Sugu aelezea sakata la ndege ya Rais wa China

Sugu aelezea sakata la ndege ya Rais wa China

mkitaka mambo yaharibike anzisheni tu hako kauchunguzi afu muone moto utakaomuwakia BABA RIZ.. mmesahau kale kamkataba alikopiga na chinese PRESIDANTOO?? kuokoa mafigisu ya MTOTOO???
· UCHUNGUZI WA KIMATAIFA UFANYIKE YAWEZEKANA RAIS WA CHINA HAJUI
· MTASIKIA WATU WAMENYONGWA CHINA SABABU SISI HATUCHUKUI HATUA

Mh. Joseph Mbilinyi “Sugu” ameitaka serikali kuchunguza kuhusu tuhuma zilizotolewa na Televisheni ya Al-Jazeera kuhusu sakata linalohusu tuhuma za kuwa ndege ya Rais wa China ilihusika kusafirisha pembe za ndovu kwa kushirikiana na maofisa wa Ikulu. Huku akisisitiza kuwa humu ndani mnasema kuna watu wanaichonganisha serikali na wananchi ila mchawi wa CCM ni CCM yenyewe kwa mambo yanayofanyika kila siku.

Watanzania wa sasa hivi sio wale, wa sasa hivi wanajua kinachoendelea wanaelewa inamaanisha nini wakiona Televisheni ya Al jazeera inapoonyesha kuwa ndege ya Rais wa China pamoja na maofisa wa Ikulu wameshiriki kusafirisha pembe za ndovu. Mbunge huyo amemtaka waziri wa mambo ya nje aache kukurupuka na kutolea majibu kuwa shutuma hizo ni uzushi badala yake wafanye uchunguzi sababu mtu amehojiwa bila kificho anaelezea kwa namna gani wanavyoshirikiana na Wachina katika kusafirisha pembe za ndovu na wanatoa ushahidi wa meno ya ndovu bila kificho.

Sugu akasisitiza kuwa Waziri anasema “Rais wa China kaja alifanya saa ngapi shopping”, Mbunge Mbilinyi akahoji yaani inamaanisha Rais wa China aende vinyagoni Mwenge kufanya shopping? Wanasema ile ziara ndiyo imetumika yawezekana ukakuta Rais mwenyewe wa China ajui kuwa ndege yake ilihusika kusafirisha pembe za ndovu mkifanya uchunguzi mtasikia kuna watu wamenyongwa China, sababu sisi hatuwezi kuchukulia hatua watu wetu

kwa mfano mara ya kwanza tulisema kuhusu meli ya Kinana watu wakapiga kelele leo tunaambiwa ndege ya Rais wa China. Ripoti inasema uchunguzi ulifanyika kwa miaka kumi halafu waziri Membe anasimama na kusema kuwa wazungu wameleta uzushi, akasema “kwa nini wazungu wakisema Rais wetu ni kinara wa utawala bora Waziri Membe asemi ni uzushi?” alihoji.

Alitakiwa aje na kusema inatakiwa ufanyike uchunguzi wa Kimataifa tujue ukweli na kama tukigundua Ripoti ni ya uongo, Tanzania kama nchi tuchukue hatua kwa wale waliotuchafua haswa ikichukuliwa taarifa imetolewa na vyombo vikubwa vya habari kama BBC na AL JAZEERA, kufanya mambo ya maendeleo inabidi tushirikishe wananchi na wananchi wanavyokatishwa tamaa na taarifa kama hizi wanashushwa moyo wa kufanya shughuli za maendeleo.
 
