Subra. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Subra.

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Globu, Dec 21, 2011.

 1. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Subra ni nguzo mama ya kuishi duniani. Subra ni jambo jema, analipenda Manani. Subra huwa daima ni funguo ya amani. Subra ni fimbo njema ya kumpiga shetani. Subra chanzo cha neema kwa viumbe duniani. Subra funguo njema ya kuingia peponi. Subra ikiwa huna, rafiki yako shetani. Subra bila imani haikukai moyoni. Subra ikikutoka unakuwa mashakani. Husababisha hasama kwa ndugu na majirani. MAASALAM.
   
Loading...