Swahiba mwingine wa Zitto ajitoa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swahiba mwingine wa Zitto ajitoa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Dec 25, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,679
  Trophy Points: 280
  Swahiba mwingine wa Zitto ajitoa Chadema[​IMG]Na Tumsifu Sanga
  SWAHIBA mwingine wa Zitto Kabwe, ambaye naibu katibu mkuu wa Chadema, ametangaza kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga ma chama cha Sauti ya Umma (SAU).

  Swahiba huyo, Toni Kamukanda anakuwa mtu wa tatu kujiengua kwenye chama hicho ambacho kinaonekana kuendelea kujijenga kisiasa, baada ya watendaji wawili wa ofisi ya makao makuu, David Kafulila na Danda Juju kujiengua baada ya kutimuliwa kazini.

  Kamkanda anasadikiwa kuwa miongoni mwa wanachama waliokuwa wakiendesha kampeni kabambe kuhakikisha kuwa Zitto anatwaa nafasi ya uenyekiti wa Chadema katika uchaguzi mkuu uliopita, kabla ya wazee kuingilia kati na kumshauri mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kumwachia mwenyekiti wake, Freeman Mbowe awe mgombea pekee.

  Kamkanda, ambaye alikuwa mwenyekiti wa vijana mkoani Dar es salaam, alisema ameamua kuondoka ndani ya chama hicho kutokana na ubinafsi na ukabila uliokithiri kwa viongozi wa juu.

  “Baada ya kubainika kuwa mimi Kafulila na Danda tuko katika mashambulizi ya kampeni ya kuhakikisha Zitto anakuwa mwenyekiti, ilianza mikakati ya kimya kimya kutufukuzisha uanachama lakini ilishindikana,” alisema Kamganda.

  Kamganda aliongeza kuwa ndio maana kuna baadhi ya watu walifukuzwa uanachama kabla ya sisi kuchukua uamuzi wa kuondoka Chadema.

  “Kama unakumbuka ndugu mwandishi kabla sisi hatujaondoka Chadema, kuna watu walivuliwa uanachama, ilikuwa tuvuliwe pamoja nao lakini kuna mtu wa karibu na Mbowe alimwambia hawa vijana waache wakae na baada ya hapo ikaanza fitina mpaka tulipoamua wenyewe kwa ridhaa yetu kuondoka,” alisema Kamganda.

  Kamganda alisema uendeshaji wa chama hicho haufanyiki kwa misngi ya kiuongozi kutokana na maamuzi ya utendaji kufanywa na mtu mmoja hali ambayo inaashiria kuwa chama hicho kinaendeshwa kikabila na ubinafsi.

  Chadema imekuwa ikitetereka tangu kipindi cha maandalizi ya uchaguzi mkuu baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea uenyekiti na hivyo kusababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa viongozi. Lakini wazee na waasisi wa chama hicho waliingilia kati na kukinusuru chama.

  Hata hivyo chaguzi za viongozi wa mikoa na jumuiya za Chadema zilikumbwa na matatizo mbalimbali yaliyoashiria kuwepo kwa makundi ambayo yalishaanza kukomaa ndani ya chama.

  Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi, Kafulila, ambaye alikuwa ofisa habari wa Chadema, alitimuliwa kazini kwa madai ya kuvujisha siri za chama. Alitimuliwa sambamba na Danda, ambaye alikuwa akishughulikiwa masuala ya Bunge. Wawili hao walitimuliwa na mkuu wao kiutendaji, Dk Willibrod Slaa, ambaye anaongoza sekretarieti.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Kamganda ni haki yako kufanya na kuamua utakalo,

  Ninachosikitika ni kuwa, huwa mnakaa humo halafu mnasema mabaya baada ya kutoka! hata kama kuna ukweli, still nyie inawaweka pabaya sana katika uaminifu, ina maana ungekuwa hakuna majungu ungeishi na hali hiyo ya ukabila na ubinafsi unayoisema?

  Mwenzenu Zitto sijui anajimini nini, anawarushia makombora humohumo, ulitakiwa kusema ukiwa humo humo, uone moto wake ukoje, ukitoka utoke umeshasema ukiwa mwanachama.Huu woga wa kusema nje si mzuri sio kwa chadema tu hata kwa vyama vingine.

  wakati unaona unawakomoa chadema, sisi wengine tunaangalia mustakabali wa upinzani kwa ujumla, watu wanadharau vyama hivi kwa sababu ya nyie mnaojitoatoa-UKIJITOA LAZIMA UJITANGAZE??,matokeo hawapigi kura na wanaopiga kura ni wana CCM wachache CCM wanaonekana wameshinda kwa kishindo , kumbe hamna lolote

  Ukitaka kupima chadema utaona kesho Slaa au Mnyika anakimbilia kwenye media na kujibu tuhuma za Kamganda,utafikiri hawana kazi ya kufanya.

  Jirekebisheni Chadema , angalieni mbele, sisi tuko nanyi.msipobadilika; sahau! it is certain you may rule this country in the next century! wakati mjukuu wa saba wa Mbowe anaongoza Chadema!!
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Chadema ni wavumilivu siamini kama wanatumia sana Media . Zitto mie nampa Hongera anawakaba humo humo .Huyu yeye kazua ukabial ndani ya Chadema hahaha . Akiwa na maana Uongozi ni Wachaga ama ukabila kwa maana gani ?Jamani mawazo mgando haya . Toka kaa kimya endelea na huko kwingine itakupa heshima kubwa .
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Watatoka wote humo wasiohusu kaskazini...
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kibunango wewe ni mkubwa kuliko aina hii ya mawazo mgando .Chadema ina uongozi hadi Zanzibar
   
 6. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #6
  Dec 25, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Toni Kamkanda aliwahi kuwa mwenyekiti wa vijana mkoa wa Dar es salaam miaka ya nyuma. Inashangaza habari hii kutolewa sasa. Katiba ya CHADEMA mpya ya mwaka 2006 haina tena cheo cha mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam. Kwa CHADEMA Dar es salaam ni kanda maalum, mikoa ni Kinondoni, Ilala na Temeke. Hivyo, hakuna Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es salaam wa vijana aliyehama chama. Wenyeviti wa mikoa yote hapa Dar es salaam wapo na wanaendelea na kazi zao kwenye chama kama kawaida. Hii habari inaandikwa leo wakati huyo Bwana alishahamia SAU miezi michache iliyopita tena alihama akiwa mwanachama wa kawaida. Kisa cha kuhama kwake ni kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2009 wa ndani ya chama aligombea nafasi zifuatazo na kushindwa Katibu wa chama Temeke, Mwenyekiti wa Vijana Temeke, Mjumbe Mkutano mkuu Temeke na zote akashindwa. Akaenda pia kugombea uenyekiti wa vijana Ilala napo akaanguka. Nipo alipohamia SAU ambapo taarifa zinaonyesha kwamba amepewa uenyekiti wa vijana Mkoa wa Dar es salam. Ni makapi tu yametoka, ametoka kapa.

  Serayamajimbo
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Sasa wasemaje wake . Kumbe hawa watu ni madaraka yanawasumbua ? Mwache aende then unategemea mtu kama huyu Chadema kuongelea habari yake ? Chadema wako na Sangara bwana imesaidia kuwaamsha watanzania juu ya CCM na mashangingi .
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhh.
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kinacho leta matumaini ni kwamba CHADEMA ina kila tahadhari za mapandikizi kwa hiyo yaache yaondoke tu wale wenye nia ya dhati ya kuleta nabadiliko ndo watako salia.
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Naona wewe binafsi ndio mwenye mawazo ya aina hiyo. Jaribu kusoma sababu ambazo wanazitoa hao wenye kuondoka humo. Kwa ufupi zote zinafanana na kama zinafanana basi lipo jambo. Na penye kufuka moshi kuna moto
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  comment yako imenifanya nicheke sana; lets hope that
   
 12. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  hizi lugha zinazotumika chadema mimi mmh,

  sisimizi, makapi, pandikizi lol
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Na Makamba akiwajibu kwa staili hiyo hiyo, huja juu sana!
   
 14. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2009
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Walafi wa madaraka mara nyingi wakikosa wanahaha kutafuta cheap politics. Hata wakienda CCM wasipopewa attention wanahamaia vyama vingine maadam wapate recognition na uongozi.
  Hili dudu la uchu wa madaraka na uongo wa kisiasa utaendelea kutuletea umasikini na rushwa daima. Ukiwa mzalendoo wa kweli utapigana hata ndani ya chama chako kuukemea na kuutokomeza ukabila kama upo, na si kukimbia na kuhama chama, tena kwa kashfa!
  Na huko SAU akikosa uongozi anaenda TLP? then CCM, then NCCR halafu huyo awe kiongozi mwadilifu kweli??? Matatizo ni kuyakabi si kuyakimbia. Watu wa hivyo hawatufai haijalishi wako CCM, Chadema, SAU, NCCR....
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Alitoka Amani K na chama hakikuteteleka. Hata watoke wote sisi tunakwenda mbele.
  Kalagabaho.
   
 16. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Amebakia Zitto sasa,

  Zitto rudi nyumbani ccm. Uwaziri wako wa nishati na madini (ulioahidiwa baada ya kuua issue ya Buzwagi) unakusubiria.
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Huyo nae amehusu kaskazini?
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kibunango sababu zao zinazofanana wewe wazijua kwasababu nyie[ccm] ndio mnaowapandikiza hawa mamluki kwenye vyama mnavyoviogopa kama CHADEMA; kwa bahati nzuri mapandikizi tenu yamegunduliwa na mmoja mmoja watakimbia wenyewe. Zitto nae anangojea ile cheki yake ya mwisho ya ubunge ndio achomoke, anavunga tu anaposema haondoki!! Good riddance.
   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Jamani nadhani si sahihi kumsakama Zitto hata pale ambapo hapana sababu . Uwaziri Zitto made clear kwamba hautaki na yeye ni Chadema kuwanzia ana miaka 16 . Now kesha tueleza hatoki na anajua nini watanzania na vijana wanategemea toka kwake . Tumwache tuongelee hawa wanao tumia maneno ya CCM kuichafua Chadema
   
 20. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2009
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa mara ya kwanza naomba kujiunga na wana JF na kutoa mawazo yangu kama ifuatavyo:
  Kuhusu swala la kuondoka wanachama CHADEMA nafikiri lilishaongelewa na Dr. Slaa kwamba Chadema ni system si mtu, hata akiondoka yeye au Mbowe chadema itabaki chadema, mimi nafikiri Slaa alitaka kusema hata akiondoka Zito Chadema itaendelea kuwa Chadema.
  Ingawa si suala jema kuondokewa na mwanachama yeyote akiwemo Zito, lakini ikibidi kuondoka na waondoke watakaobaki ndio wana Chadema halisi. Nafikiri ndani ya Chadema hakuna uanachama wa kuzaliwa, uanachama hautegemei ulijiunga na umri gani miaka 10 au 60 wote ni wanachama, aliyejiunga mwaka 1995 na aliyejiunga leo wakati wa uchaguzi wote wana kura moja moja tu.
   
Loading...