Swala la kujiunga na OIC Hawajalipatia Ufumbuzi?

Mzee Mwanakijiji,
Acha kujikanyaga kanyaga mkuu wangu., Kuna nchi ambayo haikuwepo kabla?... Hata Tanganyika ilikuwepo kabla hatujapata Uhuru na Hata Ukerewe ipo zamani tukija pata uhuru wetu ndipo tunaanza kuhesabu Ukerewe kama nchi..Sikuelewi unazungumzia kitu gani kwani ubishi wote wa madai ya Vatican kuwa nchi yanaanzia siku ilipotambulika na kukubalika kama nchi..na ndicho tunachochambua hapa.

Pengine mpe mtu mwingine ayasome maandishi yangu hapo juu na akutafsirie upate kuelewa tofauti niloizungumzia ya kwamba Vatican sio nchi. Nchi ni Vatican City na links zao nimekuwekea, zisome na upate kuelewa nachozungumza. Hakuna mahala nimekubali ulosema wewe, na hakuna mahala nimeandika ya kwamba vitu hivi havihusiani! isipokuwa swala ni nani tumeingia naye mkataba..Kisha hakuna Mtanzania anayetumia neno Holy see katika mazungumzo ya ku address Vatican.

Vatican represent Holy see na hata huyo Rugambwa anawakilisha Holy see kama balozi wa Papa..Maadam unakubali kuna tofauti baina ya nchi na Taasisi, pamoja na kwamba ni zinaunda utawala mzima bado ni tofauti na ktk utofauti huo ndipo tunapogoingana nikisema ni uwakilishi wa Taasisi ndiyo tumeingia nayo mkataba...Sasa huu ubishi unakwenda wapi?..

Mkuu wangu, kama kuna mkataba baina ya CCM na mtu yeyote kitaifa mathlan jengo la Vijana. Mtu yeyote anaweza kusema ni serikali ya Tanzania imeingia mkataba wa huyo mdosi..Tunaweza tumia jina la utawala wa CCM kuzungumza mkataba wa nchi kutokana na wao watawala lakini ipo tofauti kubwa sana..

Nimekupata vizuri kabisa, kwa vile tumeshakubaliana kuwa Vatican City ni nchi halali na inayotambulika kimataifa na kuwa Mkuu wake ni Papa na kuwa Holy See ni hakimiya ya utawala wa Papa tunaweza kuelewa basi ni kwanini Tanzania ina uhusiano wa kibalozi na Vatican (papa) kwa sababu yeye ni absolute monarch wa nchi ya Vatican City. Na kwa vile tumekubaliana kuwa OIC siyo nchi moja bali ni jumuiya ya nchi mbalimbali basi ni wazi kuwa uhusiano nayo unawezekana kama vile tulivyo na uhusiano na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa au taasisi zake mbalimbali.

Nashukuru kwamba hatimaye tumeumaliza mjadala wa Vaticani ni nchi au si nchi na kama kuna uraia au hakuna. Mchango wako kwa kweli umesaidia sana kuwaelewesha wengine ambao wamekuwa wakiuliza kwanini Tanzania ina balozi Vatican na kwanini kuna mwakilishi wa Holy See Tanzania. Natumaini maswali haya hayatakuwa yanarudiwa rudiwa tena.

Sasa tumebakiwa na swali la kuuliza ni uhusiano gani uwepo kati ya Tanzania na OIC? Uhusiano ambao utaheshimu Katiba ya OIC na katiba yetu na kuhakikisha kuwa una manufaa kwa pande zote mbili?

Binafsi napendekeza Rais Kikwete amteue Balozi wetu awe mwakilishi wa Tanzania kwenye OIC - hilo pendekezo la kwanza.

Napendekeza vile vile kama hilo la Ubalozi (ambalo naamini ni bora zaidi) tujiunge na OIC kwa masharti ya kutosimamia baadhi ya malengo ambayo yanahusiana na dini ya Kiislamu ya OIC ili kuhakikisha kuwa tunakuwa neutral. Kwa vile hoja kubwa inayotolewa ya kwanini tujiunga ni kuwa kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi basi OIC na Tanzania zikae chini na kuandika makubaliano ya kujiunga ambayo yatatufanya tujiunge kwa misingi ya uchumi tu na si kingine. Unasemaje?
 
Mzee Mwanakijiji,
Acha kujikanyaga kanyaga mkuu wangu., Kuna nchi ambayo haikuwepo kabla?... Hata Tanganyika ilikuwepo kabla hatujapata Uhuru na Hata Ukerewe ipo zamani tukija pata uhuru wetu ndipo tunaanza kuhesabu Ukerewe kama nchi..Sikuelewi unazungumzia kitu gani kwani ubishi wote wa madai ya Vatican kuwa nchi yanaanzia siku ilipotambulika na kukubalika kama nchi..na ndicho tunachochambua hapa.

Pengine mpe mtu mwingine ayasome maandishi yangu hapo juu na akutafsirie upate kuelewa tofauti niloizungumzia ya kwamba Vatican sio nchi. Nchi ni Vatican City na links zao nimekuwekea, zisome na upate kuelewa nachozungumza. Hakuna mahala nimekubali ulosema wewe, na hakuna mahala nimeandika ya kwamba vitu hivi havihusiani! isipokuwa swala ni nani tumeingia naye mkataba..Kisha hakuna Mtanzania anayetumia neno Holy see katika mazungumzo ya ku address Vatican.

Vatican represent Holy see na hata huyo Rugambwa anawakilisha Holy see kama balozi wa Papa..Maadam unakubali kuna tofauti baina ya nchi na Taasisi, pamoja na kwamba ni zinaunda utawala mzima bado ni tofauti na ktk utofauti huo ndipo tunapogoingana nikisema ni uwakilishi wa Taasisi ndiyo tumeingia nayo mkataba...Sasa huu ubishi unakwenda wapi?..

Mkuu wangu, kama kuna mkataba baina ya CCM na mtu yeyote kitaifa mathlan jengo la Vijana. Mtu yeyote anaweza kusema ni serikali ya Tanzania imeingia mkataba wa huyo mdosi..Tunaweza tumia jina la utawala wa CCM kuzungumza mkataba wa nchi kutokana na wao watawala lakini ipo tofauti kubwa sana..
Hapo kwenye highlights ndo penyewe mkuu Mkandara....Nadhani ni wazi papacy iko above all,na kwasababu wameshasema ni full monarchy,then sishangazwi....Papa kwa mujibu wa maelezo yaliyoletwa hapa,ni above all,yani vatican state pamoja holy see...Vyote ni ufalme wake,kwenye uwakilishi ni muundo tu unatofautisha na mornachies nyingine say Saudi etc,lakini ni kama the same tu...Ni ufalme wa papa....Wether holy see ama vatican state yote ni chini ya papa na nadhani anaweza kuamua atumie kipi kati ya hivyo....Kama niko wrong naomba tuelimshane.
 
JMushi1,
Siwezi kuzungumzia mfumo wa Vatican na kuufananisha na mfumo mwingine wowote ule. Haya ni makosa ya wazi kabisa kwani Vatican City kama nchi ni kipande cha ardhi kilichopewa uhuru wake mwaka 1929, hali Holy see ilikuwepo hata kabla ya kutambuliwa kwa nchi hiyo at the land ambayo ilikuwa chini ya utawala wa Kiroma..

