Sumaye amkaanga JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye amkaanga JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 13, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  WAZIRI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye, amewalipua viongozi wa sasa wa serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete kwa hatua yao ya kuruhusu baadhi ya wanafamilia wao kuwania vyeo vya juu vya uongozi.

  Akiwasilisha mada kwenye mdahalo wa maadhimisho ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, jana jijini Dar es Salaam, Sumaye alisema hatua ya viongozi wengi kuandaa watoto na wake zao kwa ajili ya kuwa viongozi wa nchi, ni kinyume na katiba ya nchi, na dalili ya ubinafsi.

  Katika chaguzi za sasa ndani ya CCM, Rais Kikwete ni mmoja wa viongozi waandamizi ambao familia zao zimegombea na kushinda nafasi za uongozi ndani ya jumuiya za chama hicho.

  Baadhi ya watu kutoka familia ya Rais Kikwete waliojitosa katika chaguzi hizo ni pamoja na mkewe, na watoto wake wawili.

  Kauli hiyo nzito ya Sumaye ni ya pili tangu alipoanguka katika kinyang'anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC Taifa, akishindwa na Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu.

  Mwishoni mwa wiki, Sumaye alikaririwa akisema kuwa, kukithiri kwa rushwa ndani ya chama hicho, ndiyo sababu kubwa iliyomwangusha na kueleza hofu yake ya nchi kupata viongozi wabovu.

  Aliongeza kuwa ubinafsi umekuwa chanzo kikubwa cha kukithiri kwa rushwa katika sekta mbalimbali kwa kuwa viongozi wengi wa serikali, hawako tayari kupoteza madaraka yao, hivyo hutumia rasilimali za nchi na uwezo wao wa kifedha kuwahonga wapiga kura ili waendelee kukaa madarakani, hata kama wananchi hawawataki.

  "Rushwa imekithiri sehemu muhimu na mtu yeyote anayetaka kwenda Ikulu kupitia rushwa hafai. Mosi hizo fedha za kuwahonga wananchi alipata wapi? Kama amekopa anategemea Ikulu kuna hela ambazo hataweza kurudisha deni hilo?

  "Chaguzi zote zimetawaliwa na rushwa moja kwa moja jambo ambalo hayati Mwalimu Nyerere alilikemea hadi mwisho wa uhai wake, na kama hatutaliangalia tatizo hilo kwa makini, kuna athari kubwa kwa taifa," alisema.

  Sumaye alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, kama Mwalimu Nyerere angefufuka leo, kusingekuwa na kiongozi wa kumlaki, badala yake watu wengine wangekuwa wa kwanza kukimbilia porini.Mbali ya ubinafsi huo, alisema uchumi wa nchi umeshikiliwa na kundi la wachache, hivyo kuzuka kwa hali ya kutojali kundi la watu masikini ambalo ni tatizo kwa taifa, kwa sababu viongozi hao wamewekeza kwa kuwajali wenye nacho ili wanufaike kama wao.

  Naye Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. John Magotti, alitumia fursa hiyo kuzungumzia suala la kiwango cha elimu itolewayo nchini hususani katika shule za kata kuwa ni chachu ya kukwamisha ufaulu sanjari na ajira kwa wahitimu.

  "Kuna haja ya serikali kutafuta ufumbuzi katika sekta ya elimu kabla haujaleta madhara makubwa, kwa sababu elimu bora inaendana na nafasi bora ya ajira, hivyo mwito wangu elimu inayotolewa katika shule za kata isitofautiane sana na ile ya shule za watu binafsi," alisema Magotti.

   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  sumaye mnafiki leo ndio anatambua CCM wanatumia fomesheni ya BMW=Baba+mama/vimada+watoto
  kuna msemo wa waswahili kuwa Nyani haoni kundule!
   
 3. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Tooo late
   
 4. n

  nkikiki Senior Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nilikuwepo kwenye huo mdahalo. Ukifuatilia alichokuwa akiwaambia waandishi pale courtyard na alichozungumza kwenye mdahalo utaona kuwa kuwa anajuta kwa aliyoyafanya/tenda. Sasa hivi anaonekana ameokoka kwelikweli.

  TUMSIKILIZE NA TUZINGATIE ANAYOYASEMA! Mbona watu sasa wanamsikiliza Lowasa?!
   
 5. s

  step Senior Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Watu wanaposhindwa ndio huja na ajenda za ubaya wa wenzao. Kwa nini asiwaonyeshe wananchi njia mbadala kwani amekwisha jiridhisha huko aliko hakufai...
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hata siku ya mwisho itakuwa kama hivi ulipokuwa duniani ulifanya nini?

  Itakuwa umechelewa ulipokuwa kwy uwezo wa kupambana na rushwa kikweli kweli ulikuwa kimya leo hii rushwa imeanza kukutafuna umeanza kupiga kelele wewe inabidi ukae kimya kabisa uwe mtu wa mwisho kulalalmikia swala la rushwa kwani you are part of the corrupted leaders in Tanzania.
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  moja kati ya LEGACY ya utawala wako na mkapa ni kulea na kulinda wala rushwa.
   