Labda mimi sielewi maana ya hoja nzito. Toka lini uzushi ukawa ni hoja nzito? Waziri Membe amekanusha kwamba kitu cha namna hiyo kilitokea, kama ambavyo wizara ya Mambo ya Nje China ilivyokanusha vikali. Kati ya wote wanaoeneza uvumi huu na hata ile documentary, hakuna hata sehemu moja inayoonyesha kwamba Meno yalionekana yakipakizwa kwenye ndege ya Rais. Hakuna kati ya wapiga kelele anayesema kwamba kweli ndani ya zile diplomatic bags waliona meno. Nchi hii tumebaki kuwa watu wa kufurahia kusikia kashfa hata pale ambapo haipo. Hawa wameanza kufanya uchunguzi huu muda mrefu na wana weledi wa kutosha. Eti wakasubiri mwaka mmoja na nusu kulipua bomu hilo na hasa baada ya ziara ya mafanikio ya Rais huko China. Watanzania wana akili ya kujua kwamba hapa kuna siasa zinachezwa na kile ambacho wenzetu huko magharibi wanakiratibu vizuri kuonyesha kwamba China ni adui wa Afrika, as if wao ni wema na marafiki. hawa ambao wamekuwa wakipora rasilimali kwa karne nyingi na kutuachia mashimo. Hatudanganyiki!
 
mkitaka mambo yaharibike anzisheni tu hako kauchunguzi afu muone moto utakaomuwakia BABA RIZ.. mmesahau kale kamkataba alikopiga na chinese PRESIDANTOO?? kuokoa mafigisu ya MTOTOO???
Ndo mnataka kwa uchafu huu mtu akae kuujadili na kupoteza rasilimali. Kamwe nchi hii haitaonja maendeleo mpaka kizazi hiki kinachoishi kwa kushikana uchawi kitakapoondoka.
 
Nilivyoona thread yenyewe ameandika sugu sikujisumbua kusoma yote najua ni uharo tu.kweli duniani kuna watu
 
Watanzania tusichulie Kashifa hii kijuu juu. Tujiulize kwa nini leo? Imeshapita miezi Kazaa Kuna jambo nyuma ya pazia ambalo tunapaswa kulitathimini dhidi ya agenda za kuuchafua utaifa wetu dhidi ya fikra dharimu za ukoloni mamboleo juu ya mustakabali wa nchi na sera yetu ya mambo ya nchi za nje. Kwa nini leo? Tuache siasa na kama Kuna jambo lenye tatizo tuangalie namna sahihi ya kuyashughurikia si kushabikia kila jambo linalofanywa au kusemwa na mzungu. WAZUNGU WAPO KULINDA MASLAHI YAO WANA POONA YAPO HATARINI.

kwa hiyo mchina yupo kulinda maslahi yenu watanzania?
 
Ndo mnataka kwa uchafu huu mtu akae kuujadili na kupoteza rasilimali. Kamwe nchi hii haitaonja maendeleo mpaka kizazi hiki kinachoishi kwa kushikana uchawi kitakapoondoka.

Sio kitakapoondoka.. sema TUTAKAPOONDOKA UKIWEMO NA WEWE MLUGALUGA
 
Kwani kuwa mfuasi wa ccm ni lazima uitetee serikali? Hata kama hoja ina mashiko?
 
Kwani kuwa mfuasi wa ccm ni lazima uitetee serikali? Hata kama hoja ina mashiko?

Hizi hoja mfu za kuipaka matope serikali yetu haziwezi kuachwa zitambe.

Wazalendo tutasimama kidete kuhakikisha hakuna Nyau yeyote anafanikiwa katika mpango huu haramu.
 
habari za jioni wakuu. Sugu amekuja na swaga gani leo?
 
Siku zinavyokwenda utakuja kufirwa ndg yng, sasa unataka kubadili njano kuwa nyekundu, mbona u ccm unawazidi kipimo, acheni ujinga, kila kitu ni kupinga tu, hizo posho mnazopewa zitawa cost one day

Nahisi huu uzi ume tembea na ban za kutosha tu...
 
