake wanaendelea kuwaamini na kusonga nao mbele.
Waziri Muhongo (Profesa Sospeter Muhongo) alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo ya Escrow. Alikuwa Wizara ya Nishati na Madini. Mwaka huu, amerejeshwa tena kwenye Wizara hiyo hiyo kwa cheo kile kile (Waziri).
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndugu Eliakim Maswi naye aliondolewa kwa kadhia hiyo hiyo. Lakini, ameendelea kuaminiwa na Serikali na ni jana tu ameteuliwa kuwa Kaimu Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.
Wapo Wabunge akina Prof. Tibaijuka, Ndugu Andrew Chenge na William Ngeleja ambao wote walihusishwa na kashfa hiyo lakini CCM imeendelea kuwaamini na wameshinda majimboni mwao. Hata viongozi wa kidini na hata wa kimahama waliohusishwa nao wanaendelea kudunda. kimsingi hapa patakuwa na jambo kubwa.
Kama si PAC kuudanganya umma, basi Bunge limepuuzwa vya kutosha. Ndiyo maana najiuliza, sakata la Escrow lilikuwa si kitu halisi yaani abrakadabra?