Sukari ya magendo yakamatwa ghala la Mbolea Makambako- Mbunge na vigogo wa CCM wahusishwa

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Ikiwa ni takribani saa 48 tu baada ya Chadema kuibua tuhuma za kuwepo kwa sukari ya magendo iliyofichwa katika maghala 7 ya mbolea katika mji mdogo wa Makambako polisi kwa kushirikiana na TRA na TAKUKURU wamekamata zaidi ya tani 1000 za sukari inayodaiwa, narudia tena inayodaiwa kuwa ni mali ya Mbunge wa Njombe Kaskazini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa ndugu Deo Sanga (Jah People). Aidha usafirishaji wa sukari hiyo unadaiwa kufanywa kwa kutumia yale magari ambayo Mtikila na Dr Slaa walidai kuwa yanamilikiwa na Ridhiwan Kikwete.
Akihutubia katika mkutano wa Chadema uliofanyika katika viwanja vya polisi makambako, mwana chama wa Chadema bwana Thomas Nyimbo aliibua tuhuma nzito huku akiwahusisha vigogo wa CCM (bila kuwataja majina) na tuhuma hiyo ya kuficha sukari katika ghala la mbolea. Nasisitiza tena katika ghala la mbolea ndimo sukari ilimochanganywa na mbolea.
Akiongea kwa kujiamini Thomas Nyimbo aliwaambia polisi, Takukuru na Usalama wa Taifa waliokuwepo kwenye mkutano huoyupo tayari kuongoza nao kwenda kufanya ukaguzi kwenye maghala hayo hata wakati huo wa mkutano huo.
Hata hivyo kabla vumbi la tuhuma hizo halijatulia leo Polisi, Takukuru na TRA kutoka Makambako, Njombe na Iringa wamezingira maghala hayo na kuthibitisha uwepo wa sukari kiasi kilichotajwa hapo juu ikiwa imechanganywa na mbolea.
Tukio hili linafuatia sakata la mwaka 2007 ambapo katika maghala hayo yaliyopo jirani na njia ya Makambako- Mbeya kulikamatwa sukari na mashine ya kuchapa mifuko ya sukari inayodaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha katika kiwanda cha sukari cha kilombero- Mkoani Morogoro. Kesi iliyofunguliwa dhidi ya mfanya biashara aliyehusishwa na tukio la wakati huo liliyeyuka katika mazingira yasiyoeleweka mpaka leo.
Aidha tukio hili linakuja wakati ambao maisha ya wananchi yakiwa yanapanda kila siku huku sukari hiyo inayodaiwa kuwa ya magendo toka nchini Malawi ikiwa imehifadhiwa kwenye ghala la mbolea. Hawa ndio viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza lakini wameamua kutulisha hata mbolea kwa ajili ya kushibisha matumbo yao na familia zao. Kweli Rais Kikwete anayo kazi kwani Mbunge / Mwenyekiti wa CCM Mkoa ni kiongozi aliyetakiwa kuwa mfano na mstari wa mbele katika kumsaidia Mwenyekiti wake
Tutaendelea kuwajuza kitachoendelea.
Chanzo: Mimi mwenyewe
 
Kama ni kweli, hawa jamaa wa magamba wametuteka nyara (hostage). Yaani tunalalamika sukari bei juu, wao wameihodhi na kuuza kidogo kidogo ili kupata faida. Matatizo ya waTZ ni faida kubwa kwao
 
mungu wangu jamani ccm na jk munaona sasa? Alafu mtuambie eti chadema wana udini tuwaepuke kwendeni zenu uko mnatufilisi alaffu na kutulaza njaa alafu mnasema chadema ni wabaya tutawapenda chadema daima na nchi hii lazima waichukue kwa nguvu zetu sisi wananchi hyo aina mjadala sukari inapanda bei kumbe nyie mnaficha wanafiki wakubwa eti mnajivua magamba? Lazima huyo mbunge na huyo gamba ccm lazima wawajibike
 
hata mohammed dewji ndiyo mchezo wake,hapa ninapo post gari za moetl zipo malawi zinapakia sukari.ccm wananuka rushwa!
 
hawa kilichobaki ni kuwapiga mawe tu ili magamba yatoke vizuri hawana adabu hakuna hata mmoja aliemsafi yote mijizi
 
hata mohammed dewji ndiyo mchezo wake,hapa ninapo post gari za moetl zipo malawi zinapakia sukari.ccm wananuka rushwa!
Nakubaliana na wewe kwa 100%.. Sakata la mwaka 2007 lililomhusisha mmiliki wa Durban Lodge pale Makambako ildaiwa sukari ile ilikuwa inatoka Malawi na kupelekwa Singida kusaidia yatima na Dewji alitajwa. Maskini kumbe ilikuwa ni magendo. Jk alijifanya kutuma kikosi kupitia IGP walipogundua ni wafadhili wao wakaufyata mpaka leo. This country bwana
 
Niliwashauri na narudia kuwashauri ndugu zangu Watanzania kwamba inabidi tumtangaze Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ni 'Janga la Kitaifa'
 
