Sugu aelezea sakata la ndege ya Rais wa China

Sugu aelezea sakata la ndege ya Rais wa China

Sugu+Prof J kihama cha ccm
Hawa jamaa ni mpango wa mungu ili vijana wa tz wajue majukumu ya serekali yao!
 
Labda mimi sielewi maana ya hoja nzito. Toka lini uzushi ukawa ni hoja nzito? Waziri Membe amekanusha kwamba kitu cha namna hiyo kilitokea, kama ambavyo wizara ya Mambo ya Nje China ilivyokanusha vikali. Kati ya wote wanaoeneza uvumi huu na hata ile documentary, hakuna hata sehemu moja inayoonyesha kwamba Meno yalionekana yakipakizwa kwenye ndege ya Rais. Hakuna kati ya wapiga kelele anayesema kwamba kweli ndani ya zile diplomatic bags waliona meno. Nchi hii tumebaki kuwa watu wa kufurahia kusikia kashfa hata pale ambapo haipo. Hawa wameanza kufanya uchunguzi huu muda mrefu na wana weledi wa kutosha. Eti wakasubiri mwaka mmoja na nusu kulipua bomu hilo na hasa baada ya ziara ya mafanikio ya Rais huko China. Watanzania wana akili ya kujua kwamba hapa kuna siasa zinachezwa na kile ambacho wenzetu huko magharibi wanakiratibu vizuri kuonyesha kwamba China ni adui wa Afrika, as if wao ni wema na marafiki. hawa ambao wamekuwa wakipora rasilimali kwa karne nyingi na kutuachia mashimo. Hatudanganyiki!

wewe ndiyo una piga siasa, mafanikio yapi? Kama huwezi kutawala mafanikio huna tofauti yule unayemzodoa hapo juu.be objective kwa mafanikio
 
Msalani kweli umeshindwa kuona mantiki iliyo katika ujumbe wa Sugu?
Kuna kauliza humu kuwa Membe anajua kila kilichokuwa katika diplomatic bags za ujumbe wa China?
Kwa nini unajitoa fahamu kiasi hiki?

MIGNON;
Usimwonee Msalani. Ili uwe shabiki wa ccm lazima kwanza uwe na sifa mbili: 1. Utoe kabisa akili yako umwachie mkeo au mmeo, weye uende tupu bila fikira yeyote. 2. Unjue kusema hapana tu hata ukiulizwa nani jina lako, weye sema HAPANA.
Kwa maisha hayo ukiyaweza, utakula na kunywa mpaka uvimbiwe. Umesikia hayo ya Bandari?? Huwezi amini kama si kichaa. 800 million per day mtu anajiandikia allowance bado Mwakyembe anacheka cheka tu. Maccm, mhhhhhhhh
 
sugu kichwa...kwa hoja hyo bado usemi wa mnyka una nguvu kuwa.''tumefikia umaskn huu kwa juhud za ccm.''..mnaomponda sugu wote..ACHENI UKALE(CONSERVATISM)
 
Binafsi hata sijaona lamaana alilosema SUGU

Kwa kawaida kuelimika kunasaidia sana kuwa na uwezo mpana wa kuelewa. Nailaumu CCM kwa sera zake kufanya watu wengi kukosa elimu, na kutumia ujinga wao ili kuwatawala milele.
Ova
 
Hizi hoja mfu za kuipaka matope serikali yetu haziwezi kuachwa zitambe.

Wazalendo tutasimama kidete kuhakikisha hakuna Nyau yeyote anafanikiwa katika mpango huu haramu.

Nadhani we we ata ukikuta mke wako Ana....fi...lwa na jibaba lilovalia sare za ccm utasimama kidete kulisia kwamba limefanya kazi nzuri
 
Hizi hoja mfu za kuipaka matope serikali yetu haziwezi kuachwa zitambe.

Wazalendo tutasimama kidete kuhakikisha hakuna Nyau yeyote anafanikiwa katika mpango huu haramu.

Nadhani we we ata ukikuta mke wako Ana....fi...lwa na jibaba lilovalia sare za ccm utasimama kidete kulisifia kwamba limefanya kazi nzuri
 
· UCHUNGUZI WA KIMATAIFA UFANYIKE YAWEZEKANA RAIS WA CHINA HAJUI
· MTASIKIA WATU WAMENYONGWA CHINA SABABU SISI HATUCHUKUI HATUA

Mh. Joseph Mbilinyi “Sugu” ameitaka serikali kuchunguza kuhusu tuhuma zilizotolewa na Televisheni ya Al-Jazeera kuhusu sakata linalohusu tuhuma za kuwa ndege ya Rais wa China ilihusika kusafirisha pembe za ndovu kwa kushirikiana na maofisa wa Ikulu. Huku akisisitiza kuwa humu ndani mnasema kuna watu wanaichonganisha serikali na wananchi ila mchawi wa CCM ni CCM yenyewe kwa mambo yanayofanyika kila siku.

Watanzania wa sasa hivi sio wale, wa sasa hivi wanajua kinachoendelea wanaelewa inamaanisha nini wakiona Televisheni ya Al jazeera inapoonyesha kuwa ndege ya Rais wa China pamoja na maofisa wa Ikulu wameshiriki kusafirisha pembe za ndovu. Mbunge huyo amemtaka waziri wa mambo ya nje aache kukurupuka na kutolea majibu kuwa shutuma hizo ni uzushi badala yake wafanye uchunguzi sababu mtu amehojiwa bila kificho anaelezea kwa namna gani wanavyoshirikiana na Wachina katika kusafirisha pembe za ndovu na wanatoa ushahidi wa meno ya ndovu bila kificho.

Sugu akasisitiza kuwa Waziri anasema “Rais wa China kaja alifanya saa ngapi shopping”, Mbunge Mbilinyi akahoji yaani inamaanisha Rais wa China aende vinyagoni Mwenge kufanya shopping? Wanasema ile ziara ndiyo imetumika yawezekana ukakuta Rais mwenyewe wa China ajui kuwa ndege yake ilihusika kusafirisha pembe za ndovu mkifanya uchunguzi mtasikia kuna watu wamenyongwa China, sababu sisi hatuwezi kuchukulia hatua watu wetu

kwa mfano mara ya kwanza tulisema kuhusu meli ya Kinana watu wakapiga kelele leo tunaambiwa ndege ya Rais wa China. Ripoti inasema uchunguzi ulifanyika kwa miaka kumi halafu waziri Membe anasimama na kusema kuwa wazungu wameleta uzushi, akasema “kwa nini wazungu wakisema Rais wetu ni kinara wa utawala bora Waziri Membe asemi ni uzushi?” alihoji.

Alitakiwa aje na kusema inatakiwa ufanyike uchunguzi wa Kimataifa tujue ukweli na kama tukigundua Ripoti ni ya uongo, Tanzania kama nchi tuchukue hatua kwa wale waliotuchafua haswa ikichukuliwa taarifa imetolewa na vyombo vikubwa vya habari kama BBC na AL JAZEERA, kufanya mambo ya maendeleo inabidi tushirikishe wananchi na wananchi wanavyokatishwa tamaa na taarifa kama hizi wanashushwa moyo wa kufanya shughuli za maendeleo.

Ahsante Sugu.
 
Binafsi hata sijaona lamaana alilosema SUGU

Kuna madaktari wa macho wa kujitolea wanakuja tarehe 12 nov 14 ktk hospitali ya Irembura njombe kwa ajiri ya uchunguzi wa macho na operation ya kutibu upofu! Tumia fulsa hii, then utaweza kuchangia mada za humu!
 
nchi hii wengi ni mbumbu ndo watu wanafanya wanavyotaka
 
Mafanikio tunayo yaoni ni piki za kichina na vifo na majeruh kibao pale moi muhimbili vilema wanaongezeka tu hizo ndio faida za wa china
 
Back
Top Bottom