Swali chokonozi: Membe ni Jasusi Mbobezi au Doezi?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Nimesoma mahojiano ya Mheshimiwa Membe na Gazeti la Jamhuri akilalama kwamba Marehemu Magufuli alimuwekea roho ya Korosho ili asiwe Katibu Mkuu wa Jumuia ya Madola.Kasema mengi ikiwemo jinsi hiyo “Roho ya Korosho” ilivyopelekea Membe kukosa donge la pesa zinazofikia paundi Bilioni Saba za Common Wealth Fund. Vile vile, amedai marehemu Magufuli alifunga Switch mbalimbali ikiwemo Switch ya mambo ya nje ikiwemo iliyoleta athari mbalimbali ikiwemo kutoenda kwenye vikao vya Kimataifa na kuwaondoa mambo ya Nje akina Liberatha Mulamula na mengine mengi aliyoongelea. Kwa muktadha huu, naomba tu nijadili hili suala la pesa alizozikosa Membe.

Ninapenda kuchokoza mjadala kwa kumuuliza Membe yafuatayo:

1. Mhe.Membe kwa uzoefu wake wa Ujasusi na uhudumu wake katika Wizara ya Mambo ya Nje,unapokabidhiwa pesa kutokana na Idara au Ofisi Fulani pesa hizo zinakuwa zako binafsi au unakuwa unakabidhiwa ili ujipangie mambo kadri unavyoona?

2. Je, Mhe.Membe alikuwa ameambiwa kuwa akishakabidhiwa pesa paundi Billioni saba, hizo pesa zilikuwa zinakuja kutumika Tanzania pekee au Tanzania ingenufaika vipi na pesa hizo anazolalamika Membe kuzikosa?

3. Mhe,Membe analalamika kuwa Marehemu Magufuli alikuwa kama Nyuki kazi zake ikiwa ni kutengeneza Asali, Asali, Asali tu sawa na jinsi Magufuli alivyotumia muda wake wote kutengeneza Miundombinu. Je, pesa zake hizo paundi Bilioni saba zilikuwa ni kwa ajili ya nini?

4. Membe anadai Marehemu Magufuli alifunga Switch mbalimbali ambazo sasa mama Samia anazifungua. Je, wakati wa Uongozi wake na Raisi Kikwete, switch mbalimbali anakumbuka zilipokuwa zimewashwa ndizo ziizoleta kashifa na wizi kama kama wa RICHMOND, DOWANS, AGGREKO na nyinginezo?

5. Je, Membe anapolalamika kuwa Magufuli alizima Switch za Mambo ya Nje, anakumbuka kuwa ni yeye alipata kumuunga Mkono Magufuli kwa kufunga hizo switch kwani katika Serikali yao na Kikwete ilikuwa imefikia mahali Viongozi wanapishana Angani kama Mwewe? Je, alikuwa ametoa kauli kama hiyo ili tu Magufuli aweze kumthibitisha kama Katibu Mkuu wa Jumuia ya Madola au alilenga nini?

6. Je,kwa kutoka Moyoni ni kweli kabisa utendaji wa mama Samia unaweza kulinganishwa na wa marehemu Magufuli?

7. Je, kama Membe anamshutumu Marehemu Magufuli kwa kuhisia kuwa alikuwa anampinga kwa kuhofia kupingwa katika uchaguzi,mbona hatoki hadharani kuongelea suala la Kesi ya Mhe.Mbowe ambayo inaonekana kwa jinsi inavyoendelea kuwa ni ya Kubambika?

8. Je, huyu Membe anadai Magufuli alimchukia kutokana na hofu ya kupingwa katika uchaguzi wa Mwaka 2020, Je, yeye Membe mbona anakaa kimya hata baada ya Kusikia kuwa mama Samia atagombea peke yake hapo mwaka 2025? Je,ikiwa yeye mama Samia ni mtu asiyetaka upinzani ni kwa nini hatoi nafasi wanachama wenzie nao wagombee ili kupima uwezo katika kuwaongoza Watanzania?

9. Membe anadai huko nje, kuna pesa nyingi sana. Je, kwa taaluma yake ya Ujasusi sawia na uzoefu wake, kuna pesa za Burebure hapa Duniani? Kama zipo kwel,i ni kwa nini yeye na Raisi wake Kikwete hawakufanikiwa kuzikomba zote na kuzileta hapa Nchini? Walikosa chombo cha aina gani ambacho walitaka Marehemu Magufuli ampatie Membe aende kuzichota?

Maswali ni mengi sana juu ya mambo aliyoyaeleza Membe. Na ningependa tujadili kauli zake. Tujadili kauli zake za kutaka kuonyesha kuwa Mama Samia ni bora sana kuliko Magufuli? Hivi Ubora wa mama Samia unakuja tu kwa sababu anasafiri nje ya Nchi? Je, taaluma ya ujasusi ni taaluma ya kuwafundisha watu kuwa wadoezi kwa maana ya kujipatia pesa kijanjanja?

