Toni Kamkanda aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar es salaam miaka ya nyuma. Inashangaza habari hii kutolewa sasa. Katiba ya CHADEMA mpya ya mwaka 2006 haina tena cheo cha mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam. Kwa CHADEMA Dar es salaam ni kanda maalum, mikoa ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivyo, hakuna Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam wa vijana aliyehama chama. Wenyeviti wa mikoa yote hapa Dar es salaam wapo na wanaendelea na kazi zao kwenye chama kama kawaida. Hii habari inaandikwa leo wakati huyo Bwana alishahamia SAU miezi michache iliyopita tena alihama akiwa mwanachama wa kawaida. Kisa cha kuhama kwake ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2009 wa ndani ya chama aligombea nafasi zifuatazo na kushindwa Katibu wa chama Temeke, Mwenyekiti wa Vijana Temeke, Mjumbe Mkutano mkuu Temeke na zote akashindwa. Akaenda pia kugombea uenyekiti wa vijana Ilala napo akaanguka. Nipo alipohamia SAU ambapo taarifa zinaonyesha kwamba amepewa uenyekiti wa vijana Mkoa wa Dar es salam. Ni makapi tu yametoka, ametoka kapa.
Serayamajimbo
watakaobaki ndio wana Chadema halisi. Nafikiri ndani ya Chadema hakuna uanachama wa kuzaliwa, uanachama hautegemei ulijiunga na umri gani miaka 10 au 60 wote ni wanachama, aliyejiunga mwaka 1995 na aliyejiunga leo wakati wa uchaguzi wote wana kura moja moja tu.
dah!Watatoka wote humo wasiohusu kaskazini...
lol!Toni Kamkanda aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar es salaam miaka ya nyuma. Inashangaza habari hii kutolewa sasa. Katiba ya CHADEMA mpya ya mwaka 2006 haina tena cheo cha mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam. Kwa CHADEMA Dar es salaam ni kanda maalum, mikoa ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivyo, hakuna Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam wa vijana aliyehama chama. Wenyeviti wa mikoa yote hapa Dar es salaam wapo na wanaendelea na kazi zao kwenye chama kama kawaida. Hii habari inaandikwa leo wakati huyo Bwana alishahamia SAU miezi michache iliyopita tena alihama akiwa mwanachama wa kawaida. Kisa cha kuhama kwake ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2009 wa ndani ya chama aligombea nafasi zifuatazo na kushindwa Katibu wa chama Temeke, Mwenyekiti wa Vijana Temeke, Mjumbe Mkutano mkuu Temeke na zote akashindwa. Akaenda pia kugombea uenyekiti wa vijana Ilala napo akaanguka. Nipo alipohamia SAU ambapo taarifa zinaonyesha kwamba amepewa uenyekiti wa vijana Mkoa wa Dar es salam. Ni makapi tu yametoka, ametoka kapa.
Serayamajimbo
Swahiba mwingine wa Zitto ajitoa ChademaNa Tumsifu Sanga
SWAHIBA mwingine wa Zitto Kabwe, ambaye naibu katibu mkuu wa Chadema, ametangaza kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga ma chama cha Sauti ya Umma (SAU).
Swahiba huyo, Toni Kamukanda anakuwa mtu wa tatu kujiengua kwenye chama hicho ambacho kinaonekana kuendelea kujijenga kisiasa, baada ya watendaji wawili wa ofisi ya makao makuu, David Kafulila na Danda Juju kujiengua baada ya kutimuliwa kazini.
Kamkanda anasadikiwa kuwa miongoni mwa wanachama waliokuwa wakiendesha kampeni kabambe kuhakikisha kuwa Zitto anatwaa nafasi ya uenyekiti wa Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita, kabla ya wazee kuingilia kati na kumshauri mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kumwachia mwenyekiti wake, Freeman Mbowe awe mgombea pekee.
Kamkanda, ambaye alikuwa mwenyekiti wa vijana mkoani Dar es salaam, alisema ameamua kuondoka ndani ya chama hicho kutokana na ubinafsi na ukabila uliokithiri kwa viongozi wa juu.
âBaada ya kubainika kuwa mimi Kafulila na Danda tuko katika mashambulizi ya kampeni ya kuhakikisha Zitto anakuwa mwenyekiti, ilianza mikakati ya kimya kimya kutufukuzisha uanachama lakini ilishindikana,â alisema Kamganda.
Kamganda aliongeza kuwa ndio maana kuna baadhi ya watu walifukuzwa uanachama kabla ya sisi kuchukua uamuzi wa kuondoka Chadema.
âKama unakumbuka ndugu mwandishi kabla sisi hatujaondoka Chadema, kuna watu walivuliwa uanachama, ilikuwa tuvuliwe pamoja nao lakini kuna mtu wa karibu na Mbowe alimwambia hawa vijana waache wakae na baada ya hapo ikaanza fitina mpaka tulipoamua wenyewe kwa ridhaa yetu kuondoka,â alisema Kamganda.
Kamganda alisema uendeshaji wa chama hicho haufanyiki kwa misngi ya kiuongozi kutokana na maamuzi ya utendaji kufanywa na mtu mmoja hali ambayo inaashiria kuwa chama hicho kinaendeshwa kikabila na ubinafsi.
Chadema imekuwa ikitetereka tangu kipindi cha maandalizi ya uchaguzi mkuu baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea uenyekiti na hivyo kusababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa viongozi. Lakini wazee na waasisi wa chama hicho waliingilia kati na kukinusuru chama.
Hata hivyo chaguzi za viongozi wa mikoa na jumuiya za Chadema zilikumbwa na matatizo mbalimbali yaliyoashiria kuwepo kwa makundi ambayo yalishaanza kukomaa ndani ya chama.
Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi, Kafulila, ambaye alikuwa ofisa habari wa Chadema, alitimuliwa kazini kwa madai ya kuvujisha siri za chama. Alitimuliwa sambamba na Danda, ambaye alikuwa akishughulikiwa masuala ya Bunge. Wawili hao walitimuliwa na mkuu wao kiutendaji, Dk Willibrod Slaa, ambaye anaongoza sekretarieti.
Hongera sana Kamganda ni haki yako kufanya na kuamua utakalo,
Ninachosikitika ni kuwa, huwa mnakaa humo halafu mnasema mabaya baada ya kutoka! hata kama kuna ukweli, still nyie inawaweka pabaya sana katika uaminifu, ina maana ungekuwa hakuna majungu ungeishi na hali hiyo ya ukabila na ubinafsi unayoisema?
Mwenzenu Zitto sijui anajimini nini, anawarushia makombora humohumo, ulitakiwa kusema ukiwa humo humo, uone moto wake ukoje, ukitoka utoke umeshasema ukiwa mwanachama.Huu woga wa kusema nje si mzuri sio kwa chadema tu hata kwa vyama vingine.
wakati unaona unawakomoa chadema, sisi wengine tunaangalia mustakabali wa upinzani kwa ujumla, watu wanadharau vyama hivi kwa sababu ya nyie mnaojitoatoa-UKIJITOA LAZIMA UJITANGAZE??,matokeo hawapigi kura na wanaopiga kura ni wana CCM wachache CCM wanaonekana wameshinda kwa kishindo , kumbe hamna lolote
Ukitaka kupima chadema utaona kesho Slaa au Mnyika anakimbilia kwenye media na kujibu tuhuma za Kamganda,utafikiri hawana kazi ya kufanya.
Jirekebisheni Chadema , angalieni mbele, sisi tuko nanyi.msipobadilika; sahau! it is certain you may rule this country in the next century! wakati mjukuu wa saba wa Mbowe anaongoza Chadema!!
Toni Kamkanda aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar es salaam miaka ya nyuma. Inashangaza habari hii kutolewa sasa. Katiba ya CHADEMA mpya ya mwaka 2006 haina tena cheo cha mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam. Kwa CHADEMA Dar es salaam ni kanda maalum, mikoa ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivyo, hakuna Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam wa vijana aliyehama chama. Wenyeviti wa mikoa yote hapa Dar es salaam wapo na wanaendelea na kazi zao kwenye chama kama kawaida. Hii habari inaandikwa leo wakati huyo Bwana alishahamia SAU miezi michache iliyopita tena alihama akiwa mwanachama wa kawaida. Kisa cha kuhama kwake ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2009 wa ndani ya chama aligombea nafasi zifuatazo na kushindwa Katibu wa chama Temeke, Mwenyekiti wa Vijana Temeke, Mjumbe Mkutano mkuu Temeke na zote akashindwa. Akaenda pia kugombea uenyekiti wa vijana Ilala napo akaanguka. Nipo alipohamia SAU ambapo taarifa zinaonyesha kwamba amepewa uenyekiti wa vijana Mkoa wa Dar es salam. Ni makapi tu yametoka, ametoka kapa.
Serayamajimbo
Mwenzenu Zitto sijui anajimini nini, anawarushia makombora humohumo, ulitakiwa kusema ukiwa humo humo, uone moto wake ukoje, ukitoka utoke umeshasema ukiwa mwanachama.Huu woga wa kusema nje si mzuri sio kwa chadema tu hata kwa vyama vingine.
!!
Sasa kama hakuna uanachama wa kuzaliwa iweje kuwe na wanachadema HALISI, WAKUJA na MAPANDIKIZI?
Haya matabaka ya uanachama mnayoyajenga na kuyaneemesha kwa minajili ya kuwahakikishia nafasi zenu na fikira zenu za kimikakati ndani ya chama yataendelea kuwagharimu....
omarilyas