Rushwa izidi hapa iweje? Huyu nae ni mnafiki tu abaki huko huko na rushwa zao
Mkuu nakubaliana na wewe. Kipimo cha rushwa kuwa imezidi, ipo Kati au imepungua Ni nini! Yeye aliicha katika scale ipi. Rushwa kwani imekuwa chumvi au sukari kujaji kwa kulamba?
Alishughulika na kesi ngapi za rushwa wakati wake? Mambo ya ovyo mangapi ya ovyo yalitokea wakati wake? Leo anakuja kusema eti walifanya makosa kufuta michezo shule za msingi na sekondari. Na eti anayaona sasa hivi wakati akitafuta kugombea urais. Duh..... Twesha!
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema kwamba ikiwa rushwa itazidi ndani ya chama chake chama cha CCM, atajiondoa kutoka chama hicho. Haikuweza kufahamika mara moja kama atahamia chama gani lakini kuna tetesi kwamba huenda akahamia CHADEMA.
Inaelekea wewe mwenyeji wa Mpanda!Ish!! kumbe na sumaye nae kamanda mwe!!!! kwa jeshi lipi sasa
Rushwa izidi hapa iweje? Huyu nae ni mnafiki tu abaki huko huko na rushwa zao
mkuu nimeipenda sana hii hoja yako. ni kweli kabisa tena hili lingekuwepo kwenye katiba kuwa mtu asipate masurufu yake kama bado yupo kwenye siasa.Mkuu Tipau, asante kwa taarifa hii!. Huyu naye?!, eti kama rushwa itazidi?!. Ndani ya CCM, anataka rushwa izidi mara ngapi zaidi ya hii rushwa iliyopo?!. Sumaye anataka ikizidi kufikia kiwango gani?, hapo ilipo ndani ya CCM, rushwa imeisha zidi hadi kufurika kitambo!, sasa huyu anayeulizia kama rushwa ikizidi, anaulizia CCM ipi?!.
Sumaye aseme tuu, baada ya UKAWA kukosa mgombea mmoja wa 2015, wamemuomba yeye agombee and in principle atakuwa kakubali, sasa anatafuta pa kutokea CCM, ili aeleweke na jamii imuelewe!. Tena namshauri afanye hivyo mapema, kabla jamaa zake hawajabadili ile sheria ya viongozi wakuu wastaafu na kuongeza kipengele "kiongozi mkuu mstaafu atalipwa mafao na marupurupu stahiki" only if hatajishughulisha na siasa basada ya kustaafu!" kwani kuendelea kujishughulisha na siasa nayo ni ajira!.
Hajajifunza tuu kwa wenzake!, Mwalimu Nyerere Foundation, Benjamin Mkapa/IOTF, sasa JMK Foundation/WAMA on the making, na yeye aunde NG'0 yake!, hive ile HOPE FOUNDATION imeishia wapi?!.
Thanks.
Pasco.
Safi Sana karibu chadema
Anafaa kumpigia kampeni dr Slaa
Karibu kamanda Sumaye