SoC02 Suluhisho kwa wakulima wadogo wa miwa nchini

Stories of Change - 2022 Competition

mtozatozo

JF-Expert Member
Sep 25, 2021
459
412
UTANGULIZI

Tangu enzi za ukoloni Hadi baada ya nchi yetu kupata Uhuru kumekua na tatizo la nchi kushindwa kujitosheleza katika bidhaa muhimu ya sukari.

Sukari ni miongoni mwa bidhaa muhimu kwa matumizi ya nyumbani na viwandani pia. Ukiangalia kwa kina tatizo hili linaletwa na ukosefu wa uongozi makini na u-serious wa watawala kwa usimamizi wa mashamba ya miwa na viwanda vya sukari hapa nchini.mnyororo mzima wa uongezaji thaman kutoka miwa Hadi kua sukari unatoa bidhaa nyingine chungu mzima,ikiwemo ethanol na molasses.Lakini utajiri wote uliopo katika bidhaa hizo bado haujaleta mabadiliko chanya kwa mkulima mdogo wa chini alieko kule kilombero,mvomero,kilosa, Moshi,kagera nk.... Tanzania Ina maeneo mengi makubwa yanayofaa kwa kilimo Cha miwa inayotumika kutengeneza sukari.

Endapo pangekua na usimamizi makini kamwe pasingekua na malalamiko ya upingufu wa sukari,Wala malalamiko ya wakulima kukosa soko la mazao yao.Japokua nchi yetu haijawah kujitosheleza kwa sukari, lakin wakulima wadogo hawajawahi kunufaika na deficit hiyo.

Tutakumbuka ktk utawala wa awamu ya tatu,chini ya rais Benjamin William mkapa kulikua na ubinafsishaji wa mashirika ya umma pamoja na viwanda vyilikokua chini ya milki ya serikali.hiyo ilileta matumaini makubwa kwa wakulima wadogo na wananchi kwa ujumla kuhusu suluhisho la masoko ya mazao yao kwa wawekezaji hao ambao kwa asilimia kubwa walikua ni wafanyabiashara kutoka nje ya nchi,lkn haikua km watu wengi walivyodhani kwani ugumu wa soko bado ulikuepo palepale licha ya jitihada kubwa kwa wawekezaji hao kujaribu kupanua uwekezaji wa viwanda vya sukari.

Ktk awamu ya tano chini ya rais John Pombe Joseph Magufuli,palikua na jitihada kubwa pia wa kuhamasisha uwekezaji wa viwanda pamoja na kujaribu kufufua vile vilivyoonekana kufa au kusuasua ktk uzalishaji....hapo palifunguliwa mashamba mapya makubwa ya miwa yakiwemo ya mbigili na bagamoyo sugar kujaribu kuziba pengo la upungufu wa sukari na kuepuka uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi, lakin suluhisho la wakulima wadogo dhidi ya uhakika wa soko la miwa haukupatikana. Wakulima wameendelea kuteseka na matatizo mbalimbali ktk kipindi chote tangu matayarisho ya mashamba hadi utunzaji wake, kwani miongoni mwa changamoto wanazopitia ni pamoja na kuombwa rushwa na viongozi wao wa vyama vya ushirika pindi miwa yao inapokomaa ili wavuniwe na kuuzwa kwa wawekezaji wenye viwanda.changamoto nyingine kubwa ni ukosefu wa bima kwenye kilimo hiki.

Kwani karibu kila mwaka kumekua na ajali za moto kwenye mashamba ya wakulima hao wadogo,ambapo maelfu kwa maelfu ya ekari za mashamba ya miwa huungua eitha kwa hujuma,au kwa bahati mbaya.Inapotokea mkulima/wakulima wakaunguliwa mashamba yao,hakuna fidia yoyote kutoka kwenye vyama vya ushirika au mwekezaji mwenye kiwanda,hivyo basi gharama zote tangu maandalizi ya shamba(kulima, harrow,rija,kupanda,palizi Mara mbili Hadi tatu, kupiga dawa za kuulia magugu, mbolea ya kupandia na kukuzi)zote hizo hua ni hasara kwa mkulima

Pia baada ya janga hilo la moto usiotarajiwa, mkulima atalazimika kuikata miwa hio ilioungua na kuitupa nje ya shamba na kujiandaa tena kwa gharama nyingine za msimu unaofuata. Ukiangalia mlolongo wote huo wa gharama ambao mkulima mwisho wa yote anapata hasara kubwa bila faida yoyote, kwani wengi wao huwezeshwa gharama hizo kwa mikopo yenye riba toka kwa taasisi za fedha zilizo rasmi na zisizo rasmi hivyo mkulima mwisho wa msimu anabaki kwenye lindi kubwa la umasikini na madeni yasiyolipika.

Kutokana na tabu zote na madhila ambayo mkulima huyu masikini anayapitia,tena bila matumaini ya suluhisho la moja kwa moja kwa matatizo hayo ya kila mwaka,ipo namna ya kumfuta machozi mkulima huyu na kumsahaulisha tabu zote alizopitia tangu enzi na enzi za ukulima wake wa zao hilo


SULUHISHO:
Zipo juice mbalimbali zinazozalishwa kwa matunda mbalimbali toka ndani na nje ya nchi yetu... miongoni mwazo ni juice ya embe,nanasi,machungwa,tufaa,matunda mchanganyiko na kadhalika.Lakini pamekosekana juice halisi iliosindikwa na kufungashwa itokanayo na miwa.kwa miaka ya hivi karibuni juice ya miwa imejizolea umaarufu mkubwa Sana hususani jijini Dar Es Salaam.

Lakini maandalizi ya utengenezaji na mazingira ya uuzaji wa juice hiyo yamekua sio safi na salama katika maeneo mengi ambapo biashara hiyo inafanyika.Pamekua na ombwe la juice ilioandaliwa kiwandani na kua-packed tayari kwenda sokoni(kwenye supermarket,maduka ya kawaida na hata nje ya nchi)Wazo nililonalo kama likifanikiwa kupenya kwenye jamii,litaleta mapinduzi makubwa sana,hasa kumpa uhakika mkulima huyu mdogo wa miwa popote alipo.

Uhakika wa soko la mazao yake, kwani hatolazimika tena kuendelea kumtegemea mnunuzi mmoja tu ambae ni mwekezaji wa kiwanda Cha sukari,hapo tutamuongezea wigo wa machaguo ya soko aamue wapi akauze miwa yake.pia demand ya miwa itaongezeka hivyo kuongeza pia Bei ya miwa kwa mkulima kwani kutakua na ushindani kati ya wanunuzi, tofauti na hali halisi ilivyo sasa kwani bei ya miwa ya mkulima mdogo haipangwi na soko,bali mwekezaji wa kiwanda Cha sukari, na mkulima hana namna yoyote ya kukwepa ukandamizaji huo kwani hakuna sehemu nyingine anaweza kupeleka miwa yake, Lakini sio miwa pekeyake, kwani juice ya miwa huchanganywa na kiungo muhimu cha tangawizi,hivyo kupanua soko pia la wakulima wa tangawizi japo mlengwa mkubwa hapa ni mkulima wa miwa.Tafiti zinaonyesha miwa hii itumikayo kutengeneza sukari ni bora zaid kwa juice kuliko ile iliozoeleka sokoni,kwani kiwango chake cha utamu (saclos)ni kikubwa Mara dufu zaid ya miwa ya kawaida,pia kumekua na uwekezaji mkubwa wa tafiti na gunduzi mbalimbali za aina mpya chotara za miwa ambayo ni bora zaidi.

Zipo namna mbili za uwekezaji wa viwanda hivi vya juice ya miwa.Moja ni viwanda vidogovidogo katika maeneo mbalimbali yenye wakulima kwa wingi,miwa inaweza kukamuliwa huko na maji yake kusafirishwa hadi mahali patakapokua na kiwanda kikubwa kwajili ya packaging.Pia kuna uwezekano kwa wawekezaji wengi kuweka viwanda kamili katika maeneo yote yenye wakulima hao,ambapo mchakato mzima tangu kukamua hadi ufungashaji utafanyika hapo na kusafirisha bidhaa iliyo tayari kwa matumizi kwenda moja kwa moja kwa mtumiaji wa mwisho yaani sokoni.

Mchakato mzima wa uongezaji thaman kutoka miwa Hadi kua juice kutaleta msisimko wa kiuchumi kutoka kwa mkulima, wafanyakazi mbalimbali kwanzia wa mashambani hadi kiwandani,pia biashara hii itawezesha serikali kuongeza wigo wa mapato yake, kwani wawekezaji hawa wapya watakua walipa kodi pia,vilevile itaimarisha afya miongoni mwa wanajamii, kwani tafiti zinaonyesha unywaji wa juice ya miwa husafisha vizuri mfumo wa haja ndogo na kusaidia mtiririko mzuri wa damu miilini mwetu.mwisho kabisa nakushukuru sana wewe uliotumia muda na bando lako kupitia andiko hili.

Nikuombe kwa dhati kabisa unipigie kura ili andiko hili lishinde ktk shindano la story of change la mwaka huu.
 
Back
Top Bottom