Manifestation
Senior Member
- Jan 22, 2020
- 193
- 315
Umefika wakati mamlaka ya usafiri kuangalia upya namna hizi kampuni za usafiri zinavyowahudumia wateja wao. Ukiangalia kampuni kama Uber wanatoa huduma nyingi kwa dereva na abiria kwa kumuwekea bima dereva na abiria iwapo anapata ajali wakati wa safari na bei zao ni za uhakika na zinaendana na mazingira halisi ya abiria na dereva.
Ila ukija kwenye mtandao inaitwa bolt/ taxify kwanza dereva/ abiria hana bima ya kumlinda Safarini pia bei zao haziendani na uhalisia na madereva hawapewi kamisheni yoyote huku vyombo vyao vikiumia sana.
Ni vizuri SUMATRA wakaingilia kati hizi biashara na kuwe na bei elekezi kulingana na kilometers alizotembea sio mtu anatoka Makumbusho mpaka Tabata Segerea kwa Shilingi 3000.