Ndio maana nikamuuliza Mwanakijiji ya kuwa kama Vatican ni nchi (the said Vatican City) ilikuwaje Papa mtawala akamtuma balozi wake wa mambo ya nje kwenda kuweka mkataba na Musolini ili kuunda nchi ya Vatican City?..Kabla ya hapo alikuwa akitawala kitu gani maanake hakuwa na nchi iweje awe na balozi hali hana nchi? Navyofahamu mimi Vatican sii ardhi, bali ni taasisi ambayo ilijulikana kwa jina hilo hata kabla ya Vatican City kuwa nchi huru mwaka 1929.

Hivyo maana yangu Papa alikuwepo na mtawala wa Taasisi ya Holy see ambayo ndio Vatican, na ulikuwepo na ukifanya kazi zake zooote kabla hata ya makubaliano yale kuunda nchi iitwayo Vatican City..Vatican existed even before the signing of Lateran Packs which founded Vatican City as an Independent State...

Kwa hiyo mkuu wangu huwezi kufananisha Utawala huu na ule wa Saudia au Malkia na ndivyo nilivyosema toka mwanzo nilipokuwa nikizungumza na Mwanaflsafa1. Utawala huu ni wa kidini (kiroho) sio wa kuhodhi ardhi kama wafalme na hakika Pope akisikia unamwita Mfalme anaweza kulia machozi kwa sababu Ufalme anao Mungu tu (oooh sijui na Yesu vile!).

Kwa hiyo mtu kama Rugambwa leo hii ni balozi na pengine raia wa vatican sasa sielewi kama kajivua uraia wa Tanzania..(natania), ila nachofahamu mimi Rugambwa ana serve Pope kupitia Holy see ambayo ni DISTINCT from Vatican City State.
The fact of the matter is - Holy See and Vatican City State are distinct entities. Na kila moja yao imesaini mikataba ya Kimataifa kulingana na kazi zake..Sisi Tanzania tumeweka mkataba wa mamlaka ya Kikanisa..

Mathlan Tanesco wanaweza kuweka mkataba na shirika la nje kuzalisha Umeme nchini. Hata kama imepitiwa na kupitishwa na Rais au makamu wake au Waziri mkuu...maadam mkataba huo ni wa kuzalisha umemem kwa ajili ya tanesco hatuwezi kusema Tanesco ni nchi kwa sababu tu imepitishwa na utawala wa JK..Tanesco itabakia kuwa Tanesco na Tanzania ni Tanzania pamoja na kwamba tanesco na tanzania zote zipo chini ya JK kama mtawala... kufanana kwa majina Vatican na Vatican City State hakuwezi kubadilisha maana ya Vatican kama sii taasisi ya kanisa Katoliki..

wakuu zangu niemchoka, nimejaribu saaana kuelezea lakini naona hatufiki mahala popote hivyo endeleeni na yale mnayoyaamini nyie na ukweli tuuache ulipo simama..
 
Naona mjadala umepanuka sana kuliko nilivyokuwa nimeuliza awali kwenye kufungua mada. Swali langu lilikuwa ni dogo sana, yaani kutopatikana kwa ufumbuzi wa swala la Zanzibar kujiunga na na OIC na hivyo kuichelewesha au kuizuia Zanzibar kujiunga na OIC kumesababisha hasara zipi kwa Zanzibar, na thamani ya hasara hiyo ni kiasi gani ili tujue wanaidai serikali ya Muungano Shilingi ngapi kutokana na kuwazuia kujiunga na OIC. Swali hilo lilikuwa na maana pana zaidi ikiwa ni pamoja na kujua faida gani ambazo tutazipata kama nchi tukijiunga na OIC.


Mambo mengine mengi yaliyoongelewa hapa hayakuwa yanajibu swali hilo.

(1) Tukumbushane kuwa uanachama wa taasisi yoyote una responsibilities kama vile kukubaliana na kanuni na malengo (sera) ya taasisi ile, kulipa ada ya uanachama katika taasisi hiyo, kuchagua uongozi wa taasisi hiyo, na vile vile kushiriki katika uongozi wa tasisis hiyo.

(2) Kumekuwa na maswali yaliyojitokeza kuhusu uhusiano wa Tanzania na Vatican, jambo ambalo sioni uhusiano wake na mada hii. Nchi yoyote inaporuhu uhusiano wa kibalozi na nchi au taasisi nyingine yoyote hakuna maana kuwa nchi hiyo ina wajibu wowote wa kukubaliana na sera za nchi au taasisi yenye ubalozi nayo; hiyo ni tofauti na uanachama wa taasisi. Kwa mfano, Tanzania tumewahi kuwa na mabalozi wa Iran na Iraki kwa wakati mmoja ambapo nchi hizo mbili zilikuwa zinapigana vita baina yao. Kuna nchi nyingi za kiislamu pia zina uhusiano wa kibalozi na Vatican na wala hiyo haizifanyi nchi hizo ziwe za kikatoliki; kwa mfano, balozi wa vatican huko Kuwait ni Bishop Paul-Munjed al-Hashem, Balozi wa vatican huko Pakistan ni Archbishop Adolfo Tito Yllana.

(3) Maswali mengine yanayoletwa kuhusu mapumziko rasmi ya shughuli za serikali kuwa Jumamosi na Jumapili ni mambo ambayo pia haya uhusiano wowote na mada hii. Miaka ya nyuma sana wakati wa Nyerere mapumziko yalikuwa ni Jumapili na nusu ya Jumamosi, Rais Mwinyi akaongeza na kufanya Jumamosi na Jumapili, kama tuna uwezo wa kupumzika zaidi tunaweza kuamua tuwe tunapumuzika siku tatu Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, na tunaweza tukaamua tusiwe na mapumzizo kabisa ya kiserikali,yaani siku zote ziwe ni siku za kazi, sioni kama jambo hilo lina uhusiao wa wowote na uanchama wa OIC. Ninavyoelewa, mapumziko ya Jumamosi na Jumapili na mambo tuliyorithi kutoka kwa wakoloni, ingawa Nyerere aliongeza Jumamosi nayo iwe siku ya kazi. Historia hiyo ndiyo inayofanya hata baadhi ya nchi za kiislamu kuendela kuruhusu mapumziko siku ya Jumapili. Kwa mfano huko Pakistani business hours ni kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni Jumatatu hadi Alhamisi na Jumamosi. Siku ya Ijumaa ni nusu siku ambapo kazi zinafungwa saa sita na nusu mchana, na Jumapili yote ni siku ya mapumziko. Malaysia wanatumia system kama yetu bila mabadiliko yoyote: mapumziko rasmi ni siku ya Jumamosi na Jumapili, ingawa wanaruhusiwa kwenda msikitini siku ya Ijumaa lakini bado ni siku ya kazi kama kawaida.


(3) Maswali yahusuyo wimbo wetu a taifa, bendera yetu, kwa nini tulipata uhuru mwaka 1961 na siyo 2010, kwa nini rais wetu wa kwanza alikuwa mkatoliki na mengineyo ya namna hiyo hayana uhusiano na swali la msingi lilioko mbele yetu. Ninafahamu kuwa kunapokuwa na faida kwa nchi kujiunga na shirika lolote, faida hizo ni kwa nchi nzima; kwa mfano, Tanzania kama mwanachama wa FIFA, tunafaidi kwa kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu mchezo wa kandanda kama taifa, ingawa watanzania wote siyo wachezaji na wapenzi wa mpira huo.

Nadhani nimeeleweka kuwa tupeleke mjadala huu upande upi ili kutafakari faida za OIC kwetu kama nchi kwa mapana, siyo kuanza kurumbana kama makundi ya dini. Bila kujali dini, tukumbuke kuwa Tanzania tumewahi kufaidika kutoka nchi za kiislamu, nchi za magharibi zinazoshabikia sana ukristo, na nchi za mbali mbali za Asia zisizoshabikia dini yoyote.
 
Kichuguu,
Mkuu wangu mimi nilikuelewa toka mwanzo isipokuwa naliona kosa la kwanza unapouliza hasara za kitu ambacho hakikufanyika. Kama Tanzania tusingejiunga na IMF tungekuwa na hasara gani? hili ni swali gumu sana kulijibu kisayansi tofauti na mfano wa FIFA ambao hakuna taasisi nyingine inayosimamia mpira duniani isipokuwa yenyewe..
Na hakika kinachozingatiwa hapa ni HAKI na FREEDOM ya Wazanzibar kama nchi tuloungana nayo kufanya maamuzi ambayo yatawanufaisha wao kama nchi na sio kuwa treat wao kama mkoa wa Tanzania na hwana sauti yoyote ila maamuzi yanatoka bara..Ukinambia Mwanza au Musoma wanataka kuweka mkataba na hata taasisi ya Kenya naweza kabisa kukuelewa lakini sio Zanzibar.. haya mawala ya waioslaam mmeyaingiza wenyewe kwa sababu zanzibar ni nchi yenye raia wengi waislaam basi issue imekuwa Waislaam...

Hayo mambo yaliyoongelewa yanahusuMKATABA baina ya nchi yetu na taasisi yoyote ya nje..Usiseme haihusiani na Vatican kwa sababu ambazo huwezi kuzitaja ikiwa mnaweza ku ID issue ya OIC na Waislaam badala ya Zanzibar..kumbuka on the issue of Vatican mnataka tuseme ni NCHI lakini ktk hili mnaliweka kama swala la Waislaam na sio Zanzibar.

Na kibaya zaidi ni kwamba ktk mikataba yote miwili iwe wa Vatican au OIC kuna masharti ambayo tunayafuata. Kinachonishangaza mimi ni kwamba mkataba wa Vatican hakuna mtu anayeuzungumzia kufahamu kuna masharti gani na unawahusu vipi wananchi wote kwa ujumla ikiwa ni pamoja na wale wasikuwa waumini wa dhehebu hilo, lakini ilipofikia OIC, kila mtu anataka kujua faida na hasara zake tena kwa Watanzania wote....gimme a break!....Mbona hatuzungumzia hasara/faida ambazo tungezipata kama tusingeweka Mkataba na Vatican!..Hizi zote ni Taasisi za kidini ambazo zinafanya kazi karibu sawa ktk kuendeleza jumuiya zao. Faida ya Vatican wanaijua Wakatoliki, ukiniuliza mimi Mkandara kusema kweli sijui na wala sina haja ya kuuliza kwani hainihusu...

Binafsi sioni tatizo kabisa kuwepo mkataba wa Taasisi yeyote hata huu wa Vatican ni mmkataba mzuri kwa faida ya Wakatoliki.. lakini kama nitaanza kufikiria faida yake kwa Waislaam nakujaribu kumueleza Muislaam tutakesha.. Kinachotakiwa ni kwa Muislaam kufahamu haki na freedom waliyo kuwanayo Wakatoliki kulingana na katiba ambayo inawapa uhuru wa kuabudu na kufanya ibada zao.. Misaada ya kuendeleza jamii ya Kikatoliki ni Ibada ya Wakatoliki.

Haya maswala ya mapumziko siku za kazi hayahusiani kabisa na Uislaam. Ila yanaweza kuwa na uhusiano mkubwa na Ukristu kwani ktk Uislaam hakuna siku unayotakiwa kupumzika isipokuwa muda wa sala.. Kwa hiyo nchi inaweza kufanya kazi siku zote wakaruhusu tu muda wa sala na wasivunje sheria yoyote ya dini. Ndio tunarudi palepale kwamba tusijaribu kufananisha mfumo wadini ya Kikristu na kiislaam kwani haifanani kabisaaa. Hivyo hata hizo nchi za Pakistan au Malaysia zinafuata utaratibu wa mapumziko kulingana na mazingira yao na sii kwa kuitazama dini ya kiislaam, kisha viongozi wao sii Wachungaji (clergymen).

Faida za OIC wanazijua Zanzibar na kwa Wazanzibar kama tunavyowaita Barricks kuchimba dhahabu pasipo wao kuulizwa..Haituhusu sisi Wabara tuwe Waislaam au Wakristu.. Nachotaka tufikirie ni Zanzibar wanaotaka kuingia OIC, faida na hasara zake hilo ni swali ambalo jibu lake halikuhusu wewe Mbara kama Waislaam wasivyohusika na mkataba wa Tanzania na Vatican..
 
Kaka Mkandara,

Kilichonifanya kuuliza hasara hizo ni kwa sababu wabunge wa Zanzibar wamemtaka Waziri kiongozi aiambie Serikali ya Muungano iilipe fidia Serikali ya Zanzibar kutokana na hasara wanayopta kwa kuchelewesha au kukataliwa kujiunga na OIC.

Siyo kweli kuwa ukiruhusu nchi au taasisi ya nje kuweka ubalozi wake nchini kwako unawajibika kukubaliana na masharti ya nchi au taasisi uliyokaribisha, sisi tumeukaribisha ubalozi wa Vatican lakini hatuna mkataba wowote wa kukubaliana na mambo wanayofanya; ndiyo maana nimetoa mifano ya nchi za kiislamu ambazo zina balozi za vatican. Hiyo ni tofauti kabisa na kuwa mwanachama wa taasisi kama AU, FIFA, OIC, UN, EAC (itakapokuja) n.k. Uanachama katika taasisis yoyote ni kuwa umekubaliana na malengo ya tasisi ile.

Bila kuangalia Vatican, ukristo na politics za jambo hilo, sisi tujiulize swali dogo tu: Ni nini faida tunazokosa kwa kuchelewa au kuzuiwa kuwa wanachama wa OIC? Tuliangalie swali hili objectively tukianisha faida na hasara bila ushabiki.
 
Mimi kusema ukweli uwa nashangaa sana ni kwa vipi hizi dini mbili zimeweza kuwafanya watu wengi ninao wajua kuwa rational kwenye masuala mengine, kuwa irrational inapokuja kwenye masuala ya dini. Na jee inakuwaje sisi Waafrika tunapinga vitu vingi tulivyoletewa na wakoloni( Wazungu na Waarabu) , lakini inapokuja kwenye dini ambazo tumeletewa na hawa hawa wakoloni tuko tayari kutoana roho na wazalendo wenzetu . Ni jambo la kusikitisha jinsi hizi dini zilivyopunguza uwezo wetu wa kufikiri.
 
