SUGU, achana na Muziki!

Nenda Mbeya au waaulize wanambeya wanasemaje juu ya Sugu kufanya muziki? Binafsi naunga mkono sugu kuendelea na muziki na ningependa wasomi na hasa waalimu wa vyuo vikuu na madaktari kuendelea kufundisha hii itawapa maisha ikitokea wananchi wanaamua kuwapa watu wengine nafasi ya ubunge.

Hayo ni maoni yako
 
wana mwita sugu nani?? wana mwita sugu nani?? wana mwita sugu sugu sugu,,sugu kiboko wa mabitozi
 
Ushauri butu sana huu. Mbona hujawaambia madaktari, walimu, wafanyabiashara waliojazana CCM kuwa waachane na biashara au ualimu au qualifications zao kwa kuwa tu wamechaguliwa kuwa wabunge?. Nilitaka nisichangie hii thread lakini tunaambiwa kuwa unapoona upotoshaji ni lazima usahihishe. Reframe your thread to have a great thinkers spices.

Nadhani unamwonea mtoa hoja!
Muziki ni biashara kama biashara zingine!
Mtu anapokubali kuwa kiongozi anapaswa kuacha biashara zake zote na kuwawakilisha wananchi!
Ndio maanza tunashangaa mawaziri na wabunge wanaoendelea kufanya biashara na kuwasahau wananchi!
Tunawashangaa wanapoenda kwenye mabenki na kupata mikopo mikubwa mikubwa na kufungua biashara.
Watanzania tubadilike.
Wabunge waache biashara.
mawaziri waache biashara.
Acheni kung'ang'ania tenda! Waacheni wengine wafanye!
Ninyi mmekuwa viranja kuangalia ushindani wa haki.

Hata Sugu aache matamasha ya biashara, ili awawakilishe wananchi na wanamziki wote bila upendeleo.
Baada ya ubunge anaweza kuamua kurudi.

Ila kama ni matamasha ya kuelimisha jamii (sio biashara) hatuna haja ya kumpigia kelele.
 
sugu ni hopeless eti atakua na tamasha mbeya! ana dhalilisha ubunge wake,lazima tukubali mtu kuwa mbunge ni kiongozi,yani sugu ameshindwa kupata hela ya maendeleo kwa jimbo hadi aimbe!

Bora yeye anaeimba anapata pesa kwa maendeleo ya jimbo kuliko wezi mafisadi wanaoiba pesa za walala hoi mpaka tunarudishiwa chenchi
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Haule a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.


Acha kudesa kijinga weye, kama kitu hujui si bora uulize ili ujuzwe? Mh Sugu haitwi Joseph Haule, anaitwa Joseph Mbilinyi kwa faida yako ya baadaye, Joseph Haule ni Profesa J mzee wa mitulinga.
 
I know what you mean.Lakini sasaaa,siasa sio kazi,hasa siasa hizi uchwara za Tanzania.Nadhani pamoja na siasa,angebuni kitu kingine cha kufanya just incase he is out of politics.Mziki ni aibu tupu,ni noma!
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Haule a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.
 
SUGU ni muhuni na jimbo hapa mbeya ndio bye bye!
atalisoma kwenye magazeti,hakuna alichofanya mpaka leo.
yaani sijui anawaza nini? labda b**ngi.
 
Ntombi kila siku! Mtoa mada amekurupuka, by the way sugu habahatushi kuimba, its his talent, so hawezi acha talent yake kwa wazo la mtu mmoja kama huyo.
 
Umekosa kazi ya kufanya?

Fikiria tena!
Maige alipokuwa alipojenga nyumba ya kifahari kwa biashara yake (anadai yeye) mlimpigia kelele!
Akiwa busy na matamasha ya Muziki atawatumikiaje wananchi?
Unaonaje kila kiongozi tunayemlipa mshahara angefanya kazi alliyopewa.
Tungekuwa masikini?
Wabunge wangekuwa na shida ya kujua matatizo ya majimbo yao?
Chunguza ratiba za wabunge kwenye majimbo yao, uone wanawafikia wananchi kwa asilimia ngapi!
Tuwe mifano ya kuigwa!
 
Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Haule a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.
unahangaika sana
 
Kwani muziki anaimba kila siku, kwani Sugu alitoa ahadi gani kwa wananchi?

Hujui Muziki unahitaji maandalizi?
Muda wa kuwatumikia wananchi wewe unaupeleka kuandaa Muziki?
No wonder mawaziri wa JK wanafungua biashara na kujenga magorofa, maana hawafanyi biashara kila siku!
 
Muziki, Siasa na Maisha havitengemani!

Bila Muziki asingekuwa Sugu na bila (u)Sugu asingkuwa mbunge!

Waziri mkuu mmoja huko Ulaya ya kati ambaye ni mwanasoka hadi mwanzoni mwa mwaka huu alikuwa bado anacheza na alikuwa anagombea kuwa mchezaji bora wa nchi hiyo na alifanikiwa kupata taji hiyo!

Nadhani mengi ya Matamasha yake Sugu kwa sasa huyafanya kama Charity!

Conception ya uongozi katika nchi hii ni hovyo sana toka katika kuchagua na outcome za mbunge, watu hutegemea kuwa mtu anapochaguliwa uongozi huleta maendeleo kwa maana ya material dvt, huu ni uvivu mkubwa wa kufikiri. Juzi nimeangalia ITV kipindi cha ahadi ni deni na nikamwona Mbunge wa Bukene akijinadi namna alivyoleta maendeleo kwa kugawa mipira soksi n.k, katika hotuba hiyo yote haku acknowledge hata mara moja kuwa kuna kitu kinaitwa Mfuko wa Jimbo...

Maelezo yake yote hayo ilionekana kana kwamba pesa hata za kupauwa choo ilitoka mfukoni mwake! Uongo huu wa viongozi wetu unatokana na sisi kujitumbukiza katika wimbi la kudhani kuwa ni kazi ya Mbunge kutoa pesa mfukoni na kufanya shughuli za maendeleo katika jimbo husika!

Nashukuru katika kipindi hicho hicho Peter Msigwa nae alizungumza na kila mara alisema kuwa Fedha za mfuko wa jimbo zimetumika kufanya suala hili na lile!

Kazi kuu ya Mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali! Mkuu peremende mnazoletewa huko na kudhani ni maendeleo ni danganya toto na umajinuni wa kisiasa!

Kama alivyosema EMT hapo juu, There is more in life than politics!
 
Kwan. Mama lwakatale ameacha uchungaji?

Hili ni swali zuri sana!
Huu ndio mzizi wa umaskini wetu!
Mtu anaomba kazi, akipewa haifanyi anaendelea na shughuli zake kama kawaida!
Wabunge wengi wanafanya biashara zao, hawawakilishi wananchi!
This should be questioned, indeed!
 
Biashara na Siasa ni Kama Mlenda na Pilau, Muziki ni Biashara. Kwa hiyo Muziki na Siasa pia ni kama Mlenda na Pilau.
 
Mawazoyako ni mgando,


Sioni haja ya Mbunge wa Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuendelea kujitangaza kwa matamasha mbalimbali ya Muziki.

Ninadhani umefika wakati kwa yeye kujikita katika siasa na utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Mbeya mjini.
 
Back
Top Bottom