Suluhisho la ukosefu wa Ajira Tanzania: Tuwape Wahitimu wote hii kitu "Graduate Card"

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,339
Reaction score
1,493
Habari Tanzania !

Naomba kuweka wazo langu hapa jukwaani. Nawaomba taasisi za Elimu ya kati na juu kupitia Wizara ya Elimu mkaja na hii huduma kwa hawa vijana wanaohitimu chuo hususani ngazi ya kati na juu ( Diploma & Degree holders) tuwapatie kadi maalumu kwaajili ya kupata kibali cha ajira za muda mfupi mfano miezi 9 mpaka mwaka 1 na miezi 6.

LENGO: Kuwapa uzoefu na kuwasaidia kuonyesha ujuzi na uwezo wao wa kitaaluma kwenye taasisi tutakazo wapangia kwa hicho kipindi. Hii huduma itaondoa ushindani usio na maana kwa vijana wa taifa hili na kuwapa uwezo zaidi Wizara ya Elimu na Vyuo husika kuwa na mipango endelevu na hawa wahitimu watumike kulitumikia taifa kwa kipindi kifupi huku wakisubiri ajira za kudumu ama kujiajiri.

WALENGWA/ WAHUSIKA: Hii huduma iwe maalumu kwa vijana wote ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu na kati kwa kuanzia ( Diploma & Degree ).

NAMNA YA KUPATA KADI: Hii huduma itolewe mara tu muhitimu anapomaliza elimu yake chuo husika kupitia Chuo chake (Pawepo na Muhudumu toka wizara ya Elimu kila chuo itapendeza).

MAENEO YA KUTUMIKA KADI HIZI: Huduma hii itumike taasisi zote za umma zenye upungufu wa watumishi hawa vijana waelekezwe na kupangiwa huko kwenye hayo maeneo. Pia kwa taasisi binafsi zitakazoingia mikataba na Vyuo husika na taarifa zao zitumwe Wizara ya Elimu na Wizara ya Ajira kwa utunzaji mzuri wa kumbukumbu.

MALIPO NA POSHO: Hii huduma iwe na malipo na posho maalumu ya kujikimu tu. Mfano Fedha ya Chakula, Usafiri (Nauli), Nyumba na Mavazi (Fedha hizo zikizi hizi huduma pekee).

HITIMISHO
Wahitimu wafanye kazi kwa bidii na watuletee maendeleo. Tusiwaache wazagae na elimu zao zilitumikie taifa barabara.

Hii huduma inanyika pia kwa nchi za wenzetu kama UFARANSA, AUSTRALIA NA POLAND (UHOLANZI).

Karibu.
 
Sasa mbona hapa ulichosema ni sawa na INTERN tu.

Hakuna idea mpya.
 
Hii sio hata Internship brother kama utaiangalia kwa umakini. Uwe na subirq kuna jambo jema linakuja kwa Wahitimu wote nchi nzima na utaielewa maana halisi ya hii Idea kaka.
 
Pole kwa kukosa ajira Mkuu.

Ni vizuri kuishi kwa matumaini
 
Pole kwa kukosa ajira Mkuu.

Ni vizuri kuishi kwa matumaini
Hmm !
Inamaana ukiweka wazo hapa kwaajili ya kuisaidia Jamii na Serikali katika kutatua changamoto inakuwa nongwa Afisa Jamii ?
 
Kwanza unatakiwa kujua yafuatayo:

  • Mwajiri siku siku zote anaangalia maslahi yake na siyo kuwapa watu kazi watatue matatizo yao.
  • Siku zote mwajiri anapambana kupunguza matumizi na punguzo kubwa hufanywa kwenye idara ya raslimali watu

Ukiyajua haya, utaacha kuwa na matumaini yasiyokuwepo
 
Ulichosema n internship, kitu ambacho kipo tayari kupitia taesa kwa muda wa mwaka mmoja na unapewa posho ya laki unusu kila mwezi
 
Siyo TaeSA tu hata Serikali inatoa internship hasa wizara ya afya, na kuna mwongozo tayarinwa malipo ya nusu mshahara
 
mnatoa masuluhisho ya kihuni huku mnapigana kuchukua fomu za kuteuana kwakuwa hakuna upinzani, na ukitaka kujua mwenye njaa ana dharau na wala hajli mtu angalia tamaa yule bwana aliwaambia mmalize vyuo muende VETA yeye pamoja na kwamba ana cheo na atalipwa asilimia 80 ya atakayekuwepo hadi kufa bado anaenda tena kuhangaika na ubunge, ndiomaana jiwe alikua anawaambia wawe wanaridhikaa.
 
Mbona Tanzania wanapokea kila muda Wanafunzi na Wahitimu toka Vyuo vya nchi zilizoendelea hasa kwenye maeneo kama Hospital na NGOs za hapa ndani.

Unahisi wanaletwaje hapa?
Kuna tatizo kubwa hasa hapa Tanzania la watumishi sekta zote (Umma na Binafsi). Hapa pakiwekwa vizuri kama hivi Vijana wataajirika na watapata uzoefu na wengine tutaweza watengenezea uwezo mzuri sana.
 
Siyo TaeSA tu hata Serikali inatoa internship hasa wizara ya afya, na kuna mwongozo tayarinwa malipo ya nusu mshahara
Bongo hii. Wale TAESA wanafundisha namna ya kuandika CV na siasa kibao.

Iko hivi, ukiwa na hii programme hata hao TAESA, Wizara ya Ajira, Wizara ya Utumishi na Wizara ya Elimu Database zao kuhusu Wataalamu na wahitumu zitakaa radar sana na tutakuwa na taifa la kijanja sana.
 
Ulichosema n internship, kitu ambacho kipo tayari kupitia taesa kwa muda wa mwaka mmoja na unapewa posho ya laki unusu kila mwezi
Sekta binafsi wanawasikilizia Sekta ya Umma.
Hii programme hata wewe brother ukiwa na Ofisi yako sehemu na unahitaji mtu, ni rahisi kumpata maana anakuwa anaaminika, ana elimu husika na pia utampa uzoefu katika kazi na huenda mkaingia makubaliano ukamuajiri.
 
mnatoa masuluhisho ya kihuni huku mnapigana kuchukua fomu za kuteuana kwakuwa hakuna upinzani, na ukitaka kujua mwenye njaa ana dharau na wala hajli mtu angalia tamaa yule bwana aliwaambia mmalize vyuo muende VETA yeye pamoja na kwamba ana cheo na atalipwa asilimia 80 ya atakayekuwepo hadi kufa bado anaenda tena kuhangaika na ubunge, ndiomaana jiwe alikua anawaambia wawe wanaridhikaa.
Pole sana. Tuzidi kuweka mawazo makini kwenye kujiletea maendeleo sisi wenyewe.

Tuwapende wanaotuchukia. Ama namna gani?
 
Back
Top Bottom