Karibuni kwa mjadala.
 
Hakuna Jasusi mropokaji hivyo ila ameishi nao wakati akiwa kwenye nafasi ya serikali alikuwa akifanya kwahiyo hana hadhi ya kuitwa kuwa ni 'Professional Spy' ila inawezekana akawa 'MSALATA' kwa mtindo wa 'KUTIMBULIA' kwa faida ya watu fulani kwa ujira au ahadi ya kupewa kitu au nafasi fulani ya kimaslahi
 
Umeuliza swali moja ulichokifanya ni kubadili maneno tu. Utafiti kazi sana
 
Huyo si jasusi ,bali ni mpika majungu hodari sana.Ana miaka 68 bado hajitambui kabisa.Hapa bongo ,nchi yetu ni ya ajabu sana.Tunapenda kuwasifia wahuni wasio na uelekeo wowote.Eti jasusi mbobezi.Mbona hana hata uelekeo wowote.Hana tofauti na Mambe kimambi tu.
 
Mi nadhani Membe aheshimiwe kwa maoni yake!ametusemea Wengi sana na pia Ameonyesha UOZO wa idara ya kijasusi na DEEP STATE kwa kushindwa kufanya upembuzi yakinifu wa mteule wa ugombea URAISI ANAEFAA Kutuvusha!!!!KWA JPM WALIFELI SANA!HATA MEMBE AMESEMA KWA JPM TULIFELI!!!
 
Point/swali hili linafikirisha na kuchekesha kwa wakati mmoja.Haya Pro Membe njooni hapa mtupe majibu
 
Mi nadhani Membe aheshimiwe kwa maoni yake!ametusemea Wengi sana na pia Ameonyesha UOZO wa idara ya kijasusi na DEEP STATE kwa kushindwa kufanya upembuzi yakinifu wa mteule wa ugombea URAISI ANAEFAA Kutuvusha!!!!KWA JPM WALIFELI SANA!HATA MEMBE AMESEMA KWA JPM TULIFELI!!!

Tunayaheshimu mawazo yake lakini tuna haki pia ya kuhoji sawa na yeye alivyofanya.Kwa hiyo pia wanaohoji alichokielezea Membe mawazo yao pia yaheshimiwe.
 
Membe alicholenga ni kujionyesha ni mtu mwema na mwenye nia njema na nchi,kumbe ni mchumia tumbo Kama Msoga gang.

Alichokosea ni kumjaribu JPM huku akimutishia 'niguse ninuke' Jiwe likamugusa lione hiyo harufu! Kumbe ni vitisho tu.
Anamusifia Hangaya 😂😂😂 huku akijua hata ungewajumulisha wote Hangaya+Msoga gang hawafiki hata nusu ya aliyofanya Jiwe,hata Kama Hangaya atatawala mpaka 2050.
 
Jiwe,
Nimekuta kule ndani mambo ya ovyoovyo tu.nilimdharau

Mzee wa dk ya 90 kwa wino mwekundu akaingia mitini

Ni bora kumwamini mzee Rungwe wa Chauma anayesema linalowezekana watoto wale ubwabwa
 
Membe alicholenga ni kujionyesha ni mtu mwema na mwenye nia njema na nchi,kumbe ni mchumia tumbo Kama Msoga gang.

Alichokosea ni kumjaribu JPM huku akimutishia 'niguse ninuke' Jiwe likamugusa lione hiyo harufu! Kumbe ni vitisho tu.
Anamusifia Hangaya 😂😂😂 huku akijua hata ungewajumulisha wote Hangaya+Msoga gang hawafiki hata nusu ya aliyofanya Jiwe,hata Kama Hangaya atatawala mpaka 2050.
Mimi mpaka leo sielewi ni kwa nini Hangaya anadhani anao uwezo wa kutuongoza? Hivi wewe umeshamuona akiongelea jambo lolote ambalo ni intuition yake ukiachilia kuandikiwa?
 
Membe alicholenga ni kujionyesha ni mtu mwema na mwenye nia njema na nchi,kumbe ni mchumia tumbo Kama Msoga gang.

Alichokosea ni kumjaribu JPM huku akimutishia 'niguse ninuke' Jiwe likamugusa lione hiyo harufu! Kumbe ni vitisho tu.
Anamusifia Hangaya 😂😂😂 huku akijua hata ungewajumulisha wote Hangaya+Msoga gang hawafiki hata nusu ya aliyofanya Jiwe,hata Kama Hangaya atatawala mpaka 2050.
Utopolo. Je niguse alinuka hakunuka?? Kamuulize 7baya na Mcba
 
Back
Top Bottom