Dx and Rx
JF-Expert Member
- Jul 16, 2017
- 1,303
- 3,085
Salamu wakuu, naomba kuuliza swali kama linavyojieleza hapo juu. Sio kwa nia mbaya(naomba nieleweke hivi), bali napenda kujua.
Mwaka 2012, Waislamu walifikia hatua ya kususia sensa kwa madai kuwa kwenye dodoso la sensa kulikuwa na kipengele cha nyumba za Ibada(Msikiti, Kanisa) bila kuwepo kipengele cha Dini, jambo ambalo lilitafsirika kuwa kulikuwa na nia ya kupata takwimu za nyumba za Ibada bila kupata takwimu za watumiaji(waumini) wa hizo nyumba za ibada.
Waislamu walileta hoja yao ya kutaka pawepo na kipengele cha dini kwenye dodoso baada ya kuhisi kuwa kuna upotoshaji wa takwimu za idadi ya Waislamu na Wakristo Nchini, sasa kukata huo mzizi wa fitina walishauri kwenye dodoso pawekwe kipengele cha dini ili takwimu sahihi zijulikane ila mamlaka(Serikali) ilikataa kusikiliza hoja yao.
Baada ya hapo Waislamu nchi nzima walianza kuhamasishana kususia Sensa ingawa kuna wapo waliweza kuhesabiwa na wengine hawakuhesabiwa.
Je mwaka huu hii agenda haipo? Takwimu sahihi walizokuwa wanadai kupotoshwa walishapata usahihi wa hizo takwimu?
Nimeamua kuuliza baada ya kuona Shule moja ya Kiislamu inahamasisha Sensa ya Mwaka huu kupitia tangazo lao la kutangaza nafasi za masomo.