Swala la fumanizi kisheria likoje.

Mroojr

Member
Nov 15, 2010
65
8
Jamani kwa wale mnaoijua sheria vizuri swala la kufumania ama kufumaniwa likoje kisheria?Nimeuliza hivyo makusudi kwa sababu mara nyingi sana wafumaniaje huwa wanavifungu vya sheria wao wenyewe vichwani mwao.Mwingine atamuacha mke au mume,mwingine anaweza kutoa kipigo kikali kwa mke au wote kwa pamoja na mwingine anaweza hata kuua kabisa.Sasa kwakuwa haya wanayoyaamua wafumaniaji hayapo kisheria je kwa nyinyi mnaozijua sheria vizuri kesi hizi za fumanizi zinafunguliwa polisi au mahakamani moja kwa moja?
 
:decision:Kwa mwanaume akimfumania mke wake akifanya uzinzi, anaweza kumshitaki huyo mwanamume mzinzi moja kwa moja mahakamani kudai fidia kwa tendo hilo. Upande mwingine mume au mke anaweza kwenda kulalamika dhidi ya mwanandoa mwenzake kwenye baraza la usuluishi la kata katika eneo analoishi lengo kubwa likiwa ni kutafuta usuluishi wa ndoa. Ikiwa mwanandoa huyo ataendeleza tabia hiyo na jitihada za usuluhishi zikashindikana, mume au mke huyo aliyefumania anaweza kwenda mahakamani kudai talaka.:decision:
 
pls wenye uelewa na hii mambo tujuzeni na mm ninahamu sana yakujua hii k2
 
Back
Top Bottom