SUGU, achana na Muziki!

Wapiga kura wake hawakumchagua kwa kigezo cha muziki

Una haki ya kushauri kama ulivyofanya katika post ya kwanza lakni pia pima point za wanaochangia na sio tu kutaka mwisho wa siku uone kuwa hoja yako ndo zaidi, binafsi naamini shughuli ya muziki haiathiri utendaji wa huyu bwana, na umesema aache kujitangaza kupitia muziki,sidhani kama SUGU anajitangaza kwa sasa,SUGU anafahamika TZ hii kuliko hata watendaji wengi tu wa ngazi za juu serikalini
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.

wanamwita SUGUUUU....WANAKWITA SUGUUUU,,,,,SU.....SU..,.SUGU....
AAAAA MBONA WANAKATAAA,,,,,,MBONA WANAKATAAAAA.....SUGU NI MVUA AKIAMUA KUNYESHA ANANYESHA
 
Nadhani unamwonea mtoa hoja!
Muziki ni biashara kama biashara zingine!
Mtu anapokubali kuwa kiongozi anapaswa kuacha biashara zake zote na kuwawakilisha wananchi!
Ndio maanza tunashangaa mawaziri na wabunge wanaoendelea kufanya biashara na kuwasahau wananchi!
Tunawashangaa wanapoenda kwenye mabenki na kupata mikopo mikubwa mikubwa na kufungua biashara.
Watanzania tubadilike.
Wabunge waache biashara.
mawaziri waache biashara.
Acheni kung'ang'ania tenda! Waacheni wengine wafanye!
Ninyi mmekuwa viranja kuangalia ushindani wa haki.

Hata Sugu aache matamasha ya biashara, ili awawakilishe wananchi na wanamziki wote bila upendeleo.
Baada ya ubunge anaweza kuamua kurudi.

Ila kama ni matamasha ya kuelimisha jamii (sio biashara) hatuna haja ya kumpigia kelele.

Lakini inategemea anafanya hivyo kwa kusudio gani. Angalia, Shwaznegar alikuwa Seneta wa state mojawapo Marekani, lakini aliendelea kucheza Filamu zake kama kawaida. Hata Mr George Bush.Junior akiwa President wa Marekani, alicheza Filamu moja hive ya " Attempt to Kill the President". Nae ni member wa Holywood. Haya mambo ni taalima. Tunataka wale Wabunge ambao ni Madaktari angalao siku momja moja waende Mahoosipitali wakatibu watu. Wale ambao ni Waalimu wa Vyuo vikuu wakatoe Lectures mavyuoni...Hii itasaidia sana kusukuma maendleo.
 
Muziki, Siasa na Maisha havitengemani!

Bila Muziki asingekuwa Sugu na bila (u)Sugu asingkuwa mbunge!

Waziri mkuu mmoja huko Ulaya ya kati ambaye ni mwanasoka hadi mwanzoni mwa mwaka huu alikuwa bado anacheza na alikuwa anagombea kuwa mchezaji bora wa nchi hiyo na alifanikiwa kupata taji hiyo!

Nadhani mengi ya Matamasha yake Sugu kwa sasa huyafanya kama Charity!

Conception ya uongozi katika nchi hii ni hovyo sana toka katika kuchagua na outcome za mbunge, watu hutegemea kuwa mtu anapochaguliwa uongozi huleta maendeleo kwa maana ya material dvt, huu ni uvivu mkubwa wa kufikiri. Juzi nimeangalia ITV kipindi cha ahadi ni deni na nikamwona Mbunge wa Bukene akijinadi namna alivyoleta maendeleo kwa kugawa mipira soksi n.k, katika hotuba hiyo yote haku acknowledge hata mara moja kuwa kuna kitu kinaitwa Mfuko wa Jimbo...

Maelezo yake yote hayo ilionekana kana kwamba pesa hata za kupauwa choo ilitoka mfukoni mwake! Uongo huu wa viongozi wetu unatokana na sisi kujitumbukiza katika wimbi la kudhani kuwa ni kazi ya Mbunge kutoa pesa mfukoni na kufanya shughuli za maendeleo katika jimbo husika!

Nashukuru katika kipindi hicho hicho Peter Msigwa nae alizungumza na kila mara alisema kuwa Fedha za mfuko wa jimbo zimetumika kufanya suala hili na lile!

Kazi kuu ya Mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali! Mkuu peremende mnazoletewa huko na kudhani ni maendeleo ni danganya toto na umajinuni wa kisiasa!

Kama alivyosema EMT hapo juu, There is more in life than politics!

Huyo mwanasiasa wa ulaya aliendelea kuwa mchezaji wa timu gani?
Kinachotakiwa ni wabunge na mawaziri kuacha kufanya kazi mbili!
Ubunge/uwaziri na biashara, sio kuacha fani!

Kama anaalikwa na wenzake kwenda kutumbuiza, hiyo haina neno.
Ila kama anaandaa na kutafuta pesa za kuandaa matamasha, sidhani kama atapata muda wa kuwatumikia wananchi kwa haki.

Kazi aliyopewa ni zaidi ya muziki. Yeye anawakilisha wananchi wa fani zote, wakulima na wafanyakazi.
Mshika mbili lazima moja itamponyoka.

