Sumaye amkaanga JK

Sumaye amkaanga JK

kete za cdm kuelekea kuishika Dola zinaongezeka. 'Nawapenda' ccm. Ni greda zuri sana. Cdm tulitumie jamani
 
Sizitaki Mbichi hizi-Sumaye

Unafikiri angemshinda Merry Nagu angekuwa anapiga makelele sasa hivi? ungemkuta yupo busy tu na chama chake.

Sioni ubaya mtu kutambua ubaya wa kitu hakuna muda maalumu katika kukosoa kitu unaweza kuwa umechelewa na bado ukasema ukweli hata Kikwete alisema asipochaguliwa kupeperusha bendera ya CCM atahamia CHADEMA mbona watu hawakumsema kuwa analazimisha madaraka? alipohonga kwa rushwa Dodoma akashinda kupeperusha bendera hajaitaja tena CHADEMA mpaka leo
 
ukweli sisi wengine tunataka ukweli tu hata ukiwa wa zamani lakini utatufundisha kitu...
kuhusu kmkaanga Jk hilo liwekwe vizuri na tujue katiba inasemaje maana siku hizi mfumo wa BMW
umeshika hatamu maana ule wa kujilimbikizia vyeo unapitwa na wakati.....
Jingine Sumaye na Lowasa ni wakati wao kuonyesha uzoefu na kutoa busara zao katika mambo lakini si
kutaka uongozi wa juu tena.... maana nyakati zao zimepitwa na wakati.
wabaki kuwa washauri tu wa chama chao na si kuleta malumbano (kumbuka vita vya panzi na faida kwa kunguru)
 
Sumaye anajikaanga mwenyewe, tangu yule mama ambwage kwenye uchaguzi anaropoka hovyo tu na yeye eti anajifanya kuinga kauli za Nyerere.
 
Tooo late

Not too late bana,kwani mtu akigundua kuwa alikuwa anapaswa kufanya kitu fulani tangu jana lakini anakifanya leo na ni baada ya kugundua kosa hiyo ni too late!!?
Kuchelewa kupo kwenye uhai tu kwani ndio ambao hauwezi kurudishwa
 
62056_4772657843037_1698397433_n.jpg


Haya ni mashuka ya hospitali ya Chalinze jimboni kwa mkuu

Matambala ya kupigia deki?
 
Unajua mfungwa ujuta aliyoyatenda, na kama system haitoweza kumfanya mfungwa kutoa siri ya ubaya wake kamwe hatutotatua tatizo siku za usoni, Nafikiri tumpe moyo Sumaye aongee ya moyoni "how game played inside" mwisho wake atakuwa outsider
 
:eyebrows::eyebrows::eyebrows::eyebrows::eyebrows::eyebrows:Chadema hawana kazi nzito 2015 kwani ccm watajikaanga kwa mafuta yao wenyewe! MAKUNDI
 
Bwana Sumaye, huu sasa ni uvuvuzela.

Ulikuwa na opportunity ya ku-score points majuzi ulivofanya press conference, ukakojolea pembeni!

Keep your freaking bowl shut!!
 
WAZIRI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Frederick Sumaye, amewalipua viongozi wa sasa wa serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete kwa hatua yao ya kuruhusu baadhi ya wanafamilia wao kuwania vyeo vya juu vya uongozi.

Akiwasilisha mada kwenye mdahalo wa maadhimisho ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, jana jijini Dar es Salaam, Sumaye alisema hatua ya viongozi wengi kuandaa watoto na wake zao kwa ajili ya kuwa viongozi wa nchi, ni kinyume na katiba ya nchi, na dalili ya ubinafsi.

Katika chaguzi za sasa ndani ya CCM, Rais Kikwete ni mmoja wa viongozi waandamizi ambao familia zao zimegombea na kushinda nafasi za uongozi ndani ya jumuiya za chama hicho.

Baadhi ya watu kutoka familia ya Rais Kikwete waliojitosa katika chaguzi hizo ni pamoja na mkewe, na watoto wake wawili.

Kauli hiyo nzito ya Sumaye ni ya pili tangu alipoanguka katika kinyang’anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC Taifa, akishindwa na Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu.

Mwishoni mwa wiki, Sumaye alikaririwa akisema kuwa, kukithiri kwa rushwa ndani ya chama hicho, ndiyo sababu kubwa iliyomwangusha na kueleza hofu yake ya nchi kupata viongozi wabovu.