Ikiwa ni takribani saa 48 tu baada ya Chadema kuibua tuhuma za kuwepo kwa sukari ya magendo iliyofichwa katika maghala 7 ya mbolea katika mji mdogo wa Makambako polisi kwa kushirikiana na TRA na TAKUKURU wamekamata zaidi ya tani 1000 za sukari inayodaiwa, narudia tena inayodaiwa kuwa ni mali ya Mbunge wa Njombe Kaskazini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa ndugu Deo Sanga (Jah People). Aidha usafirishaji wa sukari hiyo unadaiwa kufanywa kwa kutumia yale magari ambayo Mtikila na Dr Slaa walidai kuwa yanamilikiwa na Ridhiwan Kikwete.
Akihutubia katika mkutano wa Chadema uliofanyika katika viwanja vya polisi makambako, mwana chama wa Chadema bwana Thomas Nyimbo aliibua tuhuma nzito huku akiwahusisha vigogo wa CCM (bila kuwataja majina) na tuhuma hiyo ya kuficha sukari katika ghala la mbolea. Nasisitiza tena katika ghala la mbolea ndimo sukari ilimochanganywa na mbolea.
Akiongea kwa kujiamini Thomas Nyimbo aliwaambia polisi, Takukuru na Usalama wa Taifa waliokuwepo kwenye mkutano huoyupo tayari kuongoza nao kwenda kufanya ukaguzi kwenye maghala hayo hata wakati huo wa mkutano huo.
Hata hivyo kabla vumbi la tuhuma hizo halijatulia leo Polisi, Takukuru na TRA kutoka Makambako, Njombe na Iringa wamezingira maghala hayo na kuthibitisha uwepo wa sukari kiasi kilichotajwa hapo juu ikiwa imechanganywa na mbolea.
Tukio hili linafuatia sakata la mwaka 2007 ambapo katika maghala hayo yaliyopo jirani na njia ya Makambako- Mbeya kulikamatwa sukari na mashine ya kuchapa mifuko ya sukari inayodaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha katika kiwanda cha sukari cha kilombero- Mkoani Morogoro. Kesi iliyofunguliwa dhidi ya mfanya biashara aliyehusishwa na tukio la wakati huo liliyeyuka katika mazingira yasiyoeleweka mpaka leo.
Aidha tukio hili linakuja wakati ambao maisha ya wananchi yakiwa yanapanda kila siku huku sukari hiyo inayodaiwa kuwa ya magendo toka nchini Malawi ikiwa imehifadhiwa kwenye ghala la mbolea. Hawa ndio viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza lakini wameamua kutulisha hata mbolea kwa ajili ya kushibisha matumbo yao na familia zao. Kweli Rais Kikwete anayo kazi kwani Mbunge / Mwenyekiti wa CCM Mkoa ni kiongozi aliyetakiwa kuwa mfano na mstari wa mbele katika kumsaidia Mwenyekiti wake
Tutaendelea kuwajuza kitachoendelea.
Chanzo: Mimi mwenyewe

du jah people mbona anaonekana ni mtu mwenye heshima kubwa!
 
halafu cha ajabu tbc1 hawaleti hizi habari pumbavu zao,sasa ipo haja ya kuchukua vijana wa tarime na kuwasambaza wilaya zote tanzania bara ili watufundishe ujuzi wa kutumia kombeo kwaajjili ya kurushia mawe hawa wezi hapo ndio tutaheshimiana nadhani.
PIPOZ POWERRRRRRRR
 
siku zote sina imani na Deo Kasenyenda Sanga@ Jah People juu ya nia thabiti ya kuwakilisha wananchi katika kutatua kero zao na kuwaletea maendeleo. ni mfanyabiashara aliyejipenyeza ktk siasa ili tu afanye biashara zake chafu kwa mwavuli wa ubunge. ccm wanashangaza sana,lkn pia wananchi waamke sasa, wasichague mtu kisa amewagawia kanga na ti shirt ama kutoa mabati kuezeka darasa moja la shule
 
Mwenye macho hambiwi tazama,jungu kuu halikosi ukoko.tutakipenda daima chama cha wachaka.
 
Mnaoendela kufikiria kwamba Tanzania chini ya CCM itatoka kwenye umaskini licha ya mali asili kama wananyama, milima, madini, arithi, watu tulionao ni kujidanganya.

Ni mara ngapi tumepiga kelele hadi makoo kuuma tukidai kwamba CCM ni viongozi karibu wote ni wezi, mafisadi, siyo waaminifu, wanatumia madaraka yao kujitajirisha wao ni siyo taifa na kwamba umaskini wetu umechangiwa kwa zaidi ya 95% na chama hiki fithuli !

Tanzania haina "future" kama tutaendelea kuikumbatia CCM na viongozi wake Corrupt !
 
du jah people mbona anaonekana ni mtu mwenye heshima kubwa!
Kwani Rostam Aziz, Chenge, Mramba, Liyumba, Kikwete, Nimrod Mkono na wengineo hawana heshima kubwa? Ana heshima kubwa kwa nani? Yule Mkuu IMF hakuwa na heshima kubwa? Nini kimetokea? Humfahamu Jah People wewe!
 
Sina wasiwasi juu ya hili, sukari hii ni mojawapo ya zinazoingilia mbambabay-mbinga-songea-makambako?
 
Tunashukuru kwa taarifa ingawa ni nzito kuipokea kwa vile inaumiza sana, kwani zile lugha za biashaa ya magendo na misamiati kama MAGENDO leo hii kwenye utawala huu dhalimu tunazisikia. Hapa naamini kuwa Azimio la Arusha limekufa na kuoza. Tujipe pole watanzania na tuwe wavumilivu kwa kuwa hawa viongozi tunawachagua sisi wenyewe. Inauma sana!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom