Watanzania tumetawaliwa na unafiki mkubwa sana. Kwanza kitendo cha Kikwete kwenda kwenye mkutano mkuu wa chama chake na kuzungumzia Sumaye na Lowasa ni UNAFIKI NA KUFILISIKA kisiasa na hata kiuongozi. Hiyo maana yake ni kwamba hotuba iliyotayarishwa iliwekwa Yale majina, kwa faida gani kwa Watanzania? Mtu aliyekaa Ikulu kwa miaka kumi na aliyekuwa mwenyekiti wa chama miaka kumi, halafu anamalizia kwa kutoa vijembe ni kukosa uvumilivu, kutawaliwa na umbea na unafiki ktk maisha. Lakini pili, Sumaye na Lowasa sasa ni wanachama wa Chadema, wao kushika wadhifa wowote ni wajibu na haki yao kama wanachama. Suala la kwàmba mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kushika madaraka ya chama ngazi za kawaida kuonekana ni kushuka thamani ni matokeo ya fikra mgando tulizolishwa na tunazoendelea kulishwa na Ccm. Na huo ndiyo UNAFIKI wa wanaccm. Mbona Urusi Putin alishika Urais, akarudi kwenye Uwaziri Mkuu na kisha Urais tenà? Na kwa nini kukaa unamfikiria mtu aliyekwisha kuondoka kwenye chama chenu? Taifa linabaki kushuhudia unafiki kwa watu walioaminiwa na wananchi na kucheza vigodoro tu kama kwamba dunia inatusubiri. Tunavaa mamitumba kwa sababu ya unafiki wenu viongozi, na kamwe hatutakaa tufanikiwe kupata maendeleo.