· uchunguzi wa kimataifa ufanyike yawezekana rais wa china hajui
· mtasikia watu wamenyongwa china sababu sisi hatuchukui hatua

mh. Joseph mbilinyi “sugu” ameitaka serikali kuchunguza kuhusu tuhuma zilizotolewa na televisheni ya al-jazeera kuhusu sakata linalohusu tuhuma za kuwa ndege ya rais wa china ilihusika kusafirisha pembe za ndovu kwa kushirikiana na maofisa wa ikulu. Huku akisisitiza kuwa humu ndani mnasema kuna watu wanaichonganisha serikali na wananchi ila mchawi wa ccm ni ccm yenyewe kwa mambo yanayofanyika kila siku.

Watanzania wa sasa hivi sio wale, wa sasa hivi wanajua kinachoendelea wanaelewa inamaanisha nini wakiona televisheni ya al jazeera inapoonyesha kuwa ndege ya rais wa china pamoja na maofisa wa ikulu wameshiriki kusafirisha pembe za ndovu. Mbunge huyo amemtaka waziri wa mambo ya nje aache kukurupuka na kutolea majibu kuwa shutuma hizo ni uzushi badala yake wafanye uchunguzi sababu mtu amehojiwa bila kificho anaelezea kwa namna gani wanavyoshirikiana na wachina katika kusafirisha pembe za ndovu na wanatoa ushahidi wa meno ya ndovu bila kificho.

Sugu akasisitiza kuwa waziri anasema “rais wa china kaja alifanya saa ngapi shopping”, mbunge mbilinyi akahoji yaani inamaanisha rais wa china aende vinyagoni mwenge kufanya shopping? Wanasema ile ziara ndiyo imetumika yawezekana ukakuta rais mwenyewe wa china ajui kuwa ndege yake ilihusika kusafirisha pembe za ndovu mkifanya uchunguzi mtasikia kuna watu wamenyongwa china, sababu sisi hatuwezi kuchukulia hatua watu wetu

kwa mfano mara ya kwanza tulisema kuhusu meli ya kinana watu wakapiga kelele leo tunaambiwa ndege ya rais wa china. Ripoti inasema uchunguzi ulifanyika kwa miaka kumi halafu waziri membe anasimama na kusema kuwa wazungu wameleta uzushi, akasema “kwa nini wazungu wakisema rais wetu ni kinara wa utawala bora waziri membe asemi ni uzushi?” alihoji.

Alitakiwa aje na kusema inatakiwa ufanyike uchunguzi wa kimataifa tujue ukweli na kama tukigundua ripoti ni ya uongo, tanzania kama nchi tuchukue hatua kwa wale waliotuchafua haswa ikichukuliwa taarifa imetolewa na vyombo vikubwa vya habari kama bbc na al jazeera, kufanya mambo ya maendeleo inabidi tushirikishe wananchi na wananchi wanavyokatishwa tamaa na taarifa kama hizi wanashushwa moyo wa kufanya shughuli za maendeleo.

huu ndio uzi kamili pamoja na kichwa cha habari ajabu kichwa cha habari kimewekwa na story ya kutunga jf punguzeni kuchakachua....
 
Utaonaje bila kufungua MACHO??!!!

Eti OLESAIDIMU kipofu anasikia watu wanamsifia mrembo aliyepita mahali hapo halafu yeye anaponda kuwa wala si mzuri kitu wakati hata giza hawezi kuliona! Si maajabu hayo?
 
Last edited by a moderator:
Sugu1 [pambano.jpg
 
hoja za Sugu ni nzito ila vichaa hawawezi mwelewa hata siku moja
wewe kigori..
kila kitu unatafsiri kinyume, yaani sugu ndio mzima na wengine ndio vichaaa?????!!!!!!!!
huu ni zaidi ya utani we dada. au ni kwa sababu mumeo anakuendea kinyume ndio maana unatafsiri mambo kinyume!!
 
Wonderfully yaani taarifa ya uchunguzi uliofanyika kwa muda wa miaka kumi na kupata airtime ya kutosha kwenye vyombo kama aljazila bbc we una simama kwa dakika zisizozidi therathini halafu kwenye bunge la tanzania aisee kweli kituko hapa hata hatuhitaji akili ya chuo kikuu kujua uwezo wa viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom