Sumatra: Tunavunja mkataba leo ............... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumatra: Tunavunja mkataba leo ...............

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Dec 31, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Sumatra: Tunavunja mkataba leo Thursday, 30 December 2010 20:38

  [​IMG]Patricia Kimelemeta na Imakulata Peter
  MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesema leo itavunja rasmi mkataba wake na kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart na kueleza kuwa itafanya hivyo bila kulipa fidia yeyote.

  Kuvunjwa kwa mkataba huo kunafuatia utekelezaji wa agizo la Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu, aliyeitaka Sumatra ivunje mkataba wake na kampuni ya Majembe ifikapo Desemba 31 mwaka huu, kutokana na kampuni hiyo kukosa ufanisi.

  Nundu alisema kampuni ya Majembe imekuwa ikifanya kazi za usalama barabarani kinyume cha sheria kwa kukagua matairi, kuangalia leseni za barabara, bima taa za magari na vioo wakati hawana ujuzi wala mamlaka ya kufanya hivyo.


  Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray alisema mkataba huo utavunjwa leo kama ilivyoagizwa na waziri Nundu. Alisema Sumatra itavunja mkataba huo leo bila kulipa fidia yeyote kwani yenyewe kazi yake ni kutekeleza agizo la waziri.

  Ā“Mkabata tunauvunja kesho (leo) kama alivyoagiza Waziri na hakuna fidia wala malipo yoyote yatakayotolewa na Sumatra kwa Majembe," alisema Mziray. Kwa mujibu wa Mziray baada ya kuvunja mkataba huo Sumatra itaandaa wafanyakazi wengine kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na jeshi la polisi na Sumatra yenyewe kuhusika kikamilifu kwenye udhibiti wa daladala.

  Alibainisha, ili kukidhi matakwa ya sheria ya usalama barabarani, Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wadau wake wanatakiwa kuandaa utaratibu wa vitambulisho kwa wafanyakazi na mawakala wa kampuni binafsi ya usafirishaji ili waweze kutambulika kisheria hadi ifikapo Januari 15 mwakani.

  Hata hivyo wakati Sumatra ikisema haitailipa Majembe fidia yeyote, kampuni hiyo ya udalali mwanzoni mwa wiki hii ilisema inafanya tathmini ya hasara itakayopatikana na hatua inazoweza kuchukua kufidia hasara hiyo.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Motema Motto alilieleza gazeti hili Desemba 27 kuwa, suala hilo sasa liko kwa wanasheria wao. "Mkataba una mambo mengi na ni wakisheria,kwa sasa hatuna la kusema tunasubiri Desemba 31 Sumatra itekeleze agizo la Waziri," alisema Motto.

  Hata hviyo alisema ni dhahiri kuwa kukatishwa ghafla kwa mkataba huo, kutaiathiri kampuni ya Majembe hivyo ili kukabiliana na tatizo hilo, kampuni hiyo sasa inafanya tathmini ya hasara na kupata ushauri wa kisheria. "Agizo la waziri kutaka mkataba huo uvunjwe Desemba 31 mwaka huu, litafanya mkataba huo uvunjwe mwezi mmoja kabla ya kumalizika jambo ambalo kwa vyovyote, litailetea hasara kampuni," alisema Motto.

  Motto alisema mbali na mkataba wa Sumatra na Majembe kutakiwa kumalizika Januari 31 mwakani, kampuni hiyo pia ilikuwa kwenye mazungumzo ya kuomba iongezewa mkataba jambo ambalo limeifanya iongeze wafanyakazi zaidi.
  Wiki iliyopita Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu aliipa Sumatra siku saba kusitisha mkataba na kampuni ya udalali ya Majembe ikiwa ni njia mojawapo ya kuondoa matatizo ya usafirishaji wa abiria.

  Katika hatua nyingine, Sumatra imeandaa mikutano ya kukusanya maoni kuhusu mapitio ya nauli za mabasi ya mijini na mikoani itakayofanyika Januari 6 na Januari 7 mwakani.

  Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Mawasiliano kwa Umma ilieleza kuwa mikutano hiyo itajumuisha wadau wa sekta ya usafirishaji abiria kwa barabara, wamiliki na watumiaji wa huduma za usafiri na wananchi.

  Taarifa hiyo imesema mikutano hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam na katika mikoa mingine ya Tanzania Bara. Taarifa hiyo imesema katika mikutano hiyo viongozi wa chama cha wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani (Taboa) na |Chama cha Wamiliki wa Daladala (Darcoboa), watawasilisha mapendekezo yao kuhusu viwango vipya vya nauli.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Hapa naona harufu ya hoja ya fidia imeanza kujengwa kutoka ndani ya SUMATRA yenyewe.............DOWANS in the making?
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Hoja ya kuongeza wafanyakazi kwa matarajio ya mkataba kuongezwa haina mashiko......................biashahra ni pamoja na kubeba mzigo wa madhara yaani risks.......................

  Fidia ni ngumu kama mkataba wenyewe ulibeza sheria zilizopo...........kwa hiyo mkataba huo ni batili.........
   
 4. C

  Chagula Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :embarrassed: SUmatra ni kampuni ya nani kama sio mafisadi wezi? MAJEMBE ni kampuni ya nani kama siyo akina EPA,RICHMOND NA RADA? Haya yetu macho tutaona itafikia wapi. Je serikali inazo hela za fidia za kukata mkataba wa kisheria ghafla kabla wakati wake haujafika?
   
Loading...