VETA na suluhisho la ajira kwa Walimu

VETA na suluhisho la ajira kwa Walimu

bosy

New Member
Joined
Mar 21, 2025
Posts
2
Reaction score
1
Habarini wanajamii,

Leo napenda kuwashirikisha jambo moja kuhusiana na umuhimu kwa WAHITIMU wa elimu ya juu kurudi nyuma na kutafakari kauli ya Mh. Waziri mkuu Kassim Majaliwa (Mb) aliyoitoa hivi karibuni inayotoa pendekezo kwa wahitimu wa elimu ya juu kuangalia uwezekano wa kwenda VETA kujifunza kazi za mikono.

Kauli hii imeibua mawazo tofauti katika umma wa Watanzania, wengine wakiipokea kwa mtazamo chanya na wengine wakiona kama ni kebeyi.

Kwanza kabisa ninaandika andiko hili kupongeza juhudi za serikali katika kusisitiza umuhimu wa mafunzo ya ufundi kwa wahitimu wa vyuo vikuu. Hili ni jambo la msingi katika kujenga uchumi wa taifa letu.

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam shule ya biashara mwenye shahada ya fedha (B. Com Finance), lakini nilichagua kujiajiri katika fani ya useremala. Fani inayotoa fursa nyingi za kiuchumi, ajira, na maendeleo ya ujuzi.

Kwa takriba miaka tisa sasa, nimekuwa nikiendesha Kijiji Design, kampuni changa ya kibunifu iliyo jikita katika utengenezaji wa samani endelevu.

Kupitia Kijiji Design, nimeweza kuanzisha program maalumu ya kutoa elimu ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa mafundi wa kada zote ili waweze kukuza brand zao mitandaoni na kujiongezea kipato.

Aidha nimeweza kuhusanisha biashara ya furniture na mazingira kupitia kampeni maalumu ya kupanda miti 10 kwa kila oda tunayotengeneza.

Hata hivyo, kama wahitimu wengine waliojiajiri katika sekta ya ufundi, tunakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo upatikanaji wa mtaji, vifaa vya kisasa, na mbinu endelevu na za kisasa za ufundi.

WITO KWA SERIKALI
Kwa mantiki hiyo, natoa rai kwa serikali izingatie kuunda kitengo maalumu kwa kushirikiana na vyuo vikuu; mosi, kuwatambua wahitimu wao waliopo mtaani wajue wanafanya nini. Pili baada ya kuwatambua waangalie namna ya kushirikiana na kuwashika mkono wahitimu waliopo mtaani walio chukua maamuzi ya kujiajiri ili wao wawe chachu kwa wahitimu wengine waliokata tamaa na hawajui nini cha kufanya.

MWISHO
Ninaamini kabisa kwa dhati ya fikra zangu suluhisho pekee la ajira kwa vijana nchi hii hususa wahitimu wa elimu ya juu ni serikali itazame upya njia sahihi za kuwawezesha wahitimu wa elimu ya juu walioamua kujiajiri.

Kijana mmoja akijiajiri naamini ndani ya miaka 5 ameshatengenza ajira si chini ya watu 10.
 
Hongera sana kijana kwa kujiajiri pasipo kujali Mtazamo hasi wa stadi/fundi unafanya.

Upokelewaji hasi wa taarifa ya Waziri mkuu, ukweli ni kwamba jamii imekuwa na Mtazamo hasi kwa wale wanao kwenda kusoma veta. Hivyo wengi wanaona kudharauliwa kwasababu wa naamini wanao kwenda veta ni wajinga., kitu ambacho si kweli.
Wewe ni kijana Wa mfano, naamini hadi sasa umeajiri zaidi ya vijana 10, na unamaisha swafi... Jitahidi uwahamSishe wenzio wajiongeze veta kuliko kuzub kitaa na degree zao!
 
Back
Top Bottom