Ikiwa ni takribani saa 48 tu baada ya Chadema kuibua tuhuma za kuwepo kwa sukari ya magendo iliyofichwa katika maghala 7 ya mbolea katika mji mdogo wa Makambako polisi kwa kushirikiana na TRA na TAKUKURU wamekamata zaidi ya tani 1000 za sukari inayodaiwa, narudia tena inayodaiwa kuwa ni mali ya Mbunge wa Njombe Kaskazini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa ndugu Deo Sanga (Jah People). Aidha usafirishaji wa sukari hiyo unadaiwa kufanywa kwa kutumia yale magari ambayo Mtikila na Dr Slaa walidai kuwa yanamilikiwa na Ridhiwan Kikwete.
Akihutubia katika mkutano wa Chadema uliofanyika katika viwanja vya polisi makambako, mwana chama wa Chadema bwana Thomas Nyimbo aliibua tuhuma nzito huku akiwahusisha vigogo wa CCM (bila kuwataja majina) na tuhuma hiyo ya kuficha sukari katika ghala la mbolea. Nasisitiza tena katika ghala la mbolea ndimo sukari ilimochanganywa na mbolea.
Akiongea kwa kujiamini Thomas Nyimbo aliwaambia polisi, Takukuru na Usalama wa Taifa waliokuwepo kwenye mkutano huoyupo tayari kuongoza nao kwenda kufanya ukaguzi kwenye maghala hayo hata wakati huo wa mkutano huo.
Hata hivyo kabla vumbi la tuhuma hizo halijatulia leo Polisi, Takukuru na TRA kutoka Makambako, Njombe na Iringa wamezingira maghala hayo na kuthibitisha uwepo wa sukari kiasi kilichotajwa hapo juu ikiwa imechanganywa na mbolea.
Tukio hili linafuatia sakata la mwaka 2007 ambapo katika maghala hayo yaliyopo jirani na njia ya Makambako- Mbeya kulikamatwa sukari na mashine ya kuchapa mifuko ya sukari inayodaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha katika kiwanda cha sukari cha kilombero- Mkoani Morogoro. Kesi iliyofunguliwa dhidi ya mfanya biashara aliyehusishwa na tukio la wakati huo liliyeyuka katika mazingira yasiyoeleweka mpaka leo.
Aidha tukio hili linakuja wakati ambao maisha ya wananchi yakiwa yanapanda kila siku huku sukari hiyo inayodaiwa kuwa ya magendo toka nchini Malawi ikiwa imehifadhiwa kwenye ghala la mbolea. Hawa ndio viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza lakini wameamua kutulisha hata mbolea kwa ajili ya kushibisha matumbo yao na familia zao. Kweli Rais Kikwete anayo kazi kwani Mbunge / Mwenyekiti wa CCM Mkoa ni kiongozi aliyetakiwa kuwa mfano na mstari wa mbele katika kumsaidia Mwenyekiti wake
Tutaendelea kuwajuza kitachoendelea.
Chanzo: Mimi mwenyewe