Aliongeza kuwa ubinafsi umekuwa chanzo kikubwa cha kukithiri kwa rushwa katika sekta mbalimbali kwa kuwa viongozi wengi wa serikali, hawako tayari kupoteza madaraka yao, hivyo hutumia rasilimali za nchi na uwezo wao wa kifedha kuwahonga wapiga kura ili waendelee kukaa madarakani, hata kama wananchi hawawataki.

“Rushwa imekithiri sehemu muhimu na mtu yeyote anayetaka kwenda Ikulu kupitia rushwa hafai. Mosi hizo fedha za kuwahonga wananchi alipata wapi? Kama amekopa anategemea Ikulu kuna hela ambazo hataweza kurudisha deni hilo?

“Chaguzi zote zimetawaliwa na rushwa moja kwa moja jambo ambalo hayati Mwalimu Nyerere alilikemea hadi mwisho wa uhai wake, na kama hatutaliangalia tatizo hilo kwa makini, kuna athari kubwa kwa taifa,” alisema.

Sumaye alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, kama Mwalimu Nyerere angefufuka leo, kusingekuwa na kiongozi wa kumlaki, badala yake watu wengine wangekuwa wa kwanza kukimbilia porini.Mbali ya ubinafsi huo, alisema uchumi wa nchi umeshikiliwa na kundi la wachache, hivyo kuzuka kwa hali ya kutojali kundi la watu masikini ambalo ni tatizo kwa taifa, kwa sababu viongozi hao wamewekeza kwa kuwajali wenye nacho ili wanufaike kama wao.

Naye Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. John Magotti, alitumia fursa hiyo kuzungumzia suala la kiwango cha elimu itolewayo nchini hususani katika shule za kata kuwa ni chachu ya kukwamisha ufaulu sanjari na ajira kwa wahitimu.

“Kuna haja ya serikali kutafuta ufumbuzi katika sekta ya elimu kabla haujaleta madhara makubwa, kwa sababu elimu bora inaendana na nafasi bora ya ajira, hivyo mwito wangu elimu inayotolewa katika shule za kata isitofautiane sana na ile ya shule za watu binafsi,” alisema Magotti.



kama anasimamia kile anachokiamini atumie utaratibu mwafaka uliowekwa na na chama chake, aje na hoja za kurestructure chama ikiwa ni pamoja na kubadili katiba ya chama ili kuleta muonekano mpya wa chama ,azunguke nchi nzima aweke mapungufu ya chama chake hadharani ili akusanye sahihi za wanachama za kutosha kufanya mabadiliko vinginevyo huo ni unafiki, wivu, na uoga, la sivyo tutaamini hakustahili kuwa waziri mkuu alikuwa kwa bahati, na uwezo waka kichwani si mkubwa kama alivyokuwa akiitwa zirooo!!
 
sumaye mnafiki leo ndio anatambua CCM wanatumia fomesheni ya BMW=Baba+mama/vimada+watoto
kuna msemo wa waswahili kuwa Nyani haoni kundule!

Amekuwa muhanga wa siasa alizozibuni analalamika. Huyu si ndio alisema ukitaka biashara zako ziende vizuri jiunge na CCM? Au amesahau yeye ndio alikaribisha rasmi biashara huko kwenye chama.
 
Sumaye anajikaanga mwenyewe, tangu yule mama ambwage kwenye uchaguzi anaropoka hovyo tu na yeye eti anajifanya kuinga kauli za Nyerere.

Amesahau yeye ndiye aliyehalalisha wafanya biashara kufanya biashara kwenye chama ili mambo yao yaende. Anywe fanya yake ya baridi roho itulie. Kelele kelele hazitabadili lolote
 
Ni lini aligundua wanafalimia wa viongozi wanawania nafasi za juu kwenye chama chake?
 
Mzee angeanza kuongea kabla ya matokeo ya uchaguzi tungemuelewa labda alizidiwa rushwa ndio analalamika sasa.
Hivi zama hizi kuna uchaguzi gani wa ccm hauna rushwa?
 
Sumaye anasema wakati wa Mwalimu alikuwa anatoa elimu bila kujali watoto wa masikini na matajiri...sasa Sumaye mbona mtoto wake wa kiume alikuwa anasoma Marekani.
 
Huyu baba ni manafiki sana, anamaanisha kwamba angeshinda CCM kusingekuwa na ufisadi siyo? Shame on his face.
 
Back
Top Bottom