Subira yavuta kheri, ni kweli?

NYAMUHANZI

Senior Member
Apr 7, 2017
187
388
Habari waheshimiwa!!

Toka nimekuwa na kujitambua nimekuwa nikisikia huu usemi kuwa "subira yavuta heri" usemi huu nimeusikia si mara moja bali mara nyingi na sehemu tofauti na pia hutumiwa na watu wa rika tofauti kuanzia watoto, vijana, watu wazima hadi wazee na vikongwe.

Binafsi mimi naona kuwa MUNGU hawezi kuwapa heri watu wanaosubiri (wasiofanya chochote) na wakabaki kusubiri miujiza yake wakati alishawapa nguvu za mwili na nguvu za akili ambazo wanapaswa kuzitumia kutatua changamoto zinazowakabili maishani. Ndiyo maana kuna usemi unasema kuwa "sala bila matendo ni sala mfu (yaani hakuna kitu) hii inamaanisha kuwa MUNGU huwasaidia wanaojituma

Na kuna usemi mwingine wa wawindaji wanasema ukiwa porini unafukuzwa na simba au mnyama yoyote mkali unatakiwa kumuomba MUNGU huku ukikimbia yaani "MUNGU na mbio". Kwa mawazo yangu haya nahisi walioanzisha huu usemi walikuwa ni watu wavivu, wasiopenda kujituma na wenye kuombaomba.

Je, ninyi wakuu mnaonaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom