Swala la kujiunga na OIC Hawajalipatia Ufumbuzi?

Mag3,
Mkuu hakuna mahala nimekataa kwamba Vatican City sio nchi isipokuwa Mwanakjijiji ndiye anakataa kuwa Vatican pia ni taasisi bila kutaka kuelewa hata kama anaelewa tunazungumzia kitu gani. Wabishi ni nyie mnaokataa kukubali kuwepo kwa Taasisi Vatican City isipokuwa serikali hali Vatican wenyewe wameonyesha vitu viwili tofauti..Ebu soma kipande hiki kisha nijulishe umeelewa nini..

Vatican City State is a recognised national territory under international law, but it is the Holy See that conducts diplomatic relations on its behalf, in addition to the Holy See's own diplomacy, entering into international agreements in its regard. The Vatican City State thus has no diplomatic service of its own.

Kwa hiyo.. ukiingia mkataba na uhusiano wa kibalozi na Holy See umeingia mkataba na Vatican City State kwani Holy See inafanya hivyo "on its behalf" a.k.a kwa niaba yake. Safi kabisa. Angalau umeyapata majibu mumo kwa mumo.
 
Mwanakijiji,
Ndio maana hatuelewaniiii, lini wewe umesikia watu wakisema Washington DC wamesema hivi ama vile wakimaanisha serikali ya USA?.. mimi najua husema Capital hill na hii ikimaanisha metonym for the United States Congress. Ndicho tunachoongea hapa, hayo maswala mengine yoote unaongeza wewe mkuu wangu..Sasa tukitaka kuendeleza ubishi kwamba Capital hill ni nchi, sehemu sijui historic neighborhood,(of which is true) mkuu tutakesha...ila kwa wale wanaoelewa tuna maanisha kitu gani tunaweza kuwa ukurasa mmoja.

Hatukuwa na mkataba na Vatican City ukasainiwa na Holy see kwa niaba yao. Nisome tena natena na tena mkuu wangu - Nasema hivi, Mkataba wetu ni baina ya Tanzania na Holy see taasisi ya kidini moja kwa moja. Haihusiani kabisa na Vatican City.. Nakusoma hapo nyuma inabidi nicheke tu. Yaani unarudinyuma mbele unazunguka hali maelezo yangu yako wazi kabisa... duh ama kweli wewe CCJ..

Nilikuwepo, ngoja niangalie mpira...lakini mkuu wangu una matatizo makubwa sana ya kujaribu kuelewa watu wengine isipokuwa kwa lugha yako unayoitaka wewe.. Hii huwezi kwenda mbali kisiasa, na hakika jaribu sana kujirekebisha ktk hilo. Ni ushauri wangu tu!
 
Kwa hiyo.. ukiingia mkataba na uhusiano wa kibalozi na Holy See umeingia mkataba na Vatican City State kwani Holy See inafanya hivyo "on its behalf" a.k.a kwa niaba yake. Safi kabisa. Angalau umeyapata majibu mumo kwa mumo.
No haikufanya on behalf.. maelezo hayo hapo juu yanahusu Vatican City (nchi) na sio Vatican taasisi inavyoweza kujitegemea yenyewe.Hivyo, mkataba ya Holy see haiwekwi on behalf of Vatican City isipokuwa ipo mingi ya Vatican City inayopititishwa na Holy see on their Behalf..pamoja na kwamba hata Vatican City wanayo mikataba yao pekee.
Mathalan, unaweza kuwa na mkataba na Tanesco ku supply chai asubuhi kwa wafanyakazi wake, huu ni mkataba wa Tanesco na wewe, tofauti na huu ipo mikataba inayosainiwa na serikali kwa niaba ya Tanesco, pia ipo mikataba ya uwekezaji wa nguvu za Umeme inayosainiwa na serikali kama miundombinu ya serikali na sio kwa niaba ya Tanesco, ila kwa serikali yenyewe. Na zaidi ya hapo ipo mikataba ya CCM ambayo haihusu nchi wala shirika..Jaribu kuusoma mifano hiyo minne kunisoma nazungumzia kitu gani
 
Mkandara, je Tanzania iwe na uhusiano wa kibalozi na OIC ambayo ni jumuiya ya nchi za Kiislamu kama ilivyo na uhusiano wa kibalozi na taasisi ya kidini ya Holy See? Taasisi ambayo Tanzania haijawa mwanachama wake? Au njia pekee inayokubalika nawe ni kuwa ni lazima tujiunge kabisa kama wanachama wakati kuna option ya kuwa na uhusiano wa kibalozi?
 
Mkandara, je Tanzania iwe na uhusiano wa kibalozi na OIC ambayo ni jumuiya ya nchi za Kiislamu kama ilivyo na uhusiano wa kibalozi na taasisi ya kidini ya Holy See? Taasisi ambayo Tanzania haijawa mwanachama wake? Au njia pekee inayokubalika nawe ni kuwa ni lazima tujiunge kabisa kama wanachama wakati kuna option ya kuwa na uhusiano wa kibalozi?
Mkuu wangu haijalishi ni uhusiano wa aina gani tulokuwa na Vatican, ati ili uwe sawa na ule wa OIC kwa sababu hivi ni vyombo viwili tofauti kabisa ktk muundo wake na utawala wake..Katika Uislaam hatuna Papa wala nchi inayoongoza utawala wa dini. Hata Mecca, Saudia ni sehemu muhimu ya dini ya kiislaam lakini hakuna kiongozi mkuu wa dini ya Kiislaam duniani akiendesha dini kutoka Mecca.

Ni sawa na kulazimisha mkataba baina yetu na Vatican uwe sawa na diplomatic za nchi nyingine wakati sivyo na haiwezekani kwa sababu balozi wa Vatican (Papal nuncio) ana kazi mbili, moja ya Kitaifa (Vatican City) na nyingine ya Kiroho as head of Catholic churches ndani ya nchi hiyo.

Kwa hiyo, kama nchi inakuwa na uhusiano na Vatican City peke yake na sio Holy see, Vatican hupeleka balozi (Apolostolic delegate) asiyekuwa na kazi ya pili ingawa atafanya kazi zote za kibalozi sawa na balozi wa kawaida..Lakini mkisha weka mkataba na Holy see na ku establish full-fledge relationship - Vatican ndipo humleta Papal Nuncio ambaye ndiye anakuwa pia mwakilishi wa Papa na mkuu wa makanisa yote ya Roman Catholic nchini humo..

Kama unakumbuka zamani Marekani na Uingereza hawakuwa na Papal nuncio kwa sababu Protestant dominant hawakukubaliana na mfumo huu hadi miaka ya hivi karibuni tu..hivyo,mabalozi waliotumika walikuwa delegates tu.
Sasa tukianza ubishi hapa kuchambua kuku huyu sidhani kama tunaweza kumla na hatutafika mahala kwani Waislaam wanaweza kuuliza swali hilo hilo - Kwa nini hatukuwa na delegate tu badala ya Apolistic Nunciature?.
Lakini yote haya hayahusu kabisa mkuu wangu kujadili uhusiano wetu na Vatican kwa sababu umeshakubalika na unafanya kazi vizuri tu kwa waumini wake...

Mkuu wangu sipendi kwenda huko lakini maadam unataka tujadili tu ili mredi u prove ur point against OIC basi twende lakini ndio watu wataanza kusemna tumeingia ktk Udini. Nadhani kwa mwenye kuelewa haraka atanisoma..swala ni OIC na haki ya Wazanzibar. Je Zanzibar kama nchi wanayo haki ya madai yao au hawana?..

Sasa basi tunapobishana juu ya OIC ni bora tuzingatie wahusika wenyewe kama ndivyo wanavyotaka. Lakini tunapoanza kuchambua undani wa dini nyingine ndipo tunapoharibu na kuingia Udini. Kwa mfano mimi sikubaliani na Ukatoliki (Vatican) kutuletea dini kisha watukabidhi viongozi wao wa dini kuendesha imani ya dini nchini mwangu...
Wamlete balozi anayehusika na mambo ya nchi inatosha kabisa hayo maswala ya dini waachie wananchi watajichagulia wenyewe viongozi wao hapa hapa nchini kwa sababu Biblia ipo na inaeleza mambo yote yanayotakiwa kwa muumini kuelewa... Au watulete walimu na sio viongozi wa dini watoke nchi za nje kuendesha dini hapa nchini.

Mtazamo kama huu ni wangu, lakini utaonekana ujinga mtupu kama nitamwambia Mkatoliki hivyo kwa sababu yeye ndiye anayeamini utaratibu huo wa Holy see na ndio maana yeye ni Mkatoliki na mimi Muislaam aau Kichuguu wangu (utani) Pretestant pia..(UK na USA walikuwa wakifikiria hivyo zamani)

Kwa hiyo, siwezi kumwambia hoja yangu hii na ikamwingia akilini. Na ndivyo wewe unajaribu sana kuelewa OIC na Uislaam huku ukitumia imani yako ktk utaratibu wa Kikatoliki...

Kwa hiyo Haiwezekani kuhusiana na OIC kama balozi tu ni lazima Ujiunge na nchi nyingine kama ilivyo ktk Vatican ni lazima ukubali mkataba na Holy see kuletewa Nuncio badala ya balozi tu wa kawaida (Apostolic Delegate) I can pull up the same argument, why not just have a normal diplomatic relationship rather than give precedence to the Papal Nuncio over all other diplomatic representatives.
 
Mkuu mkandara,jamaa hawezi kukubali kukuelewa hata kama umemuelewesha kiasi cha yeye kukuelewa,maelezo yako yapo safi kabisa na yanaeleweka kwa uzuri,lkn naona kama unatwanga kinu ktk maji... hebu angalia nasikia hivi sasa kakobe yupo nchi ya jirani,huko anaponesha viwete,na kina M/kijiji wanaamini kabisa,wakati hapa tz viwete kibao wapo.. unafkiri atakuelewa kwa hali hii?
 
Mkuu mkandara,jamaa hawezi kukubali kukuelewa hata kama umemuelewesha kiasi cha yeye kukuelewa,maelezo yako yapo safi kabisa na yanaeleweka kwa uzuri,lkn naona kama unatwanga kinu ktk maji... hebu angalia nasikia hivi sasa kakobe yupo nchi ya jirani,huko anaponesha viwete,na kina M/kijiji wanaamini kabisa,wakati hapa tz viwete kibao wapo.. unafkiri atakuelewa kwa hali hii?

Bingwa wa Rivasi? au key board haina mfupa (ulimi hauna mfupa)

Hebu na tujikumbushe nyingine maana week end hii.

....Buguruni na Gongombali Mboto wapi?
..... Yule aliyevaa Kocha ndie Traksuti wenu?
...... Vile nakata mbwa tu.. kona huyu!
........ Vile navua uhar... tu! suruali hii!

Kingwele
 
Back
Top Bottom