 8. i

  iseesa JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sioni Ubaya wa aliyosema. MSEMA KWELI ni MPENZI WA MUNGU. Alikuwemo ndani yake na alikuwa mmoja wao. Kwa hivo anajua anachokisema. Katuambia Ukweli kuwa CCM hamna Kitu tena. Awe mnafiki asiwe kasema ukweli. Kilichobaki ni UMMA wa watanzania KUTAFAKARI na kuamua kuchagua kilicho MBADALA na BORA.
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hata mtoa rushwa hapendi, akisema hapendi sio kosa. Akikemea rushwa tumpe haki yake. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sizitaki Mbichi hizi-Sumaye

  Unafikiri angemshinda Merry Nagu angekuwa anapiga makelele sasa hivi? ungemkuta yupo busy tu na chama chake.
   
 11. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  CCM inanuka rushwa CCM inakumbatia watoto wa vigogo kumiliki NEC CCM inakwenda kinyume cha katiba anapiga kelele zote hizi lakini bado yumo humo humo anajifanya hakuyajua haya tangu mwanzo

  Aliyeyo CCM yupo kwenye mfumo huo ila sema tu walimzidi ujanja

  tukumbuke kauli hii " HAKUNA MSAFI NDANI YA CCM "
   
 12. lakiwosha

  lakiwosha Senior Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 9, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  jmaaa avoongea kana kwamba hajawahi kuchukua au kasababisha rushwa alipokua waziri mkuu,anyway mtafaruku wo ndo faida kwetu couse itafika mahali wataanza kutajana wenyewe ngoja tusubiri tuone  " TIME WILL TELL"
   
 13. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ANGEYATAMKA HAYO YOTE KABLA YA UCHAGUZI ALIOSHINDWA, labda yangekuwa na mantiki
   
 14. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,593
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Mh. Sumaye acha kulalama wewe ni mmoja wao umedumu ndani ya huo mfumo wa rushwa kwa miaka mingi na suala la kuwapa watoto, ndugu na jamaa zenu madaraka ndani ya CCM sio la leo, wapo waliosema mkawaambia wana wivu wa kike ila tunashukuru kama umeliona hilo, naamini uchungu wako unatoka moyoni na sio kwasababu umeshindwa NEC.

  Ombi langu kwako, badala ya kulalamika tu hembu tuonyeshe kwa vitendo jinsi gani hili suala la rushwa limekukera, TAKUKURU unapajua, namba za EDWARD HOSEA naamini unazo, unawajua kwa majina waliotoa rushwa huko Hanang, hembu waweke wazi ili nasisi tuwajue na TAKUKURU wafanye kazi yao (japo nasikia wana meno ya plastic).

  Ukizidi kulalamika na sisi wananchi tutafikiria kuwa una wivu wa kike kwa sababu wenzako wamepata ulaji unawaonea gere.
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Haya ni mashuka ya hospitali ya Chalinze jimboni kwa mkuu
   
 16. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Hivi huyu Sumaye si ndio alibatiza jina rushwa na kuiita takrima si ilikuwa kwenye utawala wake? Sasa analeta ngonjera gani ?
  CCM IMESHAKUFA IMEBAKI SIKU YA MAZISHI 2015!
   
 17. Y

  Ye Nyumbai Senior Member

  #17
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sumaye huyu huyu chini ya uongozi wa jirani yangu kule Lushoto,ndiye aliyebariki rushwa katika chaguzi akiita TAKRIMA,leo imekuwaje dhambi rushwa kumwangusha yeye? Ilikuwa takrima si rushwa!!!
   
 18. M

  Mr jokes and serious Member

  #18
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samaki mmoja akioza wote wameoza wala ata akukosea kusema hivyo ccm wote wameoza hakuna ambaye aja oza,yani hakuna kitu kibaya kama kuendekeza nafsi ukiwemo na umimi kitukibaya sana,huyu jamaa ameona wamemtenda ndio anaona makosa ya ccm,lakini tunamshukuru ndio hapo watanzania tunapata baadhi ya washuhuda wa hicho chama kujifunza kuwa chama kimeoza,lakini kunawatu wanaopindisha ukweli kuwa ccm imeoza hawa watu ndio wanaohalibu nchi hii mfano nape.
   
 19. kirumonjeta

  kirumonjeta JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 3,075
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Amesema kweli ila kama yuko serious akubali kutema dau na aje upinzani ndo tutamwelewa vinginevyo ndo walewale, wanaowekwa ccm na tamaa ya ufisadi
   
 20. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwanza huyu Sumaye amebebwa sana hakustahili ile nafasi ya uwaziri mkuu, waliombeba wametulia yeye anajaribu kusimama kwa miguu yake. Ndani ya moyo wake anayajua haya na ndio maana alienda shule Marekani labda angeweza kujipatia sifa lakini wapi imeshindikana.
  Nampa mtihani akiuweza nitamfikiria "Akemee watoto wa vigogo waliopo benki kuu kama kweli amejirudi kuwa mzalendo".
   
Loading...