Chama kinamhitaji, wananchi wanamhitaji na huo muda wa kufukuzana na matamasha unatoka wapi?
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.

'yamenikuta mzee mwenzangu mpaka najuta,,,,kiama chao ama changu,,,ama zao ama zangu,ukiishi kwa upanga na utakufa kwa upanga,,,,mungu ndo anapanga kila kitu kwa kila mtu,,,,heri nife maisha haya,,,dunia sio mbaya walimwengu ndo mabaya,wanakufatafata kila jambo,HAWAKAWII FULANI ANA HIV,WANATANGANZA HIVIHIVI,,,,,,'ENZI ZA MR II HIZO
 
Na ziendelee kuwa ENZI ZAKE....
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.

Hoja yako nzuri sana ila hawajaielewa.
Mbunge kuendelea na kazi yake ya zamani wakati anawawakilisha wananchi sio sawa!
Ukiwa mbunge unapaswa kusoma mambo mengi sana ili upate hoja.
Unapaswa kupitia hoja za zamani, hata miaka 20 iliyopita!
Unapaswa kupitia sheria mbalimbali zilizowahi kupitishwa!
Unahitaji kujua kinachoendelea duniani kote!
Bado unahitaji kuwatembelea wananchi ujue matatizo yao na namna ya kuwasaidia
Tena wabunge wengi wanawakilisha maeneo makubwa ambayo hata ukiamua kutembelea kijiji kimoja kwa mwezi hutaweza.
Bado amepangiwa majukumu ya kamati za bunge!

Huyu mbunge mwenye shughuli nyingi kiasi hiki anawezaje kuwa mfanyabiashara, kiongozi wa kanisa au msikiti, kuwa mkulima au mwanamziki maarufu wakati mmoja?

Au ndio maana wengine wanamaliza miaka 5 hawajauliza hata swali moja?
 
haya ni mawazo finyu. wanasiasa wanashauriwa kuacha biashara kutokana na shughuli yenyewe kuwa na conflict of interest na majukumu sasa huyu anaimba ili achangie maendeleo jimboni sioni conflict of interest iko wapi hapa. fikiri kwanza kabla ya kutoa maoni yako. sasa unataka sugu akaibe ndio atekeleze ahadi zake? au yeye ana uwezo kama wa musa wa kulisha wana wa Israeli?
Nadhani unamwonea mtoa hoja!
Muziki ni biashara kama biashara zingine!
Mtu anapokubali kuwa kiongozi anapaswa kuacha biashara zake zote na kuwawakilisha wananchi!
Ndio maanza tunashangaa mawaziri na wabunge wanaoendelea kufanya biashara na kuwasahau wananchi!
Tunawashangaa wanapoenda kwenye mabenki na kupata mikopo mikubwa mikubwa na kufungua biashara.
Watanzania tubadilike.
Wabunge waache biashara.
mawaziri waache biashara.
Acheni kung'ang'ania tenda! Waacheni wengine wafanye!
Ninyi mmekuwa viranja kuangalia ushindani wa haki.

Hata Sugu aache matamasha ya biashara, ili awawakilishe wananchi na wanamziki wote bila upendeleo.
Baada ya ubunge anaweza kuamua kurudi.

Ila kama ni matamasha ya kuelimisha jamii (sio biashara) hatuna haja ya kumpigia kelele.
 
Pro-Chadema JF jitokezeni Jumapili Mbagala DAR LIVE mkamsaidie Sugu.
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.

Sugu ni Competetor wako nini?
 
Mtoa mada,funguka zaidi.
Ushauri wa kuacha mziki unaweza kuwa mzuri, lakini Je afanye nini Kama mbadala?

Kabla ya kutoa ushauri wako,unamfahama mheshimiwa Man Pakiyao, ambaye ni Mbunge na Bondia mshuhuri?
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.

'hapo zaman hapo zamani,mambo mengi yalikua safi,,,,kinyume na sasa kinyume na sasa,,,mambo mengi yamebadilikaaaaaaaa'
 
haya ni mawazo finyu. wanasiasa wanashauriwa kuacha biashara kutokana na shughuli yenyewe kuwa na conflict of interest na majukumu sasa huyu anaimba ili achangie maendeleo jimboni sioni conflict of interest iko wapi hapa. fikiri kwanza kabla ya kutoa maoni yako. sasa unataka sugu akaibe ndio atekeleze ahadi zake? au yeye ana uwezo kama wa musa wa kulisha wana wa Israeli?

Maendeleo yanaletwa kwa kuhimiza watu wafanye kazi kwa bidii, la sivyo wabunge wote waanze kutafuta HELA HUKU NA HUKO HATA IKIWEZEKANA KUFANYA BIASHARA ILI TU KUCHANGIA MAENDELEO.
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.

Bangee mbaya sana,kama ulikua ujui ilo tamasha ni kwa ajiri ya kuchangia ujenzi wa shelu kwenye jimbo lake na pili mziki ndio kazi yake nyingine ni sawa na kumwambia tundu lissu aache uanasheria aendelee na siasa tu,stuka wewe reloy!
 
Back
Top Bottom