JMushi1,
Siwezi kuzungumzia mfumo wa Vatican na kuufananisha na mfumo mwingine wowote ule. Haya ni makosa ya wazi kabisa kwani Vatican City kama nchi ni kipande cha ardhi kilichopewa uhuru wake mwaka 1929, hali Holy see ilikuwepo hata kabla ya kutambuliwa kwa nchi hiyo at the land ambayo ilikuwa chini ya utawala wa Kiroma..

Mzee hii ni historia ya kutunga sasa. Hakuna mahali popote penye historia unapoweza kupata hilo isipokuwa kwa kukisia tu. Nimeweka historia fupi ya Vatican City State lakini naona umeiruka. Nakushauri fanya utafiti kwenye search engine yako kuhusu kitu kinachoitwa "Papal States" ndipo utaelewa kuwa Vatican City State ilikuwepo kabla ya makubaliano ya Lateran ya 1929 ambayo hayakuipa Uhuru Vatican City bali kutambua uhuru wake ambao ulitangulia kuwepo kwa miaka 1000 kabla.

Ndio maana nikamuuliza Mwanakijiji ya kuwa kama Vatican ni nchi (the said Vatican City) ilikuwaje Papa mtawala akamtuma balozi wake wa mambo ya nje kwenda kuweka mkataba na Musolini ili kuunda nchi ya Vatican City?.

Na nikajibu kuwa alifanya hivyo kwa sababu Vatican City State ilikuwe ni sehemu ya Papal States kwa muda mrefu na ilikuwa tayari nchi chini ya Papa. Nadhani hili itabidi nilirudie tena mbele ya safari au kwa namna nyingine hadi lieleweke. Vatican City State ilikuwa ni sehemu ya States nyingine zilizokuwa chini ya Papa kwa miaka 1000 hadi vita vya kuinganisha Italia ambapo Papa alinyang'anywa baadhi ya States zake. Aliachiwa hiyo Vatican City.

.Kabla ya hapo alikuwa akitawala kitu gani maanake hakuwa na nchi iweje awe na balozi hali hana nchi? Navyofahamu mimi Vatican sii ardhi, bali ni taasisi ambayo ilijulikana kwa jina hilo hata kabla ya Vatican City kuwa nchi huru mwaka 1929.

Sitachoka kurudia, Vatican City State ilikuwa ni sehemu ya States ambazo Papa alikuwa akizitawala kabla ya muungano wa Italia chini ya mfalme Victor Emmanuel. Baada ya vita vya kuunganisha Italia Papa alinyang'anywa States zake nyingine. Makubaliano ya Laterani ya 1929 yalimhakikishia Papa kuwa Vatican City inabakia kuwa chini yake kama ilivykuwa miaka 1000 kabla. Nimeambatanisha ramani ya Italia ya 1796 (miaka 20 baada ya Uhuru wa USA) kuonesha ukubwa wa Nchi za Papa.



[QUOTE]Hivyo maana yangu Papa alikuwepo na mtawala wa Taasisi ya Holy see ambayo ndio Vatican, na ulikuwepo na ukifanya kazi zake zooote kabla hata ya makubaliano yale kuunda nchi iitwayo Vatican City..Vatican existed even before the signing of Lateran Packs which founded Vatican City as an Independent State...[/QUOTE]

Once again hiyo yote ni historia ya kubunia kwani siyo historia iliyopo kiukweli. Labda inabidi utafute neno jingine maana "taasisi" halikutendei haki.

Kwa hiyo mkuu wangu huwezi kufananisha Utawala huu na ule wa Saudia au Malkia na ndivyo nilivyosema toka mwanzo nilipokuwa nikizungumza na Mwanaflsafa1. Utawala huu ni wa kidini (kiroho) sio wa kuhodhi ardhi kama wafalme na hakika Pope akisikia unamwita Mfalme anaweza kulia machozi kwa sababu Ufalme anao Mungu tu (oooh sijui na Yesu vile!).

Yawezekana na Yesu vile vile kwani alisema "Ufalme wangu si wa dunia hii". Papa hawezi kulia kumwita mfalme wakati hata tovuti ya VAtican City inamtambua kama absolute monarch! Kuna kufanana kwa kutosha kati ya Iran na Vatican labda siyo sana na Saudia.

Kwa hiyo mtu kama Rugambwa leo hii ni balozi na pengine raia wa vatican sasa sielewi kama kajivua uraia wa Tanzania..(natania), ila nachofahamu mimi Rugambwa ana serve Pope kupitia Holy see ambayo ni DISTINCT from Vatican City State.

Ambao mkuu wao ni mmoja yaani Papa.

The fact of the matter is - Holy See and Vatican City State are distinct entities. Na kila moja yao imesaini mikataba ya Kimataifa kulingana na kazi zake..Sisi Tanzania tumeweka mkataba wa mamlaka ya Kikanisa..

Ni distinct lakini vinahusiana. Labda wao wenyewe waeleze wanasema hivi kuhusu uhusiano wa Vatican City State na Holy See (kumbuka mkuu wa vyote viwili ni Papa).

Vatican City State was founded following the signing of the Lateran Pacts between the Holy See and Italy on February 11th 1929. These were ratified on June 7th 1929. Its nature as a sovereign State distinct from the Holy See is universally recognized under international law.
The Catholic Church carries out its mission of announcing the truth of the Gospel for the salvation of all humanity and in the service of peace and justice in favour of all peoples, both through the various specific and local Churches spread throughout the world, as well as through its central government. This is made up of the Pope and the Departments that assist him in carrying out his responsibilities towards the universal Church (identified as the Apostolic See or Holy See). The Pope lives in Vatican City where several of the aforementioned Departments are to be found. Vatican City State has the singular characteristic of being an instrument of the independence of the Holy See, and of the Catholic Church, from any earthly power. In a way, it is a sign of the Church's supernatural character insofar as the structures of Vatican City are reduced to the minimum necessary to guarantee its functions.

kufanana kwa majina Vatican na Vatican City State hakuwezi kubadilisha maana ya Vatican kama sii taasisi ya kanisa Katoliki..

Halafu ulisema hivi hapo nyuma:
Mzee Mwanakijiji,
Shukran kwa maelezo yako nadhani majibu yako yangemlenga Mwanafalsafa1 ambaye ameendelea kudai Vatican ni NCHI wakati nchi ni Vatican City..Hili jina limetokana na kitu gani sii sababu kwani hata wewe Mwanakijiji jina lako limetokana na kitu fulani. Nitaendelea kusisitiza kwamba Vatican sio nchi ni Taasisi ya Kikatoliki - Period.

Vatican sasa sijui ni nchi ya Kikatoliki au ni Taasisi ya Kikatoliki.



wakuu zangu niemchoka, nimejaribu saaana kuelezea lakini naona hatufiki mahala popote hivyo endeleeni na yale mnayoyaamini nyie na ukweli tuuache ulipo simama..

Hata mimi mzee mwenzangu nimechoka maana najikuta narudia majibu yale yale kwa maswali yale yale, majibu ambayo yanaweza kupatikana kirahisi tu.
 
Mimi kusema ukweli uwa nashangaa sana ni kwa vipi hizi dini mbili zimeweza kuwafanya watu wengi ninao wajua kuwa rational kwenye masuala mengine, kuwa irrational inapokuja kwenye masuala ya dini. Na jee inakuwaje sisi Waafrika tunapinga vitu vingi tulivyoletewa na wakoloni( Wazungu na Waarabu) , lakini inapokuja kwenye dini ambazo tumeletewa na hawa hawa wakoloni tuko tayari kutoana roho na wazalendo wenzetu . Ni jambo la kusikitisha jinsi hizi dini zilivyopunguza uwezo wetu wa kufikiri.

Hivi umeona tunajadiliana masuala ya dini au historia? Mimi hadi sasa sijagusa suala la dini isipokuwa suala la historia ambalo mtu yeyote hata asiye mwenye kuamini vifuu anaweza kuliangalia na kulijadili. Au mwenzetu historia inayohusu taasisi na vyombo vya dini nayo ni dini? Kwani vilivyoletwa na wakoloni vyote ni vibaya? I know for one sina ninavyopinga vingi vya wakoloni. Sijaona sababu ya kuvipinga bado.
 
Mzee Mwanakijiji,
Nimekuelewa sana toka mwanzo isipokuwa wewe ndio unakwepa swali la msingi. Papal states hazikuwepo baada ya nchi kuchukuliwa na Waroma mwaka 1870 kwa hiyo hakuwa akitawala nchi toka mwaka huo. Na ilipofika mwaka 1929 yakawepo makubaliano ya kuunda nchi ya Vatican City ambayo hata kwa ramani uloonyesha (njano) ni tofauti na Vatican City state halafu unapozungumza papastates zilikuwa huru una maana gani? kwa sababu hazikuwa huru ila ni sehemu walizochukua kwa vita na kunyang'anywa. Kisha kama umesoma sikutaka kabisa kuongelea maswala ya Papal states ambazo hasa ilikuwa ni kuchukua nchi kwa vita...Google - The Roman Question labda utanielewa vizuri..

Mfano mwingine nikikuuliza wewe kuna nchi inaitwa Palestine? sidhani kama utakubali pamoja na kwamba ilikuwepo lakini siku ikitokea kuundwa kwa Palestine state iwe Gaza au West bank nchi hiyo itatambuliwa kama huru na kwa mipaka iliyopo. Kinyume cha hapo hakuna nchi huru inayotambuliwa kama Gaza au Palestine pamoja na kwamba Hamas wanaendelea na shughuli zao za kiutawala ktkt eneo wanalo miliki.

Kisha swala la mahusiano ya Vatican City na Holy see unasema tuwaulize wao kwa sababu mkuu wake ni Papa. Mwanakijiji, mimi hapa ninazo kampuni zangu mbili na zote ni registered lakini kila moja yao ni incorporated as a legal entity.. huwezi kunambia vitu hivi ni kitu kimoja kwa sababu ati navimiliki mimi.. Point yangu kubwa ni kwamba Vatican ni taasisi na hiyo Vatican City haikuwa nchi hadi makubaliano ya mwaka 1929, nyuma ya hapo hizo Papal states hazikuitwa Vatican wala mjomba wake. Na Utawala wa Papa bado aliendelea na shughuli za kidini kama kawaida kabla na baada ya....

Vatican ni taasisi ya Kikatoliki, ni institution ambayo hakuna mtu anayetumia neno Holy see kuizungumzia isipokuwa Vatican..na unaposema Vatican City watu wanajua unazungumzia nchi ambayo raia wake wana passport zao tofauti na zile za wachungaji wa Holy see. Na hakika hata pasipo makubaliano ya mwaka 1929 kuunda nchi ya Vatican City, bado Papa nangeweza kuendelea na kazi zake za kidini hapo Vatican kwa sababu hii ni taasisi wanaomiliki ardhi (majengo) Vatican..

Hata familia yangu huko Ukerewe tulikuwa na ardhi yetu tukiwa tumetaliwa na mkoloni na hata baada ya Uhuru haikubadilisha urithi wa mali tulokuwa nayo. Oooh ktk kunogesha mjadala.. Ukiwa New York ukimwambia Taxi driver nipeleke United Nation.. bila shaka atakupeleka kwenye jengo la UN pale Manhattan, lakini ukimwambia mtu huyo huyo nimeweka mkataba na UN sidhani kama atafikiria umeweka mkataba na lile jengo!...Aight?

Kama umechoka nadhani tuyaache haya kwa sababu itakuwa ubishi wa Pinda na viongozi wa Zanzibar ambao wanataka kujua kama Zanzibar ni nchi au nini.. majibu ya Pinda Zanzibar sio nchi wala Taifa pamoja na kwamba wanaye rais, waziri mkuu na bunge!..Sasa pengine wenzetu mnazo tafsiri za nchi ambazo sisi wengine hatuzifahamu..
 
Mzee Mwanakijiji,
Nimekuelewa sana toka mwanzo isipokuwa wewe ndio unakwepa swali la msingi. Papal states hazikuwepo baada ya nchi kuchukuliwa na Waroma mwaka 1870 kwa hiyo hakuwa akitawala nchi toka mwaka huo.

Bado hujanielewa. Papal States zimekuwepo kuanzia 752-1870!! Unaweza kupitia hapa ili kujifunza zaidi. Papal States - Wikipedia, the free encyclopedia



Na ilipofika mwaka 1929 yakawepo makubaliano ya kuunda nchi ya Vatican City ambayo hata kwa ramani uloonyesha (njano) ni tofauti na Vatican City state halafu unapozungumza papastates zilikuwa huru una maana gani? kwa sababu hazikuwa huru ila ni sehemu walizochukua kwa vita na kunyang'anywa.

Nadhani kuna vitu unachanganya. Waitaliano ndio walimnyang'anya Papa maeneo yake aliyotawala kwa muda wa karibu miaka 1000! Sijui unazungumzia Papa alimnyang'anya nani?


Kisha kama umesoma sikutaka kabisa kuongelea maswala ya Papal states ambazo hasa ilikuwa ni kuchukua nchi kwa vita...Google - The Roman Question labda utanielewa vizuri..

MBona nimeshalizungumzia hilo huko nyuma? The Roman Question utaona linahusiana na swali la hadhi ya papa na mali zake wakati wa vita vya kuiunganisha Italia.

Mfano mwingine nikikuuliza wewe kuna nchi inaitwa Palestine? sidhani kama utakubali pamoja na kwamba ilikuwepo lakini siku ikitokea kuundwa kwa Palestine state iwe Gaza au West bank nchi hiyo itatambuliwa kama huru na kwa mipaka iliyopo. Kinyume cha hapo hakuna nchi huru inayotambuliwa kama Gaza au Palestine pamoja na kwamba Hamas wanaendelea na shughuli zao za kiutawala ktkt eneo wanalo miliki.

Lakini Palestine ina mwakilishi Vatican na Papa ana balozi na PLO! go figure!

Kihsa swla la mahusiano ya vatican na Holy see unasema tuwaulize wao kwa sababu mkuu wake ni Papa. Mwanakijiji, mimi hapa ninazo kampuni zangu mbili nazote ni registered lakini kila moja yao ni incorporated aa a legal entity.. huwezi kunambia vitu hivi kitu kimoja kwa sababu navimiliki.. Point yangu kubwa ni kwamba Vatican ni taasisi na hiyo Vatican City haikuwa nchi hadi makubaliano ya mwaka 1929, nyuma ya hapo hizo Papal states hazikuitwa Vatican wala mjomba wake.

Of course! hazikuitwa Vatican kwa sababu zilikuwa ni sehemu ya milki za Papa. Vatican City State ni sehemu ya mwisho ya Papa States. Hazikupata uhuru 1929. Sijui nikusaidia vipi kuelewa hili. Majeshi ya Italia yaliamua kuchukua kwa nguvu Papal States na kumuachia Vatican City tu na yeye mwenyewe aliachilia madai yake ya States nyingine na kukubaliana na ufalme wa Italia. Hapo ndipo Vatican City Ikabakia kama nchi ilivyo chini ya Papa! Ni sawasawa na mtu aje kumnyang'anya Rais wa Marekani ukuu wa States zote na kumuachia Maryland peke yake! Sasa huwezi kusema kuwa Maryland imeundwa baada ya kuachiwa isichukuliwe wakati tayari ilikuwepo kabla yake! Vatican City State ilikuwa sehemu ya nchi za papa na ni pekee iliyosalia baada ya uvamizi wa majeshi ya Italia.

Na Utawala wa Papa bado aliendelea na shughuli za kidini kama kawaida kabla na baada ya.

Of course. Kwani sovereignty iko kwa Papa haiko kwa nchi! Hata leo hii wakiinyang'anya Vatican City State bado Papa atakuwa na uwezo wa kuwa na mabalozi na ofisi zake kwani he is sovereign.

Vatican ni taasisi ya Kikatoliki, ni institution ambayo hakuna mtu anayetumia neno Holy see kuidedfine isipokuwa Vatican.. na unaposema Vatican City watu wanajua unazungumzia nchi ambayo raia wake wana passport zao tofauti na zile za wachungaji wa Holy see. Na hakika hata pasipo makubaliano ya mwaka 1929 kuunda nchi ya Vatican City, bado Papa nangeendelea na kazi zake hapo Vatican kwa sababu hii ni taasisi wanaomiliki ardhi (majengo) Vatican..

I give up! Unazungumza kana kwamba kuna Vatican halafu kuna Vatican City!

Hata familia yangu huko Ukerewe tulikuwa na ardhi yetu tukiwa tumetaliwa na mkoloni na hata baada ya Uhuru haikubadilisha urithi wa mali tulokuwa nayo.

Irrelevant!

Kama umechoka nadhani tuyaache haya kwa sababu itakuwa ubishi wa Pinda na viongozi wa Zanzibar ambao wanataka kujua kama Zanzibar ni nchi au nini.. majibu ya Pinda Zanzibar sio nchi wala Taifa pamoja na kwamba wanaye rais, waziri mkuu na bunge!..Sasa pengine wenzetu mnazo tafsiri za nchi ambazo sisi wengine hatuzifahamu..

Well.. nilishaligusia hilo sitaki kulirudia na halihusiani hata kidogo na suala la Vatican ni nchi au si nchi.
 
NI LAZIMA RAIS AU KIONGOZI WA VATICAN AWE NI RAIA WA VATICAN,KAMA SHERIA YA NCHI NYENGINE? lol
 
Naona topic imeanza kupiga mark-time!
Inazunguka pale pale!

Labda turudi kwenye suala la msingi, ni faida zipi ambazo Tanzania inazikosa kwa kutojiunga na OIC?!
 
strictly islam....................upuuzi tu....msituletee mambo ya kuanza kujitoa mhanga...
 
Mwanakijiji, umetoa somo tosha lakini kama kawaida ya binadamu, si wote wataweza kushinda mtihani. UN inaitambua Vatican City kama nchi na Mkuu Mkandara na kundi lake hawakubali lakini UN hiyo hiyo inapokataa kuitambua Zanzibar kama nchi huyo huyo Mkandara na kundi lake wanakuja juu! Ninachoweza kusema ni kuwa kelele za Mkandara na kundi lake kamwe hazitaizuia Vatican City kuwa nchi na kuwa na balozi zake si Tanzania tu bali Iran, Marekani na nchi nyingi tu zinazotambuliwa na UN.

Lingine la ajabu ni kuwa jaribu tu kuongelea mambo ya Uislamu na Mkandara atakuwa mstari wa mbele kukupa somo kwani kulingana na yeye asiye Muislamu hajui chochote kuhusu Uislamu. Lakini gusia jambo lolote linalowahusu Wakristo na Mr. know all huyo huyo ambaye si Mkristo atakuwa mstari wa mbele kulizungumzia kama tunavyoshuhudia hivi sasa kuhusu Ukatoliki. Laiti angekuwa tayari kukubali kuwa labda wengine tunajua si kidogo kile tunachoongelea, labda ubishi ungepungua.

Wakati mwingine imani zetu tuwe tunaziweka pembeni jamani na kujibu swali lililoulizwa nalo ni mpaka sasa tumepoteza nini kwa kutojiunga na OIC. Zanzibar wanadai fidia kwa hasara iliyopata kwa kuzuiwa kujiunga na OIC, je hiyo fidia inapimwaje ? Je, kujiunga na OIC ndiyo jibu letu litakalotuondoa kwenye umasikini kwani kulingana na Raisi wetu wa sasa, hajui kwa nini Taifa la Tanzania ni masikini ! Je, Zanzibar ingejiunga na OIC kama walivyotaka miaka ilee, hivi sasa ingeifikia Kuwait au Singapore ?
 
Mzee Mwanakijiji,

Mkuu wangu mimi nakuelewa vizuri sana isipokuwa wewe ndio hutaki kuelewa..Ya kwamba Vatican ni institution achana na jina la sehemu au nchi hiyo. Kila mtu anaposema Vatican imefanya hivi ama vile ana maanisha Taasisi (uongozi) hiyo imefanya hivi ama vile na sio nchi au sehemu..Hata Kichuguu kasenma huko nyuma kwamba Vatican ni Taasisi akielewa tuna maanisha kitu gani lakini wewe unataka tu kusisitiza Vatican ni nchi ukimaanisha Vatican City ndio tunazungumzia hali sisi hatuko huko kabisa..

Pili, umeandika kwamba Papal states zilikuwepo toka mwaka 752-1870!!
Yes, sijakataa lakini after 1870 hazikuwepo au sio? isipokuwa sehemu ndogo (Vatican hills) ambayo walikuwa wakihodhi makanisa na majengo yao majengo yao..Between 1870 to 1929 kuna mengi yalitokea Kiutawala lakini muda wote Pope was confined at Vatican hills under segregationists Romans..Kitongoji hiki hakikuwa nchi wala chenye uhuru wa kiutawala kwani kilikuwa ndani ya mji wa Roma na kilikuwa kikilindwa na askari wa Kiroma kwa watu kuigia na kutoka. Na ndio maana nimekupa mfano wa Palestine ambayo ilikuwepo zamani kama nchi lakini leo hii haipo isipokiuwa kipande kidogo cha Gaza ambacho kipo chini ya Israel.

Hadi tunavyozungumza hivi sasa, Gaza sio nchi its just a city, kama Vatican ilivyokuwa kitongoji (ward) cha mji wa Rome ambacho utawala wa Pope walichukua hifadhi ktk majengo waliyokuwa wakiyahodhi. Unapochukua nchi huwanyang'anyi raia nyumba zao, wataendelea kuishi humo na kufanya mambo yao lakini chini ya utawala wa serikali iliyopo madarakani.. kama vile Soweto ilivyokuwa ndani ya Utawala wa kaburu. Soweto na hata Gaza au West Bank hizi sio nchi..kwani tunapozungumzia NCHI ktk mada hii tunazungumzia nchi huru na sii kipande cha ardhi unachokalia ndani ya utawala fulani. MNwaka 1829 nsipo Vatican ilipewa Uhuru na kuwa nchi. Kinyume cha hapo sioni sababu ya kupata Uhuru mwaka 1929 hali tayari vatican ilikuwa nchi kwa maelezo yako wewe..Why gain independence 1929, if Vatican was independent kutokana na zile Papal states?..

Tatu, yawezekana wewe unachukulia Vatican kama sehemu yaani jina hili limetokana na sehemu inayoitwa Vatican kuendeleza ubishi wa nchi au sio nchi..wakati mimi nazungumzia Taasisi tunayoiita Vatican (Holy see) unaoongoza nchi ya Vatican City!..Kama ndivyo nadhani utanisaidia sana kama utanieleza hii Taasisi inaitwa nini ikiwa sio Vatican usije nambie Holy see kwani wengi wetu hatujui hii habari ya Holy see!..

Kihsa, Je, Mtu akisema Tanzania imeweka mkataba na IMF ina maana ni nchi ya Tanzania ndiyo imeweka mkataba na IMF, lakini haihusu Utawala uliopo?..Je, kama mtu akilenga kusema utawala anatakiwa aseme serikali ya Tanzania?...Haya sisi hatukuweka mkataba na serikali ya Vatican City isipokuwa tumeweka mkataba na taasisi yake ambayo sote tunijua kama Vatican (Holy see). Ni kitu gani kigumu wewe kunielewa hapa mkuu wangu ebu nambie...

Mwanakijiji, Najua fika unanielewa sana ila unafanya makusudi kwa sababu Vatican kuna vyombo viwili.. Serikali ya Vatican ambayo inahusiana na Nchi na pili Utawala wa Kikatoliki ambao ni taasisi (holy see) Sisi tanzania tunmeweka mkataba wetu na Holy see, sasa pengine wewe mjuzi wa kuelezea nwajulishe wengine Tanzania imeweka mkataba na nani? maanake hakuna mtu anayetumia neno Holy see!


Na mwisho, Umesema Sovereignty iko kwa papa nasio nchi au sio? exactly ndipo hoja yangu inapolenga. Mkataba wetu umewekwa kwa makubaliano ya Utawal wa Papa ambaye ndiye mwenye sovereignty...sisi hatuna Mkataba na Vatican City - NCHI, isipokuwa tuna mkataba na hiyo taasisi ya Holy see.

Anyway tuachane na mada hii maanake naona imeshawachosha watu. Ukitaka kujua historia ya Papal states, soma historia ya The Holy Romans Empire. Sioni sababu ya kuendelea kubishana vitu ambavyo ni je ya Mada hii - nachojua mimi, OIC ni taasisi na Holy see ambayo sisi tunaiita Vatican ni taasisi. Hata Mkristu anaweza kusema OIC ni nchi ya Saudia (hili ni jina la kuzugia) ikawa ubishi usiokuwa na mwisho..
 
Mag3,
Mkuu hakuna mahala nimekataa kwamba Vatican City sio nchi isipokuwa Mwanakjijiji ndiye anakataa kuwa Vatican pia ni taasisi bila kutaka kuelewa hata kama anaelewa tunazungumzia kitu gani. Wabishi ni nyie mnaokataa kukubali kuwepo kwa Taasisi Vatican City isipokuwa serikali hali Vatican wenyewe wameonyesha vitu viwili tofauti..Ebu soma kipande hiki kisha nijulishe umeelewa nini..

Vatican City State is a recognised national territory under international law, but it is the Holy See that conducts diplomatic relations on its behalf, in addition to the Holy See's own diplomacy, entering into international agreements in its regard. The Vatican City State thus has no diplomatic service of its own.
 
Mzee Mwanakijiji,

Mkuu wangu mimi nakuelewa vizuri sana isipokuwa wewe ndio hutaki kuelewa..Ya kwamba Vatican ni institution achana na jina la sehemu au nchi hiyo. Kila mtu anaposema Vatican imefanya hivi ama vile ana maanisha Taasisi (uongozi) hiyo imefanya hivi ama vile na sio nchi au sehemu..Hata Kichuguu kasenma huko nyuma kwamba Vatican ni Taasisi akielewa tuna maanisha kitu gani lakini wewe unataka tu kusisitiza Vatican ni nchi ukimaanisha Vatican City ndio tunazungumzia hali sisi hatuko huko kabisa..

Unajaribu kutofautisha Tanzania na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Vatican na Vatican City State ni kitu kimoja si vitu viwili tofauti. Mara nyingi hatuzungumzi kwa kutaja "vatican city state" wakati wote. Lakini uko sawa tunapozungumzia "Vatican" vile vile tunazungumzia makao makuu ya Upapa kama vile unaposikia watu wanasema "Washington DC imesema" wakimaanisha makao makuu ya Serikali ya USA au wanposema "Nairobi imekataa ombi hilo" wakimaanisha serikali ya Kenya imekataa. Wanaposema "Vatican" tunamaanisha serikali ya Vatican City na Utawala wa Papa.



Pili, umeandika kwamba Papal states zilikuwepo toka mwaka 752-1870!!

Sikuandika tu mimi bali vilikuwepo kwa mujibu wa historia, miye nimevionesha tu kukumbushia. KUlikuwa na nchi za kipapa kwa miaka 1000.
Yes, sijakataa lakini after 1870 hazikuwepo au sio?

Zilikuwepo na kunyang'anywa ukiondoa hiyo Vatican City State )nchi ya Jiji la Vatican. VCS ni salio la mwisho wa nchi za kipapa kufuatia muungano wa Italia.

isipokuwa sehemu ndogo (Vatican hills) ambayo walikuwa wakihodhi makanisa na majengo yao majengo yao..Between 1870 to 1929 kuna mengi yalitokea Kiutawala lakini muda wote Pope was confined at Vatican hills under segregation Romans..Kitongoji hiki hakikuwa nchi wala chenye uhuru wa kiutawala kwani kilikuwa ndani ya mji wa Roma

Roma yenyewe ilikuwa ni sehemu ya nchi ya papa ambamo ndani yake ilikuwepo Vatican City vile vile. Hadi majeshi ya Italiano yalipoamua kuvunja kuta za Roma na kuichukua Roma kwa nguvu.

na kilikuwa kikilindwa na askari wa Kiroma kwa watu kuigia na kutoka. Na ndio maana nimekupa mfano wa Palestine ambayo ilikuwepo zamani kama nchi lakini leo hii haipo isipokiuwa kipande kidogo cha Gaza ambacho kipo chini ya Israel.

Sidhani kama kumewahi kuwepo nchi ya Palestina! At least sivyo kama tunavyofahamu sisi. Limekuwepo eneo likitawaliwa na tawala mbalimbali tangu antiquity ambalo tunalifahamu kama Palestina. Lakini kama nchi huru haijawahi kuwepo kwa hiyo kuilinganisha na Vatican haifanani.

Hadi tunavyozungumza hivi sasa, Gaza sio nchi its just a city, kama Vatican ilivyokuwa kitongoji (ward) cha mji wa Rome ambacho utawala wa Pope walichukua hifadhi ktk majengo waliyokuwa wakiyahodhi. Unapochukua nchi huwanyang'anyi raia nyumba zao, wataendelea kuishi humo na kufanya mambo yao lakini chini ya utawala wa serikali iliyopo madarakani.. kama vile Soweto ilivyokuwa ndani ya Utawala wa kaburu. Soweto na hata Gaza au West Bank hizi sio nchi..kwani tunapozungumzia NCHI ktk mada hii tunazungumzia nchi huru na sii kipande cha ardhi unachokalia ndani ya utawala fulani.

Kwa vyovyote vile, tunapozungumzia Vatican City State tunazungumzia nchi huru iliyopo siyo kitongoji au eneo fulani tu hivi. Ni nchi kamili ambayo mtawala wake mkuu ni Papa.

Tatu, yawezekana wewe unachukulia Vatican kama sehemu yaani jina hili limetokana na sehemu inayoitwa Vatican kuendeleza ubishi wa nchi au sio nchi..wakati mimi nazungumzia Taasisi tunayoiita Vatican (Holy see) unaoongoza nchi ya Vatican City!..Kama ndivyo nadhani utanisaidia sana kama utanieleza hii Taasisi inaitwa nini ikiwa sio Vatican usije nambie Holy see kwani wengi wetu hatujui hii habari ya Holy see!..


Kuna mambo mawili ambayo ni lazima kwanza tuyatenganishe na tumefanya hivyo vizuri tu. Ipo nchi inaitwa Vatican City State na yapo Mamlaka ya Serikali ya Papa ambayo tunayaita Holy See. Kwa mtu anayelewa hakuna ugumu wa kuelewa Upapa na Vatican City vinahusiana vipi. Papa ni mkuu wa Holy See - yaani Mamlaka ya Serikali ya Kipapa kutawala Kanisa na vile vile ni Mkuu wa Vatican City State. Sasa, serikali ya VAtican City inafanya mambo yake kama nchi nyingine yoyote. Na wakati huo huo serikali ya Kipapa nayo inafanya kazi yake katika shughuli zake mbalimbali.

Kihsa, Je, Mtu akisema Tanzania imeweka mkataba na IMF ina maana ni nchi ya Tanzania ndiyo imeweka mkataba na IMF, lakini haihusu Utawala uliopo?..Je, kama mtu akilenga kusema utawala anatakiwa aseme serikali ya Tanzania?...Haya sisi hatukuweka mkataba na serikali ya Vatican City isipokuwa tumeweka mkataba na taasisi yake ambayo sote tunijua kama Vatican (Holy see).

Sasa kama Holy See ni taasisi ya Vatican City State ina maana Holy See inawakilisha kazi za nchi ya Vatican City State na hivyo hilo ni sahihi vile vile kusema kuwa tuna mkataba na Vatican City State yaani nchi siyo?

Ni kitu gani kigumu wewe kunielewa hapa mkuu wangu ebu nambie...

Mimi nakuelewa vizuri sana nadhani wewe ndio hutaki kunielewa kabisa. Unless uniambie umeelewa kwanini Tanzania inauhusiano wa kibalozi na Vatican (iwe Holy See au Vatican City State). Bado una tatizo la Tanzania kuwa na uhusiano wa kibalozi na nchi ya Vatican (Holy See)?


Mwanakijiji, Najua fika unanielewa sana ila unafanya makusudi kwa sababu Vatican kuna vyombo viwili.. Serikali ya Vatican ambayo inahusiana na Nchi na pili Utawala wa Kikatoliki ambao ni taasisi (holy see) Sisi tanzania tunmeweka mkataba wetu na Holy see, sasa pengine wewe mjuzi wa kuelezea nwajulishe wengine Tanzania imeweka mkataba na nani? maanake hakuna mtu anayetumia neno Holy see!

Tanzania imeweka mkataba na Holy See ambao ni utawala wa serikali ya Papa ambaye ni mkuu wa nchi ya Vatican City State. Hivyo, waambie kuwa hakuna tatizo lolote kwa Tanzania kuwa na uhusiano wa kibalozi na serikali ya nchi halali ya Kipapa.


Na mwisho, Umesema Sovereignty iko kwa papa nasio nchi au sio? exactly ndipo hoja yangu inapolenga. Mkataba wetu umewekwa kwa makubaliano ya Utawal wa Papa ambaye ndiye mwenye sovereignty...sisi hatuna Mkataba na Vatican City - NCHI, isipokuwa tuna mkataba na hiyo taasisi ya Holy see.

Ndiyo.. sasa tatizo liko wapi? Maana Holy See inaongozwa na Mkuu wa nchi yaani Papa na ina mamlaka ya serikali yake ikiwa na balozi zake n.k


Anyway tuachane na mada hii maanake naona imeshawachosha watu. Ukitaka kujua historia ya Papal states, soma historia ya The Holy Romans Empire. Sioni sababu ya kuendelea kubishana vitu ambavyo ni je ya Mada hii - nachojua mimi, OIC ni taasisi na Holy see ambayo sisi tunaiita Vatican ni taasisi. Hata Mkristu anaweza kusema OIC ni nchi ya Saudia (hili ni jina la kuzugia) ikawa ubishi usiokuwa na mwisho..

Mkristu anayeweza kuona OIC ni nchi tutamnyang'anya kadi ya Ukristu!!! OIC siyo nchi ni jumuiya ya nchi za Kiislamu. Kwa upande wa Wakristu hakuna kitu kinachofanana na hicho. Kama Tanzania ingekuwa ni 'mwanachama' wa jumuiya fulani ya nchi za Kikristu, zenye malengo ya kueneza values za kikristu au imani ya kikristu basi kungekuwa na hoja tena nyepesi sana ya kwanini Tanzania nayo ijiunge na jumuiya ya nchi za Kiislamu na kuwa memba.

Unless mkuu unaweza kutuambia kuwa Vatican/Holy See ni Jumuiya ya Nchi za Kikristu ambayo Tanzania imejiunga na kuwa memba wake. Kama hilo ndilo unalolisema basi nakubaliana na wale wote kuwa Tanzania ijitoe uanachama wake mara moja na jumuiya hii ya nchi za kikristu iitwayo Vatican City State/ Holy See. Tunakubaliana kwa hilo?
 
Back
Top Bottom